DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huko wananchi wake wanafanya kazi na kulipa kodi, Tz hata kodi hawataki kulipa wanadai ni wanyonge
Wanataka vya Bure na Kodi hawalipi,iwe Ili vya Bure lipeni Kodi harafu Serikali itenge Bajeti za kuendeshea shule Ili zinunue hayo mahitaji.

Haya majamaa ndio yanadanganywa na Machadema huko yanajua labda siku Chadema ikishika Dola kutakuwa na Bure 😁😁
 
Pole Sana, wahusika wapo humu, hope suala lako litashughulikiwa, sema umekosea kutaja mkoa uliotoka coz ni rahisi kwa walimu kumtambua mwanao. Na kuanza kumletea chuki.
Hiyo ya kumletea mtoto chuki upo sahihi kabisa. Kuna jamaa yangu mwanae alimueleza jinsi asivyo na amani Shuleni kwa madai kuwa kuna mwalimu anamchukia tu yeye bila sababu na amekuwa anaona kama vile ni yeye tu anayenyanyasika darasani kwao.

Mwanzo mzazi huyo alipuuza na hakumzingatia sana huyo mwanae. Lakini bado mtoto alionyesha kulalamika kila mara. Sasa jamaa siku moja alikwenda shuleni hapo kupeleka risit za ada na kwa kuwa alishaambiwa jina la huyo mwalimu akadadisi akamuona. Alipomuona ndipo akili ikachanganya kidogo kwavile muonekano wa huyo mwalimu ni kijana sana halafu kama mjanjamjanja hivi na jamaa mtoto wake ni wa kike mwili mkubwa.

Sasa jamaa kwa kukurupa akamuona mkuu wa Shule akamtaarifu kuwa mwanae analalamika kunyanyaswa na mwalimu fulani. Mkuu wa Shule akamuahidi kulifanyia kazi, kimsingi alionyesha kulipokea hasa. Baada ya hapo mtoto akawa anamuambia baba yake kuwa sasahivi ana amani sana na yule mwalimu alijirekebisha kabisa.

Sasa baada ya binti kumaliza la saba ndipo akamuambia baba yake kuwa alijutia sana kitendo cha kumueleza maana kilichoendelea kwake pale Shuleni ni Mungu tu ndie anajua maana ni walimu wote walionyesha kumchukia sana hadi mkuu mwenyewe wa shule na walimu wakawa wanamsimanga indirect kwa wenzao . Binti anasema ni heri ilitokea wakati yupo la saba kwani ingetokea akiwa la 5-6 angekimbia hiyo shule bila kuaga.

Hiyo Shule inaitwa Green Belt ipo Mbezi.

Kimsingi kuna yanayoendelea mashuleni huko ambayo sio mazuri. Taaluma ya ualimu mbali na kuhitaji watu wenye elimu nzuri lakini pia inahitaji walimu wenye Utu/ubinaadam , upendo na maadili.
 
Aisee lipia tu,,yaani mifagio na ndoo sio vitu vya wizara kuingilia kati
 
Kwanza imekuaje Mwanao Kapangwa Dodoma na ametoka Mtwara?

Nijuavyo kuanzia mwaka huu, ili kuepuka usumbufu serikali inampanga mwanafunzi kwenye kanda aliyosomea O-level na hilo limefanyika kweli...

Kuna kanda Ya ziwa, Kanda ya kati, kusini, kaskazini Pwani n.k,
Labda uniambie mwanao Kasomea Maeneo ya karibu ila Kwa sasa ndio mmetokea mtwara..
Kuna mwanafunzi katoka Na kasoma Songea O level, kapangwa Kagera Advance.
 
Hiyo ya kumletea mtoto chuki upo sahihi kabisa. Kuna jamaa yangu mwanae alimueleza jinsi asivyo na amani Shuleni kwa madai kuwa kuna mwalimu anamchukia tu yeye bila sababu na amekuwa anaona kama vile ni yeye tu anayenyanyasika darasani kwao.

Mwanzo mzazi huyo alipuuza na hakumzingatia sana huyo mwanae. Lakini bado mtoto alionyesha kulalamika kila mara. Sasa jamaa siku moja alikwenda shuleni hapo kupeleka risit za ada na kwa kuwa alishaambiwa jina la huyo mwalimu akadadisi akamuona. Alipomuona ndipo akili ikachanganya kidogo kwavile muonekano wa huyo mwalimu ni kijana sana halafu kama mjanjamjanja hivi na jamaa mtoto wake ni wa kike mwili mkubwa.

Sasa jamaa kwa kukurupa akamuona mkuu wa Shule akamtaarifu kuwa mwanae analalamika kunyanyaswa na mwalimu fulani. Mkuu wa Shule akamuahidi kulifanyia kazi, kimsingi alionyesha kulipokea hasa. Baada ya hapo mtoto akawa anamuambia baba yake kuwa sasahivi ana amani sana na yule mwalimu alijirekebisha kabisa.

Sasa baada ya binti kumaliza la saba ndipo akamuambia baba yake kuwa alijutia sana kitendo cha kumueleza maana kilichoendelea kwake pale Shuleni ni Mungu tu ndie anajua maana ni walimu wote walionyesha kumchukia sana hadi mkuu mwenyewe wa shule na walimu wakawa wanamsimanga indirect kwa wenzao . Binti anasema ni heri ilitokea wakati yupo la saba kwani ingetokea akiwa la 5-6 angekimbia hiyo shule bila kuaga.

Hiyo Shule inaitwa Green Belt ipo Mbezi.

Kimsingi kuna yanayoendelea mashuleni huko ambayo sio mazuri. Taaluma ya ualimu mbali na kuhitaji watu wenye elimu nzuri lakini pia inahitaji walimu wenye Utu/ubinaadam , upendo na maadili.
Kwa tuliopitia manyanyaso mashuleni, tunasema "ahsante kwa kutoka salama" vinginevyo unakimbia shule na hugeuki nyuma wala hurudi tenaaa.

Sitaki kukumbuka kabisa.
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Lipa
 
Heb share hivo vitu vinavyofika laki nne,
Wote tumesoma siku hizi, wew peleka michango mtoto apokelewe, kwa hio unataka vyoo vya mtoto wako visafishwe kwa fagio ya nani?
Mtwara wameuza ufuta bei nzuri tu na Kwa sasa wanauza mbaazi kilo Moja tsh 2000

Alipe tu Kwa kweli, mtoto wa kike atanyanyasika shuleni
 
Sasa vifaa vya usafi hujakamilisha unategemea mwanao ataishaije??elimu ya mwanao mwenyewe kwa faida yake na yako bado unaona kama unaonewa?? Wenzio wakipeleka vitu wanatoa hadi tips za walimu wawe nao karibu kuwasaidia wafaulu vzr ww unakimbilia kulalamika,
 
Timiza wajibu wako, petty issue kama hizi nazo ni za kuleta jamvini kama mzazi!?
 
Jaman elimu bure ni ada tu !! Ila mahitaji ya mtoto ni wewe mwenyewe mzazi na CCM walivyo wajanja wakasema elimu bure , wazazi msibweteke kusomesha bado ni gharama aseee

Angalau kama una mtoto anaenda kidato cha tano andaa 500k umekosa sana 350k iwepo na kama huna hela weka mambo ya msingi mbele kwanza.
Mfano sare za shule (mashati) atumie alizomalizia kidato cha nne , suruali au sketi apate moja na ya kushindia !! Viatu Pair moja anaweza kuanzia !! Shoe polish ndogo counter book sio lazima aende na Quire 4 aende na ndogo ! Bananeni hivyo hivyo dogo akasome ! Huku akiondoka na wewe unacheki mazingira jinsi ya kumwinua !

Mnavyolalamika hivi dogo akienda ndo imeisha hiyo mtoto anaishi kwa tabu vibaya mno ! Hatukatai kukosa kupo ila ukishapata mtoto na mradi ulimtafuta ukiwa kwenye furaha zako huo ni wajibu sio hiyari tena!
-mzazi mtarajiwa [emoji23]
Halafu akumbuke elimu ya advance ni chini ya miaka 2,ukimdisturb mtoto kidogo tu akatoks ktk reli kurecover huchukua muda sana,inataka utulivu wa akili,hivyo unavyofanya harakati walimu wakimmaki kuwa babaake alileta harakati unaweza kumfanya mtoto asiwe comfortable shuleni,wazazi vumilieni hakuna elimu ya bure kabisa na vifaa vingi unavoambiwa ununie ni kwa matumizi ya mtoto wako, kaongee vzr na mwlm wake uone mtamsaidiaje siyo kuleta harakati!!
 
Kwahyo unataka mitihani aandikie chini kama mtoto wa vidudu kipindi hicho au?
 
Back
Top Bottom