Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,842
- 3,618
Mimi pia ni mdau wa elimu kwenye ngazi tofauti. Hilo la GPA linaweza kuwa na hoja kama fani anayosoma mtu ni mono-specialty ambayo job title yake italandana kabisa na skills set kama zilivyo kwenye kozi husika, mfano ukisema 'BSc in Business ICT' mwenye GPA kubwa kwenye degree hii ni mahiri kwenye business ICT.Unataka GPA kwa daktari ili iweje
GPA ndo inafanya operesheni, ndo inagawa dawa, ndo inapima mgonjwa?
Acheni ulimbukeni wa GPA
Lakini ni tofauti na kusema 'BSc in ICT', huyu kwenye kozi yake kuna mambo mengi ya ICT au hata yasiyo ya ICT, including hiyo business ICT. Kama unataka kuajiri mtu akufanyie kazi ya business ICT, ukitumia hoja ya GPA kwa huyu mwenye BSc ICT utakosea kwa sababu unaweza kukuta kuwa zile modules nyingine zimeshusha GPA yake hata kama alifanya vizuri sana kwenye hiyo module ya business ICT. Na kama ana aptitude kwenye hiyo business ICT ndipo utashangaa kwenye interview mwenye GPA ndogo (kutokana na kusoma multi-specialty) amevutia kuliko hata yule mwenye GPA kubwa kwa kusoma mono-specialty. Ni rahisi kupata GPA kubwa kwenye mono-specialty programs kwa sababu contents zote ziko relevant kwa mwanafunzi.
Ni vigumu kupata GPA kubwa kwenye multi-specialty program ambako kuna maeneo kadhaa ambayo hayana mvuto kwa mwanafunzi lakini anasoma tu ili kukamilisha coursework.
Kwenye ajira ningeshauri zaidi watumie job analysis kuliko GPA, watazame job description na kuipima against the set of skills required to accomplish the job, zile ambazo hazihusiki waachane nazo. Ikiwezekana aptitude test inaweza kusaidia pia.