Shule ya English Medium imegoma kumuhamisha mwanangu. Hatiani kukosa mtihani wa darasa la nne

Pole sana ila usimwambie mwanao kua hawezi kufanya mtihani.

Pambana kimyakimya bila dogo kujua kitu, mtoto mdogo namna hiyo hawezi yabeba hayo.

Tatizo kina maza wengi wa kileo huona watoto wao kama watu wazima huwaambia mabaya ya baba zao, matatizo yao na kama hivo unamwambia hatofanya mtihani na blah blah kama hizo na ukiangalia dogo hana msaada anaishia kulia tu.
 
Kwanza, kumsaidia mwanao huyo wa std IV, lipa hiyo pesa kwanza kupitia taratibu sahihi...

Pili, peleka mashataka jeshi la polisi na mtuhumiwa awe ni huyo mwalimu mwanamama aliyekuwa anakulaghai...
Ushauri kama wa mganga wa kienyeji huu. Amesha kwambia hana hiyo hela na mtoto wapo kwenye usajili wa watoto wa darasa la nne wewe unasema tena aende kulipa hela ambayo hana na ambayo anasema alishalipa hana deni? Huo muda wa kuhangaishana na polisi huoni kuwa deadline itapita na mtoto wake hatosajiliwa kufanya mtihani?
Wewe ni great thinker kweli?

Mtoa mada nakushauri fanya kama ifuatavyo.

1. Chukua RB nenda kamkamate huyo mwalimu ikiwezekana nenda kamtafutie hapo shuleni kwao na hao watu wa hapo shuleni wakuelekeze pa kumpata au kamata mwalimu mkuu weka ndani muunganishe na huyo madam.


2. Wakati hili linafanyika watwange barua ya kuwashitaki kwa kosa la kuzuia uhamisho wa mtoto wako kinyume na sheria ya ya Elimu ya Tanzania ambayo inasema mtoto asizuiwe kufanya mtihani kwa sababu yoyote ile inayo husiana na ada.


3. Wakati huo huo nenda mahakamani maombi hati ya dharula ( injunction order ) ambayo itawaamuru uongozi wa shule kumuhamisha mwanao wakati kesi ya Msingi inasubiri kusikilizwa.

4. At the same time shirikisha media kwa mfano jirekodi wewe pamoja na watoto wako ukielezea kuhusu suala lako huku mtoto akielezea namna anavyo athiriwa na suala lako. Utapata msaada wa haraka sana.

Usifadhaishwe na majibu ya hovyo ya baadhi ya wachangia mada humu. Hivyo ndivyo walivyo wasomi wa Tanzania. Wasomi wa Tanzania huwaga hawaandaliwi kusolve matatizo mapya huwa wanaandaliwa kukariri tu.
 
Kama nimeelewa vizuri ni kuwa wewe umetapeliwa na huyo mwalimu uliyekuwa unampa ada ya mtoto wako akakulipie. Inawezekana mwalimu hakulipa bank na alikuwa anakueletea risiti ambazo hazikutoka kwenye utaratibu halali.
Kwa upande mwingine shule iko sawa kabisa kudai ada yao maana pesa hawakupokea kupitia utaratibu uliowekwa.

Nashauri uende shuleni uko Mwanza ukazungumze na wahusika wa shule muone namna gani mnaweza kutatua tatizo hilo ili mtoto apate haki.

Daa...!!!! Ulifanya kosa sana mkuu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Pole mama kama kuna mtu wa karibu anaweza akafika shuleni na kumaliza hili jambo kwa mazungumzo itakuwa vizuri kwa sababu inaonekana kuna mahali uliteleza pia kama mzazi.Ongea pande mbili mmalize hili tatizo,unakoelekea huyo madam atakukana otherwise una sms za miamala na sms za mazungumzo yenu
 
Apeleke malalamiko yake kwenye media tu ndio atapata suluhisho la haraka. Serikali imekataza mtoto kunyimwa haki yake ya kufanya mtihani eti kwa sababu ya ada.
 
Ampeleke polisi aende na kwenye media tu atapata haki yake..
 
Imagine mtoto ameyajuaje hayo
 
Pole.

Umuhimu wa baba wa familia umeonekana hapa.

Nina uhakika mwanaume angekuwa karibu wala usingefika hapa.

Mpaka unakuja JF kuomba msaada maana yake hauna ushirikiano na baba watoto.

Hili ni tatizo ambalo mwanamke kulitatua ni gumu, ila kwa sisi wanaume ni rahisi sana.
 
Nenda Wilayani ofisi ya elimu watamhamisha chap, lkn pia Prem haiwezi soma darasa la 5 Kama hajafanya mtihani, Prem inamkalilisha darasa.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Dah watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mtoa mada Anacho kitaka ni suluhisho kuhusu mtoto wake aruhusiwe kufanya mtihani wa darasa la 4. Wewe tena unazungumza kuhusu sijui baba na mama blah blah . Mtoa mada anahitaji msaada wa dharula. Instead of giving the answer , ur talking about the question sasa wewe una tofauti gani kifikra na mtu alielelewa na single mother? Maana hata wewe unawaza kaa hisia tu
 
Nenda Wilayani ofisi ya elimu watamhamisha chap, lkn pia Prem haiwezi soma darasa la 5 Kama hajafanya mtihani, Prem inamkalilisha darasa.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
Ubarikiwe sana kaka sasa niende wilayani huko Mwanza au hata hapa Dar wanaweza kufanya hilo zoezi? Vipi kama hiyo shule ilikuwa haijasajiliwa?
 
Kukusaidia waanike wote, jina la shule, jina la mwalimu tapeli, jina la mkuu wa shule, mahali ilipo na anuani na namba za simu zote.
 

Kumbuka pia hapa umeonyesha jinsi wewe ulivyo na siyo namna nilivyo mimi
 
Inatakiwa busara itumike:-
  • Huyu wa la nne, usimuhamishe kwanza, subiri amalize kwanza mtihani; kama wameweza kuvumilia deni lote hilo ni waungwana.​
  • Zungumza kwa unyenyekevu na hiyo shule ya medium, namna utakavyolipa hilo deni, pamoja na hatua za kumchukulia yule aliyekupa hasara.​
  • Hakuna haja ya kutumia nguvu wala jazba; jishushe na utafute suluhu kwa shule husika.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…