Huku finland masomo yanaanza saa tatu asubuhi yanaisha saa nane mchana. Na hakuna kutoa homeworks. Mtoto anaenda nyumbani kupumzika.
Huu ni utaratibu mzuri sana.
Japokuwa hata masaa ma3 yangetosha kabisa kukaa shule kwa mtoto.
Mtoto anaamka alfajiri anarudi jioni.
Yaani mtoto anatoka mapema nyumbani kuliko baba yake mtafutaji,na anachelewa kurudi nyumbani kuliko baba yake mtafutaji.
Kwa maana rahisi ni kwamba mtoto anatoka mwanzo nyumbani na anarudi mwisho.
MToto anahitaji muda mwingi wa kucheza michezo mbalimbali na wenzake kama mpira,kutengeneza magari,kombolela,kuogelea,kuwinda(kama ni mjini) na michezo mingine mingi.
Nakumbuka utoto wangu tulikuwa mahodari sana kutengeneza magari ya udongo na watu,tena tulikuwa jumamosa na jumapili ile kula basi ni kwa kulazimishwa kwa sababu ya ile passion ya mambo tunayoyafanya.
Ila sasa hivi watoto ndio wanaisubiri kula kwa sababu hawana cha kufanya,wapo bored hakuna kitu cha kuwasisimua ubongo wao mpaka wakasahau kula chakula,matokeo yake tunapata watoto wengine wavivu kabisa.
Wanangu nitawapeleka shule ambazo hawasomi sana na wala hakuna ujinga wa tuisheni,ukileta mambo ya tuition maana yake shule yako haitimizi wajibu.
Kimisngi kabisa maisha ya zamani ndio yalikuwa na makuzi sahihi yenye kujenga ubongo na uwezo wa mtoto kufikiri.
Mambo ya shuleni ni kujifunza mawazo ya wwengine wakati huo katika uhalisia mtoto anahitaji kujifunza mambo mengine mengi kama vile tabia,nidhamu ya matumizi,kudhibiti hisia zake,kujijua mwenyewe,kuwajua watu wengine,kujifunza kutoka kwa wazazi n.k
Mtoto anakaa masaa 12 shuleni .
Anarudi nyumbai analala saa4 usiku jivyo anakaa na wazazi masaa kama ma4 tu.
Then analala masaa 6.
Hivyo mtoto anapata masaa ma4 tu ya kukaa na wazazi tena masaa ma4 hayo pengine mzazi yuko bize hana hata muda wa kuongea na kucheza na watoto na kuwafundisha vitu kadhaa,hivyo mtoto anapoteza ile muunganiko wa uzazi na wazazi wake.
Mtoto anapotumia masaa 10-12 shuleni kwenye jengo moja na madawati hakuna wanachojifunza hapo zaidi ya kulishana ujinga na tabia mbovu.
Wangetumia masaa 12 hayo kucheza na kujichanganya mtaani kufanya vitu mbalimbali basi tungekuwa na watoto bora kabisa
Nina mengi ya kuandika ila tuishie hapo na nitahakikisha wanangu nawalea katika mifumo niliyolelewa mimi.