Shule ya English Medium imegoma kumuhamisha mwanangu. Hatiani kukosa mtihani wa darasa la nne

Pole sana ila usimwambie mwanao kua hawezi kufanya mtihani.

Pambana kimyakimya bila dogo kujua kitu, mtoto mdogo namna hiyo hawezi yabeba hayo.

Tatizo kina maza wengi wa kileo huona watoto wao kama watu wazima huwaambia mabaya ya baba zao, matatizo yao na kama hivo unamwambia hatofanya mtihani na blah blah kama hizo na ukiangalia dogo hana msaada anaishia kulia tu.
 
Kwanza, kumsaidia mwanao huyo wa std IV, lipa hiyo pesa kwanza kupitia taratibu sahihi...

Pili, peleka mashataka jeshi la polisi na mtuhumiwa awe ni huyo mwalimu mwanamama aliyekuwa anakulaghai...
Ushauri kama wa mganga wa kienyeji huu. Amesha kwambia hana hiyo hela na mtoto wapo kwenye usajili wa watoto wa darasa la nne wewe unasema tena aende kulipa hela ambayo hana na ambayo anasema alishalipa hana deni? Huo muda wa kuhangaishana na polisi huoni kuwa deadline itapita na mtoto wake hatosajiliwa kufanya mtihani?
Wewe ni great thinker kweli?

Mtoa mada nakushauri fanya kama ifuatavyo.

1. Chukua RB nenda kamkamate huyo mwalimu ikiwezekana nenda kamtafutie hapo shuleni kwao na hao watu wa hapo shuleni wakuelekeze pa kumpata au kamata mwalimu mkuu weka ndani muunganishe na huyo madam.

2. Wakati hili linafanyika watwange barua ya kuwashitaki kwa kosa la kuzuia uhamisho wa mtoto wako kinyume na sheria ya ya Elimu ya Tanzania ambayo inasema mtoto asizuiwe kufanya mtihani kwa sababu yoyote ile inayo husiana na ada.

3. Wakati huo huo nenda mahakamani maombi hati ya dharula ( injunction order ) ambayo itawaamuru uongozi wa shule kumuhamisha mwanao wakati kesi ya Msingi inasubiri kusikilizwa.

4. At the same time shirikisha media kwa mfano jirekodi wewe pamoja na watoto wako ukielezea kuhusu suala lako huku mtoto akielezea namna anavyo athiriwa na suala lako. Utapata msaada wa haraka sana.

Usifadhaishwe na majibu ya hovyo ya baadhi ya wachangia mada humu. Hivyo ndivyo walivyo wasomi wa Tanzania. Wasomi wa Tanzania huwaga hawaandaliwi kusolve matatizo mapya huwa wanaandaliwa kukariri tu.
 
Kama nimeelewa vizuri ni kuwa wewe umetapeliwa na huyo mwalimu uliyekuwa unampa ada ya mtoto wako akakulipie. Inawezekana mwalimu hakulipa bank na alikuwa anakueletea risiti ambazo hazikutoka kwenye utaratibu halali.
Kwa upande mwingine shule iko sawa kabisa kudai ada yao maana pesa hawakupokea kupitia utaratibu uliowekwa.

Nashauri uende shuleni uko Mwanza ukazungumze na wahusika wa shule muone namna gani mnaweza kutatua tatizo hilo ili mtoto apate haki.

Daa...!!!! Ulifanya kosa sana mkuu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Pole mama kama kuna mtu wa karibu anaweza akafika shuleni na kumaliza hili jambo kwa mazungumzo itakuwa vizuri kwa sababu inaonekana kuna mahali uliteleza pia kama mzazi.Ongea pande mbili mmalize hili tatizo,unakoelekea huyo madam atakukana otherwise una sms za miamala na sms za mazungumzo yenu
 
Apeleke malalamiko yake kwenye media tu ndio atapata suluhisho la haraka. Serikali imekataza mtoto kunyimwa haki yake ya kufanya mtihani eti kwa sababu ya ada.
 
Pole mama kama kuna mtu wa karibu anaweza akafika shuleni na kumaliza hili jambo kwa mazungumzo itakuwa vizuri kwa sababu inaonekana kuna mahali uliteleza pia kama mzazi.Ongea pande mbili mmalize hili tatizo,unakoelekea huyo madam atakukana otherwise una sms za miamala na sms za mazungumzo yenu
Ampeleke polisi aende na kwenye media tu atapata haki yake..
 
Pole sana ila usimwambie mwanao kua hawezi kufanya mtihani.

Pambana kimyakimya bila dogo kujua kitu, mtoto mdogo namna hiyo hawezi yabeba hayo.

Tatizo kina maza wengi wa kileo huona watoto wao kama watu wazima huwaambia mabaya ya baba zao, matatizo yao na kama hivo unamwambia hatofanya mtihani na blah blah kama hizo na ukiangalia dogo hana msaada anaishia kulia tu.
Imagine mtoto ameyajuaje hayo
 
Pole.

Umuhimu wa baba wa familia umeonekana hapa.

Nina uhakika mwanaume angekuwa karibu wala usingefika hapa.

Mpaka unakuja JF kuomba msaada maana yake hauna ushirikiano na baba watoto.

Hili ni tatizo ambalo mwanamke kulitatua ni gumu, ila kwa sisi wanaume ni rahisi sana.
 
Mimi ni single mother umri wangu ni miaka 34. Kwa ufupi Nina watoto wawili wa kiume wa kwanza ana miaka tisa wa pili ana miaka saba. Huyu kwanza yupo darasa la 4 na wa pili yupo darasa la 3. Kilicho nifanya nilete ujumbe huu hapa Jamii Forums ni kitendo cha dhulma kinacho taka kufanywa na shule ya English Medium dhidi ya watoto wangu.

Ni hivi baada ya kuachana na baba wa watoto wangu niliwapeleka wanangu kwa bibi yao Mwanza.

Wakati nawapeleka Mwanza mkubwa alikuwa kafikisha umri wa kuingia darasa la kwanza na mdogo alikuwa na umri wa kuingia chekechea.

Walipo fika mwanza nikawapeleka kwenye shule moja ya English Medium. Mwalimu wa shule hiyo ambae alikuwa jirani yangu ndio alie nishawishi niwapeleke watoto wangu kwenye shule hiyo kwa sababu alisema walikuwa na utaratibu mzuri wa malipo na walikuwa wanachukua hata shilingi elfu hamsini kwa mwezi au themanini.

Niliona inanifaa kwa sababu iliendana na kipato changu. Baba wa watoto pia alikuwa ana toa sapoti ya ada. Kweli nilienda nikalipa hela watoto wakasajiliwa wanapewa na prem number wakaanza kusoma. Pesa nililipa kwa huyu mwalimu kwa sababu aliniambia pesa niwe nalipa kwake yeye anaziwasilisha kwa uongozi kwa sababu walikuwa wanapewa commission na shule kwa kila mwanafunzi watakae mpeleka shuleni. Sikuwa Mimi tu pia kuna baadhi ya wazazi walikuwa wanalipa kwa utaratibu huo. Niliwaacha watoto kwa bibi yao nikarudi zangu Dar kuendelea na shughuli zangu. Nikiwa naendelea na utaratibu huo huo wa kulipa kupitia kwa huyo mwalimu ambae alikuwa anawaandikia watoto risiti wanaziwasilisha kwa bibi yao. Wakati mwingine anasema alikuwa anawaandikia maelezo ya kawaida kwamba wamelipa ada na kwamba ataziwasilisha hela kwa uongozi kisha atapewa risiti na shule atawapatia watoto wazipeleke kwa bibi yao.

Fast forward mwaka jana mwezi wa saba wakati wa likizo nilipiga simu kwa huyo madam kwamba ninataka kuwahamisha watoto wangu kuwaleta Dar anisaidie kuongea na uongozi tupate prem numbers za watoto. Madam akaniambia analishughulikia but akaniambia kwa wakati huo wa likizo watoto wanatakiwa kuwa shuleni hivyo ninatakiwa kulipa shilingi elfu themanini ambayo kama ilivyo kuwa siku zote alitaka niilipe kupitia simu yake. Lakini Mimi nilimwambia Nina wachukua watoto waje Dar ili niwe nao kwa ukaribu zaidi. Akasema sawa atashughulikia suala la uhamisho. Siku iliyo fuata nikampigia sikumpata nikaona nimtume mdogo wangu aende kuchukua namba za mwalimu mkuu wa shule.

Nilipo ongea na mwalimu mkuu wa shule cha kushangaza akasema huyo madam sio mwalimu wa hapo kwa zaidi ya miezi miwili na kwamba amewaliza wazazi wengi ambao walikuwa wanampa pesa yeye. Nikauliza sasa kuhusu haki za watoto wangu vipi kwa sababu ninataka kuwahamisha ma huyo mwalimu alikuwa mwajiriwa wao wanatusaidia vipi sisi wazazi tulio muamini na kumlipa pesa zetu?

Pili nikamwambia atazame kama watoto wamesajiliwa kwa sababu nilimpa shilingi laki moja na elfu sitini kama gharama za usajili kwa kila mtoto.

Niliogopa sana nilihisi huenda hata hiyo shule yenyewe haina usajili.

Mkuu akasema wacha atazame kuhusu status ya wanafunzi hao pamoja na rekodi zao za ada.

Kuhusu status ya usajili akasema watoto wote wana prem numbers ingawa gharama za kuwasajili pia nilipigwa.

Kuhusu ada nikaambiwa nadaiwa shilingi milioni moja na laki 2 kwa sababu tangu watoto waanze kusoma kwenye shule hiyo hawajawahi lipa hata senti tano.

Nikajiuliza how comes mnasema watoto hawajawahi lipa hata senfi wakati hadi matokeo ya watoto yapo nyumbani.

Walifanya vipi mitihani bila kulipa hata senti 5?

Walipata vipi prem numbers kama hawajawahi kulipa hata senti tano?

Nilifadhaika sana na nilianza kukosa imani na hiyo shule kabisa.

Niliwaagiza watoto wangu Dar then nika watafutia shule ya kawaida ya kiswahili. Nili ichagua shule hii kwa sababu ipo karibu na mahali ninapo ishi lakini pili sina uwezo wa kulipa kwenye shule za English Medium kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha na uwezo wangu kifedha kushuka na sapoti ya baba watoto imekuwa ndogo.

Kingine nilikosa kabisa imani na shule za English Mediums hasa hizi zinazo Anza Anza zenye wanafunzi wachache. Bado nilikuwa na kidonda kibichi kutoka kwa shule hiyo waliyo soma watoto wangu.

Nilipata nafasi kwenye shule ya kiswahili huku nikipambana kuomba shule waliyo kuwa wanasoma wawahamishe wanangu kwenye mfumo wawatoe kwenye shule yao wawahamishie kwenye shule hii mpya. Lakini cha ajabu muda wote wamekuwa wakinipiga danadana wanadai niwalipe pesa ambayo kiufupi hawanidai.

Sasa hivi darasa la nne wapo kwenye usajili wa mitihani ya taifa huyu mwanangu jina lake bado linasoma kwenye shule aliyo toka.

Walimu wanasema asipo hamishwa ndani ya deadline maana yake ni kwamba atatakiwa kwenda kufanya mtihani kwenye shule ile ile ambayo ni ya kiingereza au atatakiwa kurudia shule na kama akirudia basi prem number yake itaendelea kusoma juu yani itaonekana yupo darasa la 5 wakati yupo darasa la 4 yani kiufupi ndoto za mwanangu kitaaluma ndio zinakuwa zimeishia hapo. Sasa Mimi naomba msaada wa mamlaka zinazo husika zinisaidie ili mtoto wangu apewe haki yake ya kufanya mtihani wake wa darasa la 4 ambayo inataka kupokwa na wamiliki wa shule aliyo toka bila justification yoyote. Sheria na taratibu za elimu ya Tanzania zina kataza mtoto kunyimwa haki ya kufanya mtihani kwa sababu yoyote ile inayo husiana na fedha. Uongozi wa hiyo shule ya English Medium unataka kuvunja sheria hii kwa kumkosesha mwanangu haki yake ya kufanya mitihani ya darasa la nne kwa sababu ya deni hewa. Mtoto wangu ameshinda analia siku nzima ya leo anauliza sasa mama itakuwaje..

Naomba msaada tafadhali. Namba za huyo mwalimu alie kuwa anachukua ada zipo namba za mkurugenzi wa shule zipo namba za mkuu wa shule zipo na risiti zote ambazo zilikuwa zinaandikwa kwamba mwanangu amelipa ada pia zipo kwa bibi wa watoto. Nipo tayari kuziwasilisha risiti hizo mbele ya uongozi wa shule kama zikihitajika ila kwa sasa ninacho hitaji ni mtoto wangu apewe haki yake ya kufanya mtihani wake wa darasa la nne.

Uwepo wa namba za huyo mwalimu alie kuwa anachukua hela zangu pamoja na as wazazi wengine utarahisisha kukamatwa kwa huyo mwalimu ili alipe hizo pesa alizo Chukua. Niliwaambia uongozi wa shule wanisaidie huyo mwalimu akamatwe lakini wamekuwa wanapiga danadana kana kwamba wana mkingia kifua au wana ogopa kuchafua taswira ya shule yao.

Naomba msaada pia huyu madamu akamatwealipe hizo hela alizo Kula lakini wakati zoezi la kumtafuta na kumuweka ndani huyu madamu linaendelea naomba watoto wangu wapewe haki yao ya uhamisho.

Serikali waki hitaji ni disclose taarifa za hiyo shule pamoja na majina ya huyo madam wanae sema amekimbia na hela pamoja na majina ya uongozi nipo tayari kufanya hivyo.

Yericko Nyerere

Mh.
Dkt. Gwajima D
Nenda Wilayani ofisi ya elimu watamhamisha chap, lkn pia Prem haiwezi soma darasa la 5 Kama hajafanya mtihani, Prem inamkalilisha darasa.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Dah watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mtoa mada Anacho kitaka ni suluhisho kuhusu mtoto wake aruhusiwe kufanya mtihani wa darasa la 4. Wewe tena unazungumza kuhusu sijui baba na mama blah blah . Mtoa mada anahitaji msaada wa dharula. Instead of giving the answer , ur talking about the question sasa wewe una tofauti gani kifikra na mtu alielelewa na single mother? Maana hata wewe unawaza kaa hisia tu
 
Ubarikiwe sana kaka sasa niende wilayani huko Mwanza au hata hapa Dar wanaweza kufanya hilo zoezi? Vipi kama hiyo shule ilikuwa haijasajiliwa?
 
Kukusaidia waanike wote, jina la shule, jina la mwalimu tapeli, jina la mkuu wa shule, mahali ilipo na anuani na namba za simu zote.
 
Dah watanzania sisi ni watu wa ajabu sana. Mtoa mada Anacho kitaka ni suluhisho kuhusu mtoto wake aruhusiwe kufanya mtihani wa darasa la 4. Wewe tena unazungumza kuhusu sijui baba na mama blah blah . Mtoa mada anahitaji msaada wa dharula. Instead of giving the answer , ur talking about the question sasa wewe una tofauti gani kifikra na mtu alielelewa na single mother? Maana hata wewe unawaza kaa hisia tu

Kumbuka pia hapa umeonyesha jinsi wewe ulivyo na siyo namna nilivyo mimi
 
Inatakiwa busara itumike:-
  • Huyu wa la nne, usimuhamishe kwanza, subiri amalize kwanza mtihani; kama wameweza kuvumilia deni lote hilo ni waungwana.​
  • Zungumza kwa unyenyekevu na hiyo shule ya medium, namna utakavyolipa hilo deni, pamoja na hatua za kumchukulia yule aliyekupa hasara.​
  • Hakuna haja ya kutumia nguvu wala jazba; jishushe na utafute suluhu kwa shule husika.​
 
Back
Top Bottom