Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

Wyatt Mathewson,
Naomba msamaha kama ktk post zangu nimekutukana!
Lakini naomba nikueleze kuwa naanza kuamini kuwa u mgumu sana kuelewa na pia u msahaurifu (probably 'untrainable material'). Waelewa na wenye kumbukumbu nzuri wameshaelewa na hata 'way out' wameshaona.
Umesema udaktari 'is none of your business'. Nafikiri itoshe hivyo kuwa hayakuhusu, na hata kukuelezea ww ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Wyatt Mathewson, sina tatizo na vyovyote unavyoweza kuniita, maana ni wazi mtazamo wako ni finyu sana, kwako GPA kubwa=higher analytical/reasoning capacity/trainable. Na kama GPA yako pia ni kubwa na analytical/reasoning capacity ndio hii, kweli ipo kazi kwelikweli hasa ktk 'trainability'!

Kwa ajili ya wadau wote, ngoja nitoe ufupisho:
Kuna tatizo kubwa ktk upatikanaji wa wakufunzi vyuo vikuu vya udaktari walio na kiwango cha cut-off GPA tanzania.
Ipo haja ya wakuu wa vyuo, TCU, na utumishi kutathmini kwa upya maamuzi ya kigezo cha cut-off GPA iliyopo ktk kuwapata wakufunzi ktk vyuo vya udaktari nchini, ili kuvinusuru vyuo vyetu vya madaktari Tanzania hasa ktk 'biomedical sciences.

Baadhi ya maoni yaliyotolewa ni kama ifuatavyo;
1. cut-off GPA iongezwe (Wyatt Mathewson)

2. GPA iendelee kuwa juu na tuajiri wageni kutoka nje ya nchi wenye GPA kubwa kuja kutufundishia madaktari wetu watarajiwa kama wenye kiwango cha cut-off GPA kilichopo hawapatikani tanzania

3. Fani ya madaktari haina madaraja, hivyo tuachane na GPA kumpata mkufunzi wa vyuo vya udaktari, kigezo kiwe ufaulu wa somo husika analoomba kufundisha na uwezo wake ktk kufundisha somo husika

4. 'Vetting' zifanyike na wadau ili kuwapa wakufunzi wenye uwezo wa kufundisha ktk vyuo vyetu vya madaktari tanzania bila kujali GPA

5. Zianzishwe courses maalumu kwa ajiri ya biomedical sciences kuandaa wakfunzi husika wa wa baadaye ktk vyuo vyetu vya udaktari

undani wa hayo maoni matano hapo juu unapatikana ktk mjadala hai uliopo juu!
Wadau kama kuna lolote nimeliacha, mnaweza ongeza, niwashukuru sana kwa michango yenu muhimu sana ktk kutatua adha wazipatao wanafunzi wetu wa udaktari ktk vyuo vyetu vya udaktari kutokana na upungufu wa wakfunzi husika.
 
Wanashindwa kuelewa hii sekta ya utatibu haina tolerance ya mistakes kama sekta nyingine huku!

Kwa mfano sisi engineering tunaruhusiwa kua na tolerance ya error 5% lakini sio udaktari!

Sasa hawa wanataka nchi ishuke iwafate kwenye GPA zao ndogo!

Ni hatari in a long run!
Unacheza ngoma usiyoijuwa!
 
Hapo hapo ukiwauliza sasa kama GPA isiwe kigezo cha kuajiri tutumie kigezo gani? Hawana majibu. Ndio maana ukabila hauwezi kwisha.
Hivi ni kweli hauoni vigezo vingine zaidi ya GPA? Duh!
 
Unacheza ngoma usiyoijuwa!

Udaktari unaujua wewe

Mimi natoa kwa perspective kama mdau na mgonjwa

Binafsi mimi mgonjwa au mlaji wa huduma nitamuamini zaidi yule aliepata Medicine GPA ya 4.5 kuliko aliepata 3.5

Kama mgonjwa nina haki ya kukubali au kukataa daktari fulani

Wewe kuongea unaongea kwa lenzi ya mtoa huduma,mimi naongea kama mpokea huduma!

Sipo hapa kufundisha udaktari au kukuelekeza lolote katika kufanya operation or what not!

GPA ibaki walao 3.8 iliyowekwa sasa hivi mimi mgonjwa nipate imani!

Huwezi jiamulia kutusukumizia GPA zenu huko kwetu kwa jinsi mnavyotaka

Sisi ndio walaji,tuna sauti ya kuongea hapa,sio unakurupuka eti haturuhusiwi kuongea lolote kisa hatujui udaktari

Sijui hii mapafu unapata wapi kudharau upande huu wetu tunaopokea huduma eti haturuhusiwi kuhoji lolote kisa eti hatujawahi kwenda Medical School

Jeeez!
 
Hivi ni kweli hauoni vigezo vingine zaidi ya GPA? Duh!

Vipi hivyo mkuu?

Nina CV 30,000

Nina watoto 30,000 wa kuwafanyia shortlist,niangalie nini?

Na ninataka watoto 20 tu

Ninaanzia GPA5.0 kushuka chini na sitakaa niangalie 3.5 kuja juu

Nisikilize maneno yako kua unaweza?

Who cares?
 
Wyatt Mathewson,
Who cares? I do care!
Huku kwetu maombi yanayokuja siyo mengi kihivyo! hata hivyo tenga muda na manpower ya kutosha kupitia zote ili kupata watu watakaotuvusha!
 
Wyatt Mathewson, Hapana, sijadharau!
Unapomtaja mhitimu wa udaktari ambaye pia kamaliza 'internship' na kupewa usajiri, huyo maana yake yupo salama kimafunzo na kikazi kutibu mgonjwa. Mimi hapa siongelei hilo, naloongelea ni kuwa huyu daktari ambaye yupo tayari kufundisha na somo husika amelifaulu na kuonyesha uwezo wa kutosha zaidi ya 'B' apewe nafasi kama ipo!
Bado unachanganya mafaili, mie siongelei mahusiano ya daktari na mgonjwa hapa moja kwa moja, nakuomba tena urudi kwa hoja ya msingi uisome kisha uulize usoelewa!
 
Nilipoingia kazini ndipo nikajua GPA sio utendaji...tena hawa maGPA makubwakubwa ndio vilaza sana kazini... there's a difference kati ya claiming na understanding...wengi wa hao GPA kubwa ni claiming gurus ila kwenye kazi most of them kawaida tu or almost hakuna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doctor equivalent? naomba unionjeshe experience yako ya utendaji wa kazi wa hao wa Urusi ambao umeonyesha kuwa siku hizi wanarudi na "A" kama zote na wale waliopitia karinyekarinye ya wale wasukuma wa Pathology enzi hizo pale Muhimbili...sema kweli tu mungu anakuona!
Dr Louis Shika
 
H

Who cares? I do care!
Huku kwetu maombi yanayokuja siyo mengi kihivyo! hata hivyo tenga muda na manpower ya kutosha kupitia zote ili kupata watu watakaotuvusha!

Kazi yako ya kuhakikisha unapata 3.8 imekushinda

Uje utupe kazi ya kujaza manpower ya kuchambua CV zako kwa maana wewe ni nani hasa?

Kwanini usitimize wajibu wako wa kuhakikisha unapata 3.8 tuliyokubaliana?

You see,nyie watoto it is always about you you you,nyie hua hamna makosa,makosa ni ya everybody else na sio nyie!

Mkikosa 3.8 kosa sio lenu ni la system,ni la walimu,ni la serikali,ni la jamii na nchi kama nchi,nyie hapana,mpo perfect!

Self entitled people!

Hebu timizeni wajibu wenu,sisi walaji ndio tunabeba gharama yote,msitusukumizie 2.0 na 3.5 zenu!

Jeez
 
Hapana, sijadharau!
Unapomtaja mhitimu wa udaktari ambaye pia kamaliza 'internship' na kupewa usajiri, huyo maana yake yupo salama kimafunzo na kikazi kutibu mgonjwa. Mimi hapa siongelei hilo, naloongelea ni kuwa huyu daktari ambaye yupo tayari kufundisha na somo husika amelifaulu na kuonyesha uwezo wa kutosha zaidi ya 'B' apewe nafasi kama ipo!
Bado unachanganya mafaili, mie siongelei mahusiano ya daktari na mgonjwa hapa moja kwa moja, nakuomba tena urudi kwa hoja ya msingi uisome kisha uulize usoelewa!

Mkuu

Anaefanya wodini na anaefundisha wote wapo kwenye system moja ya supply chain ili sekta nzima ya udaktari ikamilike na mlaji wa mwsho kabisa wa huduma zote ni sisi wananchi!

Wodini nenda na hiyo 3.5 maana ni one track mind,darasani kafundishe kwa 3.8 maana analytical ability yako ni kubwa

Sasa sijui hilo somo ukipata B tu pekee yake mengine ulifeli upewe ruksa ya kufundisha as kufundisha ni somo pekee yake?

La hasha!

Sio hilo somo pekee yake ndio fani ya ufundishaji mzima,ni mlolongo wa mambo kibao na hilo somo ni final check box

Hayo masomo mengine ulifeli kwa sababu gani?Sababu ni kua ulikua huna akili yake,full stop!

Mengine yote blni blah blah blah tupu kuvutia kamba upande wako usamehewe hayo uliyofeli!

Usijiangalie wewe tu kwenye ecosystem nzima,wewe ni tiny minute particle tu,ukiruhusiwa kuingia products utakazotoa zinatakuwa sio all around competent!

Medical lecturer bora sio anaejua upasuaji tu,ni communicator bora,ni admin mzuri,ni psychologist mzuri,ni leader mzuri anaejua kuwaelekeza wenzake,etc ,yaani yupo good all around!
 
Nilipoingia kazini ndipo nikajua GPA sio utendaji...tena hawa maGPA makubwakubwa ndio vilaza sana kazini... there's a difference kati ya claiming na understanding...wengi wa hao GPA kubwa ni claiming gurus ila kwenye kazi most of them kawaida tu or almost hakuna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa uhandishi huu sio bure na wewe utakua na kaGPA kadogo. Sasa kama kuandika hujui alafu ungekua umemuandikia mgonjwa dawa si mgonjwa angepewa dawa isiyo sahihi na wenda angekua amesha kufa?

Na ndio maana tunapambana GPA izingatiwe maana tukiendeleza mfumo wa zamani watu kama wewe mtatuletea matatizo pamoja kuua wagonjwa huko wodini!
 
Naomba kuelimishwa jambo moja la zamani kidogo, kuna wale jamaa yaani Doctors ambao walikuwa wanasoma huko Urusi na walikuwa wakirudi na vyeti vyao vimeandikwa Diploma in Medicine lakini wanaajiriwa kama MD sawa na hawa waliopita kwa taabu zote pale Muhimbili je wao huwa na GPA ya mtindo gani?
Mi nadhani neno Diploma ndilo limekuchanganya, huko kwao hata cheti cha high school wanaita diploma.
Mimi kuna kipindi nilienda Marekani kufanya kiji course fulani, nilipipokelewa wakaanza kuniambia niwape Diploma zangu, ilinichukua muda kuwaelewa, lakini nilikuja kuelewa huku tunaita vyeti au certificate wao hujiita Diploma.
 
Tatizo letu watanzania huwa tunajiona sisi tu ndio tunaakili, na vyuo vyetu ndio vyuo sana.

Haya ma GPA waliotuletea ni wamarekani.

Lakini mimi siamini saana haya ma GPA naamini uelewa wa mtu.
 
Sina uhakika sana, lakini kwa kuwaida huwa wanaangalia 'coverage' kwa upana na kina (breadth and depth) ya mtaala waliosomea na muda waliotumia. Inapoonyesha kushabihiana na MD course basi mtu anaweza tambuliwa kama 'doctor equivalent'!
Muwakubali kwamba nao ni madaftari au doctors tu, haya ya kuwadharilisha eti doctors equivalent sio mazuri kabisa.
Nadhani equivalents labda ni Clinixal Assistants na Assistant Medical Officers.

Mnakoelekea mtawakataa na MBCh mkidhani MD peke yao ndo madaktari.

Mbona Marekani MD na DO wote wako sawa, na nchi moja title tofauti lakini hakuna shida.
Mlikuwa na waponda wa kurudi na india mbona wako vizuri tu.
 
Back
Top Bottom