Shule ambazo mtoto anashinda siku nzima shuleni kama watu wazima kazini ni hatari kwa future ya mtoto zama hizi

Shule ambazo mtoto anashinda siku nzima shuleni kama watu wazima kazini ni hatari kwa future ya mtoto zama hizi

Nakubaliana nawe 💯, watoto lazima wawe na muda wa kujifunza stadi za maisha au life skills. Sisi watoto wa zamani tunajua vitu vingi, hata nikikosa ajira najua kulima, kufuma vitambaa, kuimba, kusuka etc, sitakosa shughuli ya kufanya. Mtoto wa sasa hv hajui hata unga wa ugali unapatikanaje? Hata mashine ya kukoboa na kusaga hajawai kuiona, hatari sana. Wakirudi home wako hoiii, homework,kulala duu, hatari sana kwa taifa la kesho
 
Yaani huwa kila siku nasema , ningekuwa na mtoto anasoma ningegombana sana na walimu kuhusu tuition za jioni na weekend za hapa DSM.

Haiwezekani mwanafunzi wa primary awe busy kuliko hata wanachuo

Shule ndio zinalazimisha tuisheni ili zipate faida ya pesa zaidi
 
Shule ambazo mtoto anaenda asubuhi na anarudi jioni saa 11 ama saa 12 jioni sio nzuri kwa future ya mtoto.

Mtoto anapaswa atoke shuleni mapema. Ili awe na muda wa kujifunza skills za mtaani

Siku ya mtoto haipaswi kuishia kujifunza ya shuleni tu, anapaswa apate muda wa kujifunza extracurricular skills Mtoto acheze mpira na watoto wenzake mtaani nje ya shuleni .,

mtoto apate muda wa kujifunza kuimba iwe kwaya kanisani ya watoto ama kujifunza kupiga vyombo vya muziki kama kinanda, saxophone, drums etc, mtoto apate muda wa kujifunza kuigiza mtaani,

kama kuna waigizaji unaishi nao jirani waombe ama walipe wawafundishe wanao kuigiza mapema.

Mtoto ajifunze kupika, kupamba, kuongea mbele za watu wengi. Hivi vitu vitamsaidia kuliko masomo ya shuleni .

Jiulize why International school of Tanganyika watoto wanatoka saa saba tu mchana?

Jiulize why nchi zilizoendelea shule zao watoto wanatoka shuleni mapema?

UKWELI MCHUNGU ZAMA HIZI MAISHA YAMEBADILIKA SANA. ELIMU HAITAMSAIDIA MTOTO WAKO KWENYE FURSA ZA KIMAISHA KAMA HAJUI VITU KAMA NILIVYOVITAJA NA VINGINE VINGI
Daah! Hili sijui nani atatunasua utoto umekuwa mateso zama hizi tofauti na zamani
 
Huku finland masomo yanaanza saa tatu asubuhi yanaisha saa nane mchana. Na hakuna kutoa homeworks. Mtoto anaenda nyumbani kupumzika.
Huu ni utaratibu mzuri sana.

Japokuwa hata masaa ma3 yangetosha kabisa kukaa shule kwa mtoto.

Mtoto anaamka alfajiri anarudi jioni.

Yaani mtoto anatoka mapema nyumbani kuliko baba yake mtafutaji,na anachelewa kurudi nyumbani kuliko baba yake mtafutaji.

Kwa maana rahisi ni kwamba mtoto anatoka mwanzo nyumbani na anarudi mwisho.

MToto anahitaji muda mwingi wa kucheza michezo mbalimbali na wenzake kama mpira,kutengeneza magari,kombolela,kuogelea,kuwinda(kama ni mjini) na michezo mingine mingi.

Nakumbuka utoto wangu tulikuwa mahodari sana kutengeneza magari ya udongo na watu,tena tulikuwa jumamosa na jumapili ile kula basi ni kwa kulazimishwa kwa sababu ya ile passion ya mambo tunayoyafanya.

Ila sasa hivi watoto ndio wanaisubiri kula kwa sababu hawana cha kufanya,wapo bored hakuna kitu cha kuwasisimua ubongo wao mpaka wakasahau kula chakula,matokeo yake tunapata watoto wengine wavivu kabisa.

Wanangu nitawapeleka shule ambazo hawasomi sana na wala hakuna ujinga wa tuisheni,ukileta mambo ya tuition maana yake shule yako haitimizi wajibu.

Kimisngi kabisa maisha ya zamani ndio yalikuwa na makuzi sahihi yenye kujenga ubongo na uwezo wa mtoto kufikiri.

Mambo ya shuleni ni kujifunza mawazo ya wwengine wakati huo katika uhalisia mtoto anahitaji kujifunza mambo mengine mengi kama vile tabia,nidhamu ya matumizi,kudhibiti hisia zake,kujijua mwenyewe,kuwajua watu wengine,kujifunza kutoka kwa wazazi n.k

Mtoto anakaa masaa 12 shuleni .

Anarudi nyumbai analala saa4 usiku jivyo anakaa na wazazi masaa kama ma4 tu.

Then analala masaa 6.

Hivyo mtoto anapata masaa ma4 tu ya kukaa na wazazi tena masaa ma4 hayo pengine mzazi yuko bize hana hata muda wa kuongea na kucheza na watoto na kuwafundisha vitu kadhaa,hivyo mtoto anapoteza ile muunganiko wa uzazi na wazazi wake.

Mtoto anapotumia masaa 10-12 shuleni kwenye jengo moja na madawati hakuna wanachojifunza hapo zaidi ya kulishana ujinga na tabia mbovu.

Wangetumia masaa 12 hayo kucheza na kujichanganya mtaani kufanya vitu mbalimbali basi tungekuwa na watoto bora kabisa

Nina mengi ya kuandika ila tuishie hapo na nitahakikisha wanangu nawalea katika mifumo niliyolelewa mimi.
 
Huko mtaani mnapotaka watoto wakachangamane kupo salama?
Kwani Huko shule nako kupo salama ?

Kuna matukio kibao ya watoto kulawitiana mashuleni vyooni,na unafahamu matukio haya.

Juzi kati tu hapa kuna Nchi siikumbuki watoto wamemnyanyasa mwenzao kingono SHULENI na kumuingiza vijiti mpaka akazimia,je unadhani shule pia ni salama sio ?

kama ishu ni usalama wa mtoto basi tuwafungie ndani tu wasiende popote.

Tunataka afya ya akili ya mtoto huku tukiwafundisha namna ya kujikinga na hatari.

Hakuna pahala salama kwa 100%.

USalama wa kweli sio kuondoa mambo hatari,bali ni kuundaa mwili na akili kuwa na skills za kukabiliana na hatari hizo.

Hatari haziishi duniani.

Sawa tuondoe tunazoziweza ila zipo ambazo zitakuja automatically hata uzuie vipi.

Tuwaandae watoto wetu
 
Mkuu upo sahihi kabisa, ila kwa mazingira yetu Africa na malezi yetu,
Mtoto akiwa na muda mwingi hivo wa kuwa free wengi hutumbukia kwenye vitu vibaya kama umalaya na makundi mengine kwa wanaume,

Mfano wako umeuweka kishua sana, ila huku kwetu mtoto akitoka shule saa 10 atabaki alone home hadi saa 1 at least wazazi wanaporudi, sasa huo muda watoto wetu wengi huku mtaani ndio wanafanya upuuzi mwingi, hizo sijui kuimba au kuigiza mara computer bado ipo kwa % chache sana ya watu,

Ombi langu, shule ziwe na extra curricular activities nying sana huko huko shuleni,
Watoto wajifunze kuimba, kucheza, kugarden huko huko shulen, hii mitaa ya Kiafrica ukisema et mtoto aje ajifunzie mtaani % kubwa wataharibika tu
 
Nakubaliana nawe 💯, watoto lazima wawe na muda wa kujifunza stadi za maisha au life skills. Sisi watoto wa zamani tunajua vitu vingi, hata nikikosa ajira najua kulima, kufuma vitambaa, kuimba, kusuka etc, sitakosa shughuli ya kufanya. Mtoto wa sasa hv hajui hata unga wa ugali unapatikanaje? Hata mashine ya kukoboa na kusaga hajawai kuiona, hatari sana. Wakirudi home wako hoiii, homework,kulala duu, hatari sana kwa taifa la kesho
Sema watu wa zamani mnajipaga maujiko sana ,😂😂😂😂 mngekuwa kweli mna hizo skills mnazodai mnazo nchi hii isingelia ukosefu wa ajira na pia wengi wenu mngekuwa na maisha ya juu kiuchumi, ila hamna kitu,

Acheni kujisifia sana vijana wa zamani, mnataka kila kitu kinachofanyika now kionekane kinakosewa inabidi kifanyike ka enz zenu wakat hakikuleta matunda yeyote yale ya maana
 
Kwani Huko shule nako kupo salama ?

Kuna matukio kibao ya watoto kulawitiana mashuleni vyooni,na unafahamu matukio haya.

Juzi kati tu hapa kuna Nchi siikumbuki watoto wamemnyanyasa mwenzao kingono SHULENI na kumuingiza vijiti mpaka akazimia,je unadhani shule pia ni salama sio ?

kama ishu ni usalama wa mtoto basi tuwafungie ndani tu wasiende popote.

Tunataka afya ya akili ya mtoto huku tukiwafundisha namna ya kujikinga na hatari.

Hakuna pahala salama kwa 100%.

USalama wa kweli sio kuondoa mambo hatari,bali ni kuundaa mwili na akili kuwa na skills za kukabiliana na hatari hizo.

Hatari haziishi duniani.

Sawa tuondoe tunazoziweza ila zipo ambazo zitakuja automatically hata uzuie vipi.

Tuwaandae watoto wetu
Ni kweli shule hakuko salama 100% ila ukicompare na mtaani, shuleni ni salama sanaaaaaa,
Mnataka watoto wawahi kurudi wakati huo hup wazazi mnarudi home saa 1-3 usiku, watoto wakae alone saa 10-3 usiku, 🤔 wengi wataharibikiwa
 
kwa ambao wana wake wa nyumbani na ndugu waaminifu muda wote hawa ndio idadi kubwa ya watz ilipo.

Hivyo hao unaowasema wewe ni wachache sana hapa tanzania kwa msingi huo shule sio sehemu salama kwa asilimia kubwa ya watoto wa tanzania.
 
Shule ambazo mtoto anaenda asubuhi na anarudi jioni saa 11 ama saa 12 jioni sio nzuri kwa future ya mtoto.

Mtoto anapaswa atoke shuleni mapema. Ili awe na muda wa kujifunza skills za mtaani

Siku ya mtoto haipaswi kuishia kujifunza ya shuleni tu, anapaswa apate muda wa kujifunza extracurricular skills Mtoto acheze mpira na watoto wenzake mtaani nje ya shuleni .,

mtoto apate muda wa kujifunza kuimba iwe kwaya kanisani ya watoto ama kujifunza kupiga vyombo vya muziki kama kinanda, saxophone, drums etc, mtoto apate muda wa kujifunza kuigiza mtaani,

kama kuna waigizaji unaishi nao jirani waombe ama walipe wawafundishe wanao kuigiza mapema.

Mtoto ajifunze kupika, kupamba, kuongea mbele za watu wengi. Hivi vitu vitamsaidia kuliko masomo ya shuleni .

Jiulize why International school of Tanganyika watoto wanatoka saa saba tu mchana?

Jiulize why nchi zilizoendelea shule zao watoto wanatoka shuleni mapema?

UKWELI MCHUNGU ZAMA HIZI MAISHA YAMEBADILIKA SANA. ELIMU HAITAMSAIDIA MTOTO WAKO KWENYE FURSA ZA KIMAISHA KAMA HAJUI VITU KAMA NILIVYOVITAJA NA VINGINE VINGI
Maisha yamebadilika kila nyanja! Wee mwachieachie mtoto wako ajichanganye eti kumjengea kujiamini sijui mambo gani mwisho wa siku atakuja kaishatolewa marinda, mimba, bangi, matusi! Umri wa mtoto mpaka miaka 18 ni shule! Hayo ya mtaani ajifunze akiwa kaishajitambua!
 
Back
Top Bottom