Pengine tuna tatizo na mitaala yetu na pia wenzetu wanakuwa exposed kwa practical zaidi kuliko nadharia. Ila ukisema kwa wenzetu ni rahisi inanipa utata kidogo. Fani za afya ziwe kwa binadamu na wanyama zinafanana dunia nzima. Lakini bado kipimo sahihi cha uwezo wa mtu haswa kwa ajira za waadhiri na zingine sensitive kitabaki ni ufaulu tu na si vinginevyo. Kwa sasa hata bahadhi ya taasisi za kifedha wanaangalia GPA kushortlist watu wa interview, utasemaje mwenye GPA ya 4.2 umuache uchukue wa GPA ya 3.0 na wamesoma mazingira yanayoelekeana. Hata scholarship za nje wanaangalia ufaulu na ni kipimo sahihi kabisa ukiacha mapungufu machache yanayoletwa na wasimamizi
Kuna 'factors' nyingi sana zinazopelekea mtu kufaulu! Kubwa zaidi ni uwepo wa mazingira wezeshi ya ufundishwaji! Ukijaribu fananisha vyuo vyetu vingi, wanafunzi wetu wana'toil' sana kwa kutokuwa na miundombinu wezeshi za kuwafanya wanafunzi wetu wafikie 'potentials' walizonazo.
Jaribu kufanya kautafiti kadogo tu ktk idara mbalimbali kwenye vyuo vyetu uone namna ya ufundishaji na mafunzo yanavyotolewa. Utakuta idara nyingi sio tu hazijakamirika hata kwa idadi ya walimu, utakuta hata mwalimu mwenyewe hukuna kabisa, na kinachotokea ni kuazima mwalimu anayekuja kwa zima moto kufundisha materials yote kwa theruthi ya muda unaotakiwa!
Ukija kwa maeneo ya udaktari, unakuta hata vifaa tu vya kufanyia practicals au diagnosis vingi havipo na hivyo mwanafunzi anatakiwa awe na 'library' yake kichwani 'for reference values). wakati huko majuu, wenzetu wamewekeza vya kutosha ktk taasisi zao na hivyo kuwa na walimu na wasaidizi wao kila eneo, na pia kuwa na digitalized lab ambazo mwanafunzi wa udaktari hahitaji kukariri mambo mengi kichwani maana diagnostic facilities/computerized inafanya kila kitu kwa niaba yake. Hii inampa nafasi kubwa na pia 'interest' katika kufanya vizuri akisomea nje badala ya Tanzania.
Na kwa maana nyingine, huyu aliyesomea nje akija nchini inamuia vigumu hata kufanya kazi na mara nyingi ataonekana hafifu hata tu kwa kumlinganisha na wa hapa kwetu (aliye kariri mpaka 'normal values' za 'paramaters' nyingi ktk mwili wa binadamu na kufanya mambo mengi manually).
Kwa hiyo kwa kukosa mazingira wezeshi kazini, aliyesomea nje ya nchi anakuwa 'frustrated' na kwa kweli ataonekana ni 'MD-russia' tu kwa kushindwa kwendana na mazingira. Nimepata neema ya kwenda nje ya nchi yangu na kuona wenzetu wanavyofanya. Na pia nimepata neema ya kuwa sehemu ya wakufunzi katika vyuo vitatu mashuhuri duniani na kushuhudia mazingira ya kufundishia huko na ninakuhakikishia, ukimchukua mwanafunzi wetu hapa mwenye GPA ya chini kabisa aliye na makalayi tupu umpeleke kusomea huko, uwezekano wa kutoka na GPA 4.0 ni wa kufikia tu.
Kuendelea kuwahukumu wahitimu wetu wa hapa nyumbani waliopambana na mazingira hasi ya kujifunza wakapata walichopata, baadae kuja kukejeli jitihada zao kwa kuweka GPA zisizo na uhalisia ni ujuha! Ndugu yangu achana na kukimbilia kufananisha na nje au vigezo vya scholarship, tutatue ya kwetu hapa nyumbani! Hata hao wa nje walipitia hatua mpaka mwisho wakafikia huko!