Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

Je huko Urusi huduma za afya zikoje? Usitake uniambie URUSI ni wajinga kaisi kwamba wawe na elimu ya hovyo kwenye Matibabu.
Sijui kama nimekuelewa unataka nisemeje!
Nachokumbuka tulipokuwa intern pale Muhimbili miaka hiyo, hawa jamaa waliokuwa wanakuja na vyeti vya misonge ('A') kutoka urusi na uarabuni walikuwa wanaitwa MD-russia yaani ni vilaza maana walikuwa wanapata wakati mgumu sana kwa mchakamchaka wa machief pale Mubimbili na wengine waliishia kukimbia kabisa. Mimi pia nilihusika pia kuwasaidia saana hasa katika ku'manage' wagonjwa! Kiukweli walikuwa wamepauka sana ukilinganisha na misonge iliyokuwa kwenye vyeti vyao. Ilibidi wafanye kazi saana mpaka kuweza maliza intern salama. na kimsingi walipopitishwa kwenye tanuru la muhimbili walitoka wakiwa vizuri kwa walioweza pita salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wyatt Mathewson,
Hivi unataka sema nini ktk misitari yako hapa! Maana naona unaongea 'analytical brain' mara 'analytical capacity'!!!!
Ww kweli ukae kwenye nyundo na sululu maana hicho ukisemache 'is too mechanical'!
Hivi unavijua vigezo wa ku'join' public medical schools tanzania. Hawa tayari wameshathibitisha kuanzia kindergarten mpaka form six kuwa ni vipanga! Wanapoingia kusomea udaktari tanzania ndio mambo yanapoanza paraganyika! Wakienda nje kwenye mataifa yaliyoendelea anardi na GPA mlima! Hujaelewa tatizo lipo wapi tu mpaka sasa!
Sina shaka na uwezo wa wahitimu wa udaktari tanzania ktk viwango vyote, ndio maana wameendelea kuokoa maisha ya watanzania kila siku!

Sijui umeng'ang'ania practical…mie siongelei practical, naongelea maeneo yote ya umahili, iwe theory hata practical, hawa madaktari pamoja na udogo wa GPA zao wako vizuri sana kwa mazingira yetu kuliko hao wengi wenye GPA mlima kutoka!
Hata huko kwenye uinjinia kwenu, hivi mmekwama wapi na GPA zenu kubwa mbona kandalasi zinachukuliwa na watu wa nje. Na mnapopewa mnaharibu majengo na miundombinu…tena kwanza ebu tupishe hapa naona mnayo makandokando mengi sana yaliyowashinda! Yashughirikieni kwanza yenu!
 
Je huko Urusi huduma za afya zikoje? Usitake uniambie URUSI ni wajinga kaisi kwamba wawe na elimu ya hovyo kwenye Matibabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Elimu ya urusi imeandaliwa na pia kuwa na miundombinu wezeshi za huko huko urusi! Inapoletwa tanzania bila kuwa na miundombinu wezeshi yake hapo ndio shida inapoanza tokea! Kwa hiyo haitoi majibu ya changamoto zetu za huku kwa ukamilifu wake.

Imekuwa 'designed' kujibu changamoto za kiafya za urusi na kuwekewa 'supportive infrastructures' na hivyo kufanikiwa vizuri sana huko urusi! Ya kibongo elimu yetu sio ya hovyo kama unavyojaribu kuiita ww! Elimu yetu ya mafunzo kwa madaktari wetu in a akisi mazingira tuliyonayo, na kuna miundombinu wezeshi inayoifanya iendelee kutatua changamoto mbalimbali za kiafya kwenye jamii na mazingira yetu. Naamini nimekujibu hoja yako!
 
stritglow,
Hili pia ni wazo zuri! Na hapa ndio nilisema hapo awali kuwa vyuo vya nje walimu wa biomedical sciences ni 'scientists sio madaktari wa binadamu kama ilivyo tanzania. Na hii pia na hasara zake ukilinganisha na kumtumia daktari…ila kwa sabubu ya maada iliyopo mezani sitaki kwenda huko kwa leo!
 
Tatizo vyuo vyetu havina standard yoyote wa muhas anapata gpA ndo wakati yule wa wa imtu ambaye anafundishwa na mwalim yule yule anakuwa na gpa kubwa

Wa IMTU anafundishwa na mwalimu wa part time wa MUHAS ambaye continuation ya kupata contract yake kifundisha IMTU ipo tied na wanafunzi wake wa huko IMTU kufaulu afterall hiyo ni private institution! So anakuwa lenient kidogo huko imtu!
Sent from my iPhone using JamiiForums
 
GPA (namaanisha iliyo patika kwa kusoma na kuelewa) inaonyesha mtu yuko vizuri kichwani anaweza ku analyse mambo na kuja na solutuion mbali mbali zitakazo tatua tatizo.

Sasa akiwa na uwezo mzuri wa ku analyse mambo na akiwa mzuri kwenye kufanya vitendo basi huyo ndiye almasi nnayoitaka! sitaki mtu ambaye yuko nusu nusu!

Umeelewa?

GPA za kweli hazina tatizo ila hizi baadhi ya GPA za Tanzania ambazo watu wamezitumia kuingia bungeni na kudai wanayosema ni kweli hata kufikia kuomba kwenda kutoa ushahidi mbele ya mungu...na tuseme big NO, na ukitaka kujua GPA zetu za baadhi ya madaktari wetu ni fake kiasi gani basi nenda Hospitalini uone physical practice yao kwa mgonjwa unaweza kufa wewe observer na ukamwacha mgonjwa akiugulia
 
Hero,
Mkuu

Unaonesha kiwango cha hovyo sana ku-attack Engineering as if mimi nime-attack chochote kuhusu Medical School

Mimi nilikua hapa kukataa hoja yenu ya kupunguza GPA,basi,sija-attack Medical School

Waliosoma Engineering au Medical School ukubwani,walipokua Form Four walikua na marks sawa all across the board

Walianza kutofautiana kwa somo moja walipoenda ALevels.Chuo Kikuu ndio wakatofautiana zaidi

Kuja hapa na kuanza kuadharau eti watoto wa Engineering hawana akili ni upumbavu wako usio na maana kabisa!

Engineering ina matatizo nchi hii kama ilivyo medicine.Hakuna wa kumcheka mwenzake.Wote tunatakiwa ku-improve.

Hoja hapa ni ya kupunguza GPA ambayo umeshindwa vibaya maana unaleta sababu za binafsi kujipendelea wewe na wenzako!

Naomba ujikite kwenye msingi wa majadiliano.Kwanini unataka cut off GPA ya kua lecturer kwenye Medical School isiwe 3.8 na iwe 3.5?Jibu huna.

Na kujifanya eti watoto wa medicine Tanzania ni bora za ya wa nchi za nje sijui data umepata wapi na ulikua una compare na nchi zipi hasa?Weka majedwali hapa

Nilichogundua wewe unaangalia ugumu wa kusoma Medicine ulioupata pamoja na wenzako basi ni general worldwide,sio kweli,kuna walioona ilikua ni nzuri na challenging na wakapata marks zinazotakiwa!

Ugumu upo generally,tatizo wewe umegeuza eti ni crisis hivyo GPA zishushwe kuwafata nyie,which is nonsense kabisa!
 
Sijui kama nimekuelewa unataka nisemeje!
Nachokumbuka tulipokuwa intern pale Muhimbili miaka hiyo, hawa jamaa waliokuwa wanakuja na vyeti vya misonge ('A') kutoka urusi na uarabuni walikuwa wanaitwa MD-russia yaani ni vilaza maana walikuwa wanapata wakati mgumu sana kwa mchakamchaka wa machief pale Mubimbili na wengine waliishia kukimbia kabisa. Mimi pia nilihusika pia kuwasaidia saana hasa katika ku'manage' wagonjwa! Kiukweli walikuwa wamepauka sana ukilinganisha na misonge iliyokuwa kwenye vyeti vyao. Ilibidi wafanye kazi saana mpaka kuweza maliza intern salama. na kimsingi walipopitishwa kwenye tanuru la muhimbili walitoka wakiwa vizuri kwa walioweza pita salama.
Muhimbili mna-complicate pasipo sababu. Mnaponda waliisoma nje lakini ndipo wengi wanapoenda kutibiwa na kupona nyie mmekalia semina na kukamata wanafunzi
 
mtena,

Swala la uniformity ni mhim sana hasa hapa kwetu kuna chuo x kina fanya kozi A kwa semi sta moja kuna kingine hakigusi kabisa hiyo kozi kuna kingine kuna soma kozi hiyo hiyo kwa semista mbili yaani vurugu tu lakin siku ya siku wana graduate sawa sawa kama MD na GPA za 5


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wyatt Mathewson,
Lakin ukiaplay master nje wanalijua hilo au hata hapa ndani tu utaoneka disqualified be because of lowa gpa over


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lakin ukiaplay master nje wanalijua hilo au hata hapa ndani tu utaoneka disqualified be because of lowa gpa over


Sent from my iPhone using JamiiForums

Mkuu

Nje nako vyuo vipo kwenye madaraja na wana masharti yao ya kuchagua mtu

Wewe apply unapoona unapata,the utapata majibu sahihi
 
Hata huko kwenye uinjinia kwenu, hivi mmekwama wapi na GPA zenu kubwa mbona kandalasi zinachukuliwa na watu wa nje.
Kwanza ni kandarasi na sio "kandalasi"

Pili, unajua maana ya mkandarasi?

Kwenye UHANDISI kuna watu wawili 1. Engineer 2. Contractor.

Mtu yeyote anaweza kuwa mkandarasi lakini sio kila mtu anaweza kuwa ENGINEER!

Kandarasi kuchukuliwa na wakandarasi wa nje hilo sio kosa la injinia au mkandarasi wa ndani ni kosa la serikali yako!

Well, nadhani unajua miradi yetu mingi inatekelezwa kwa mikopo na kwenye mkopo nadhani utakua unajua kuna masharti! na mikopo mingi sharti moja wapo ni lazima uchukue mkandarasi kwa aliyetoa mkopo!

Kama china imekupa mkopo basi ni lazima utumie wakandarasi wao! Sasa hapo injinia wa tanzania unataka afanyaje?

Na mnapopewa mnaharibu majengo na miundombinu…tena kwanza ebu tupishe hapa naona mnayo makandokando mengi sana yaliyowashinda! Yashughirikieni kwanza yenu!

Unaongelea MKANDARASI na sio INJINIA/MHANDISI.
 
Upepo wa Pesa,
Asante kwa kunisahihisha, ila naamini umeelewa nilichomaanisha! Huko kwenye fani yenu kuna wahandisi wenye GPA za kufa mtu lakini output ni hovyo kabisa, majengo yanadondoka na khatarisha usalama wa raia na mali zao, sijui mmekwama wapi kama GPA ndio mpango mzima!? Pambaneni na hali zenu kwanza kabla ya kuanza kushadadia yasowahusu.
Tunaposimama kutaka kujikwamua ktk fani yetu ya udaktari usijaribu dandia treni kwa mbele!
 
Muhimbili mna-complicate pasipo sababu. Mnaponda waliisoma nje lakini ndipo wengi wanapoenda kutibiwa na kupona nyie mmekalia semina na kukamata wanafunzi
Siyo kwamba sisi wakufunzi wa vyuo vya udaktari tunakamata wanafunzi, isipokuwa miundombinu tuliyonayo siyo rafiki kwa mwanafunzi wa udaktari kufikia viwango vinavyotakia kuwa daktari salama. Kwa maana nyingine, ni kama watu wawili wote wanahitaji kufika point X, mmoja anabaiskeli na mwingine ana pikipiki! Ni wazi wa baiskeli itabidi afanye kazi ya ziada ili kuweza fika point X kwa wakati. Huyu anayetumia pikipiki ni sawa na hao wanaosomea udaktari ktk vyuo vilivyoko nchi zilizoendelea kwenye mazingira rafiki!

Napoongelea kuhusu kuangalia kwa upya madhara yatokanayo na matumizi ya cut-off GPA ktk kuwapata wakufunzi wenye uwezo na weledi, nipo humohumo ktk kuboresha mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi wetu wa udaktari Tanzania.
Sasa kuna watu wanaongelea ushabiki wa GPA za juu bila kuhusisha uhalisia na fani ya udaktari.
 
Back
Top Bottom