Shule za English Medium ni kiwanda cha kuongeza Depression kwa wazazi na watoto. Serikali iboreshe shule za umma

Shule za English Medium ni kiwanda cha kuongeza Depression kwa wazazi na watoto. Serikali iboreshe shule za umma

Wazazi wengi wana msongo wa mawazo kutokana na stress za kutafuta ada za shule za kina junior wao wanaosoma english medium eg. Atlas, Tusiime, etc. Muda wa kulipa ada ukifika mzazi anakuwa na hasira hasira tu sababu ya msongo wa mawazo

Watoto na wao wana msongo wa mawazo kutokana na ratiba ya shule zao hizo za kisasa english medium. School bus inakuja saa 11 alfajiri na kumrudisha saa 12 jioni. Hapo mtoto kabebeshwa bonge la begi mgongoni lenye vitabu ma madaftari ya masomo yote.

Hapo hapo hapati muda wa kupumzika wala kucheza ku enjoy utoto wake, maana kila siku ana home work, na likizo hakuna kufunga shule kisingizio ni kujiandaa na mitihani. Hapo Mtoto anapata depression toka utotoni maskini.

Pili hizi shule zina fake lifestyle, zinamfundisha mtoto softlife ambayo mtaani hakuna hiyo soft life. Vitu kama kufanyiwa usafi, kufatwa na school bus, mtoto huyu huyu akija kukutana na maisha halisia ya kugombea mwendokasi ama daladala anaona anaonewa.

Hapo tena mtoto anakuwa na depression akikosa hiyo soft life after school. Tukumbuke schooling is a lifestyle not a place. Mtu aliyezoea soft lifestyle lazima apate depression akikutana na real life.

Pia hii tabia ya wazazi ku buy education at high price kunawafanya wazazi washindwe kuwekeza kwenye assets zingine ili watoto wao wapate hata pa kuanzia mbeleni.

Mzazi anaishi nyumba ya kupanga ila anatumia milioni 10 kila mwaka kulipia watoto wake ada Atlas ama Tusiime. Mzazi huyu anashindwa kujenga nyumba ya familia yake ama kuanzisha miradi. Siku huyu mzazi akiumwa ama kufukuzwa kazi anakunywa sumu.

Ushauri kwa wazazi ambao bado hatujawekeza vya kutosha tuwe makini na hizi shule za english medium za kisasa.

Serikali pia ibadilike. Demand ya hizi shule ni kubwa sana, waongeze shule za umma, english medium ziwe nyingi. Sio Olimpio na Bunge tu.

Pia Jeshi la kujenga taifa ( JKT) pia.. lisiishie kuwekeza kwenye kujenga kumbi za harusi, kujenga fremu, bar na mambo ya catering tu JKT lingewekeza kwenye low cost english medium primary schools kwenye miji mikubwa. Bei za ada zao ziwe kama olimpio na bunge.
Mbona hizo shule ulizotaja za kawaida sana?
 
Mbona hizo shule ulizotaja za kawaida sana?

Hizo shule ndio zinaingia kundi la english medium za mtaala wa Necta ambazo wazazi wengi wenye depression wanasomesha watoto.

Shule ambazo hazifati mtaala wa necta wazazi na watoto wanaosoma hawaungi ungi maisha. Hawapati stress yoyote
 
Tafuteni pesa, usipokuwa na pesa kila kizuri utakitafutia ubaya hata ukimkuta mtu anatumia pesa zake utasema anazifuja huku hujui alipozipata
 
Binti yangu anamaliza form iv mwaka huuu nimemsomesha since vidudu private!! Haki ya Mungu nilikiona Cha mtema Kuni!? Wadogo zake nimesha waalert "ni mwendo wa kidumu na mfagio" sitaki tena ujinga !!!
Nitanunua vitabu na kutafuta walimu wa tuishen

🤣🤣🤣 pole sana mkuu na hongera kwa uamuzi mzuri. Mimi pia nimefanya hivyo mkuu. No value for money. Tunatoa hela watoto wetu wakajazwe ujinga
 
MamaSamia2025 Uzi wako huu kaka
Huu uzi ni mzuri sana. Jama kaeleza kiundani bila kwenda direct kuponda shule za Kayumba. Katoa ufafanuzi wa kutosha. Namuunga mkono. Tatizo kubwa kwa upande wangu ni shule za Kayumba kufundisha kwa kiswahili wakati lugha ya biashara dunia nzima ni kiingereza. Serikali ikubali tu kiswahili kiwe tu somo na sio lugha ya kufundishia masomo yote. Ikishindikana hilo basi ifanye maamuzi magumu ya kuboresha shule zake zote badala ya kutengeneza matabaka kwa kuita baadhi ya shule eti special na za kitaifa. Mkuu Likud kwa sasa mtoto anayesoma Ilboru, Moshi Tech, Weruweru, Ifunda na zingine zinazoitwa za kitaifa anapata elimu bora kwenye mazingira bora kuliko hizi private schools nyingi. Serikali iboreshe shule zake zote na kuajiri waalimu wengi. Ikifanya hivyo hakuna mtu atajihangaisha na hizi english medium zinazoamsha watoto saa 10 alfajiri na kuwapakia kwenye magari mabovu.
 
Wazazi wengi wana msongo wa mawazo kutokana na stress za kutafuta ada za shule za kina junior wao wanaosoma english medium eg. Atlas, Tusiime, etc. Muda wa kulipa ada ukifika mzazi anakuwa na hasira hasira tu sababu ya msongo wa mawazo

Watoto na wao wana msongo wa mawazo kutokana na ratiba ya shule zao hizo za kisasa english medium. School bus inakuja saa 11 alfajiri na kumrudisha saa 12 jioni. Hapo mtoto kabebeshwa bonge la begi mgongoni lenye vitabu ma madaftari ya masomo yote.

Hapo hapo hapati muda wa kupumzika wala kucheza ku enjoy utoto wake, maana kila siku ana home work, na likizo hakuna kufunga shule kisingizio ni kujiandaa na mitihani. Hapo Mtoto anapata depression toka utotoni maskini.

Pili hizi shule zina fake lifestyle, zinamfundisha mtoto softlife ambayo mtaani hakuna hiyo soft life. Vitu kama kufanyiwa usafi, kufatwa na school bus, mtoto huyu huyu akija kukutana na maisha halisia ya kugombea mwendokasi ama daladala anaona anaonewa.

Hapo tena mtoto anakuwa na depression akikosa hiyo soft life after school. Tukumbuke schooling is a lifestyle not a place. Mtu aliyezoea soft lifestyle lazima apate depression akikutana na real life.

Pia hii tabia ya wazazi ku buy education at high price kunawafanya wazazi washindwe kuwekeza kwenye assets zingine ili watoto wao wapate hata pa kuanzia mbeleni.

Mzazi anaishi nyumba ya kupanga ila anatumia milioni 10 kila mwaka kulipia watoto wake ada Atlas ama Tusiime. Mzazi huyu anashindwa kujenga nyumba ya familia yake ama kuanzisha miradi. Siku huyu mzazi akiumwa ama kufukuzwa kazi anakunywa sumu.

Ushauri kwa wazazi ambao bado hatujawekeza vya kutosha tuwe makini na hizi shule za english medium za kisasa.

Serikali pia ibadilike. Demand ya hizi shule ni kubwa sana, waongeze shule za umma, english medium ziwe nyingi. Sio Olimpio na Bunge tu.

Pia Jeshi la kujenga taifa ( JKT) pia.. lisiishie kuwekeza kwenye kujenga kumbi za harusi, kujenga fremu, bar na mambo ya catering tu JKT lingewekeza kwenye low cost english medium primary schools kwenye miji mikubwa. Bei za ada zao ziwe kama olimpio na bunge.
Hapo umenena kweli 100% mkuu. Tusubiri wenyewe wakusanye mapovu waje kukumwagia.

Shule za binafsi sio tu zinafanya watoto wawe tegemezi kwenye maisha lakini kwenye elimu pia wanajenga utegemezi. Mtoto wa Tusiime aliyezoea kumezewa kila kitu na mwalimu siku akienda High School ya serikali ambayo wanafunzi wana hustle wenyewe, anapata taabu sana.

Unakuta mtoto wa form IV wa English medium hajui kupika, kudeki au hata kufua chu.pi yake mwenyewe. Kila kazi anarundikiwa dada wa kazi. Leo na kesho wazazi hawapo duniani mtoto anaanza kuishi maisha ya mateso. Inauma sana.
 
Akiingia mbu darasani darasa zima wanalia. N.a. hao ni darasa la saba.
 
Ada ya mtoto wa Darasa la 3 ni kubwa kuliko ada ya mtu anayesoma chuo IFM [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]mimi wanangu watasoma kama nilivyosoma... tukutane sekondari ova
 
Ada ya mtoto wa Darasa la 3 ni kubwa kuliko ada ya mtu anayesoma chuo IFM [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]mimi wanangu watasoma kama nilivyosoma... tukutane sekondari ova
🤣🤣🤣 ur the true son of ur father
 
Kaka anasomesha watoto wake ada 4m kipato chake kwa mwezi hakifiki hiyo hela, sometimes anakopa ili alipie ada ya madogo 8m
Watoto wake wana umri gani now? Wapo primary au secondary?
 
Mtumie Uzi huu haraka sana mkuu
Mimi nikipata shule kama nilizosoma na waalimu wazalendo kama walionifundisha nitakuwa tayari kuwapeleka watoto palepale. Nilisoma shule ya msingi tukiwa wanafunzi wachache darasani huku waalimu wakiwa wa kutosha wanaoipenda kazi yao. Hakukuwa na tuition lakini tulifaulu na kwenda shule nzuri za serikali form one. Nikiwa sekondari kwenye shule ya serikali kama ningefeli form four basi ningekubali adhabu kali dhidi yangu. Shule niliyosoma ilikuwa na kila kitu. Practicals za sayansi tumefanya kuanzia form one. Yaani tukiwa form four tulikuwa tunawaza utapiga point ngapi kwenye kombi. Basic Mathematics nilifundishwa na waalimu wanne tofauti. Yaani kila kidato na mwalimu wake. Mkuu Likud kuna shule za serikali ni zaidi ya hizo za private. Serikali ikiboresha shule zake basi za private zitakufa kifo kibaya mno.
 
Utawakiwa vibaya mno, watakuambia tafuta hela, wana majibu mabaya, ukweli ndiyo ulivyo kwa shule hizo za fasheni. Utakuta mwingine ni hohehahe eti naye atajikakamua apeleke mtoto wake huko ili aonekane anazo kutaka sifa za kijinga huku akiumia.

Kwanza hiyo elimu inayotolewa huko ni ya kawaida tu kama ya umma na haina maajabu ya kumfanya mtoto awe fiti kimasomo. Labda ataambulia kiiengereza cha kubabaisha
Mkuu umeongea jambo zuri sana. Kinachoniuma zaidi kwenye hizi shule za medium ni kule kuwakaririshawanafunzi kwa lengo la kufaulu tu. Hawaendi extra mile kuwafundisha watoto stadi za maisha. Wao kila siku ni kuwakaririsha mitihani wanafunzi ili wafaulu vizuri shule ipate kiki wazazi walete watoto wengi zaidi wapige hela.

Unakuta vipindi vya kufanyishwa mitihani na kukakarishwa majibu ya mitihani vinazidi vipindi vya kufundisha darasani. Nilishangaa siku moja namuonyesha mtihani wa NECTA mtoto wangu anayesoma medium akaniambia tayari wameisha solve. Na wakati huo alikuwa darasa la sita. Yaani wanafunzi wanaanza kukakarishwa mitihani ya NECTA kuanzia darasa la sita kweli? Hii ni hatari kuliko maelezo.

Nailaumu pia serikali ya CCM kwa kutunga mitihani ya kubet. Hii mitihani ambayo hata wanafunzi wasiojua kusoma wanafualu na kuingia sekondari inapaswa kuangaliwa upya. Mtihani, hasa wa hesabu badala ya kuchochea maarifa, inachochea ujinga miongoni mwa wanafunzi. Wanafunzi wanafundishwa kukisia badala ya kukokotoa.

Kwa mfano, utakuta swali la hesabu kama hili hapa na machaguo yake kama ifuatavyo:

Find the value of X in the equation 2.56+x = 5
A. 20.44
B. 2.44
C. 32.34
D. 48.54

Swali kama hili hata kama mwanafunzi hakwenda shule atalijibu kwa kuangalia tu bila hata kukokotoa. Cha ajabu sasa maswali mwengi yanayotungwa na NECTA majibu yake hayafichwi hata kidogo. Yanawekwa hadharani ili wanafunzi wengi wafaulu wajaze shule za kata hata kama hawajui kusoma wala kuandika.

Shule za medium wananchofanya ni kupitia maswali ya NECTA zote na kuwakaririsha majibu wanafunzi. Pia wanawafundisha jinsi ya ku prove majibu bila kukokotoa. Mwisho wa siku tunatengeneza kizazi cha watu wasioukuwa na uwezo wa kufikiri wala kuhoji chochote kinachofanywa na wanasiasa. Lengo la elimu hapa nchini ni kuwajaza watu ujinga ili watawalike kirahisi bila shida. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom