Hiyo ni kazi ya mzazi/mlezi.
Kazi ya mwalimu ni kufundisha, asipofanya hivyo ashughulikiwe ila kuhusu kuchapa HAPANA.
Kumbuka hata huyo mwalimu ana watoto hivyo ata deal na watoto wake wawe na nidhamu kama ambavyo wazazi wengine wanavyo deal na wanao kwao.
Kuna matukio mengi ya walimu kutukanwa, kusimamishwa kazi, kupelekwa mahakamani na kupita kwenye tanuru la moto kisa kuchapa watoto, wakati angeachana nao asingepungukiwa chochote.
Kuna walimu hawachapi hata kama mtoto amefanya kosa kubwa kiasi gani. Mwalimu wa aina hii anaishi vema na kibarua chake kiko salama.
Unawachapa ila likitokea la kutokea kwa bahati mbaya unabaki pekee yako waliokuwa wanakusifia kuwa unawapa wanafunzi nidhamu wanakukimbia.
Kujiepusha na yote hayo mwalimu fundisha kwa bidii ila usichape mtoto wa mtu.
KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE