bulletface
JF-Expert Member
- Jul 14, 2017
- 354
- 392
Nilishaona vyuoni huku nikama kutesana, kunyanyasana, kuzarauliana tu, nakumbuka prof.mmoja pale Sua siku moja anatuambia ili mgraduate mpaka nione jasho la damu linawatoka, nikaja kumuelewa semista ya mwisho, aise halikaza paper kila mtu alikohoa kwenye mtihani
Sent using Jamii Forums mobile app
Masiya,
Nafikiri ni muda muafaka wakuu wetu wa vyuo wajitafakari kama kweli wanalitendea taifa hili haki au wapo kwa ajiri ya kupambana kulinda vyeo vyao. Haiwezekani unahamisha gori kulipeleka mbali afu unalifinya(kulipunguza upana na urefu) kisha mwenyewe unaanza kulalamika kuwa magori hayapatikani baada ya kutoka bilabila…hizi ni kama hadithi za Abunuasi! Wachukue hatua badala ya kulalama corridor-ni/pembeni!
Nikiangalia MUHAS, UDOM-medical school, UDSM-MCHAS vinatia aibu sana kwenye maeneo ya Biomedical Sciences hasa hayo niliyoyataja kwenye hoja ya msingi na unakuta wakuu wa vyuo husika kama vile hawajielewi! Wanalalamika tu wanalalamika tu sijui mpaka lini…si wakutane na wafanye maamuzi na wayapeleke TCU na utumishi ili kuendana na uhalisia. Idara nyingi kama (Human Anatomy (Anatomia ya Binadamu), Human Physiology (Fisiologia ya Binadamu), Human Pathology (Pathologia ya Binadamu), Pharmacology) ziko hoi bini taabani. Kama kitu hakitafanyika mapema iwezekanavyo kuna 'crisis' ya kujitengenezea inakuja na kwa kweli imeshakuja ktk baadhi ya idara ktk vyuo vyote hivyo.
Katika kuziba vilaka wanajaribu kukimbilia waliosomea biomedical sciences za wanyama ambao hata hivyo hupwaya sana katika ku'merge' na Human Anatomy (Anatomia ya Binadamu), Human Physiology (Fisiologia ya Binadamu), Human Pathology (Pathologia ya Binadamu), Pharmacology.
Natamani hawa jamaa (wakuu wa vyuo vikuu vya uma wangetumbuliwa kwa uhujumu elimu ya juu tanzania. Vinginevyo wayapishe majukumu waliyopewa kama yapo juu sana kwa uwezo wao!
Sent using Jamii Forums mobile app