Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

Umejiona unavyopuyanga sasa?

Unaulizwa hiki unajibu mengine. Rudia tena kusoma maswali niliyokuuliza alafu linganisha na mashudu uliyojibu hapa.

Nimekuuliza TEC kumkosoa na kumpinga Magufuli aliyekuwa mkristo na mkatoliki mwenzao unakuja kuleta maelezo ya Mzee Mwinyi na Nyerere.

Unaongelea suala la Lissu kwa kwa kuhusisha na Acasia kwani kesi tulizoshtakiwa na kulipa matrilioni ya pesa za walipakodi ni kesi ya Acasia?

Hujui kuhusu Winshare? Hujui kuhusu Nachingwea? Hujui kuhusu Rukwa? Lissu alishauri kuhusu utaratibu sahihi wa kisheria kufuatwa kabla ya kufuta leseni za wawekezaji wa madini. Na aliposema tutashtakiwa MIGA alimaanisha tusipofuata hizo taratibu tutachukuliwa hatua za kisheria.

Hujui kuwa tumechukuliwa hatua za kisheria? Hayo makesi yote hujui tumelipa pesa nyingi za walipakodi baada ya kushindwa?
 
Hakika mkuu, social order ya nchi yetu imeharibiwa vibaya sana na wanasiasa wapuuzi na wabinafsi waliohakikisha wanazima siasa zote rasmi za kweli za upinzani, ukosoaji makini na mawazo mbadala na sasa wanataka kuiparamia na TEC kutepeleka wote gizani kabisa wote tuwe makondoo tunaoishi kwa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti.
 
Suluhu ni kumpata Rais asiyekuwa Mkatoliki wala Muislamu.

Na ndipo itazaliwa Tanzania mpya.
 
The Bigger Picture is:

Politicians think about the next election. Statesmen think about future generations.
​
Hoja, it's not about POLITICIANS. It's about HOJA ZA UMMA.

Hata mwanasiasa anayepata nguvu ni yule anayesimama na HOJA ZA UMMA.
Ni lini TEC walikataa BUSARA?

Ni lini TEC walipinga MAZUNGUMZO?

Watawala wa ovyo ndio waliotyfikisha hapa kwa kwenda KUMPIGA NONDO KUMUUA PADRE KITIMA na KUUWA MAELFU ya WATU.

Unataka UUE MAELFU ya watu, halafu maisha yaendelee tu, kama.HAKIJATOKEA kitu.

Ili mauaji iwe ni TABIA yako, kuua tu, kwasababu baada ya MAUAJI maisha yataendelea????
Kioa mtu mwenye akili timamu, alijitahidi kadri ya uweso wake, kuhakikisha taifa halifiki hapa tulipo.

Ila MITAWALA ikaona njia ni KUTEKA, KUUA, KUFUNGA watu, tena wengine ni vitoto vidogo visivyo na madhara kabisa.

Mzee Nyerere alishawahi kupambana na TEC, akawalima barua ya kutisha kweli.​
Hiyo barua iko wapi?
Alipambana nao kuhusu nini?
Jitahidi kuweka hoja za sababu. Siyo maneno tu na watu.
Nadhani jitahidi sana kutofautisha MAPAMBANO na KUTOFAUTIANA.
 
Suluhu ni kumpata Rais asiyekuwa Mkatoliki wala Muislamu.

Na ndipo itazaliwa Tanzania mpya.
Tanzania haipo kwenye udini. Idadi kubwa ya Watanzania ambao ni vijana hata hizo dini wanazitumia kwa mazoea tu na wengine hawaziamini kabisa.

Tanzania inahitaji haki, utawala bora na mifumo sahihi ya kulisimamia hili Taifa hasa wanasiasa.

Nchi hii ni tajiri sana, tukiwa na mifumo imara na utawala bora nchi yetu inaweza kuwa nchi ya mfano sio tu Afrika bali hata dunia nzima kwa maendeleo ya kweli na mafanikio.
 
Bwana Mpwimbe, Acacia hakuwahi kusajiliwa nchini Tanzania.

Acacia walikuwa wanafanya biashara bila A Certificate of Compliance. Hili silo suala la kimkataba bali suala la usajili na hata ukienda BRELA kwenye A Register of Companies taarifa ungezipata. Lissu kusema kwamba makinikia yasikamatwe kisa tutashitakiwa MIGA au kwingineko was impulsively misleading.

MAFISADI Sijawatetei na Sijawatetea. Lissu nasimama naye mpaka mwisho kwasababu nilipishana naye hoja kisomi siyo kisiasa. Hili wengi hamtaki kukubali.
================================================================

Kuhusu TEC vs CCM vs BAKATWA Rift.

Samia amekosea sana kucheza karata za udini, kwamba wanamkosoa kwasababu yeye ni muislamu. TEC imekosoa maraisi wote wa Tanzania, hivyo Samia yeye kutotaka kukosolewa yeye ni nani ??? TEC wamekosoa mauaji ya watanganyika na katika hili historia iko upande wao mpaka mwisho.

Tatizo ni kwamba huu ugomvi mbali na kuhusu mauaji, CCM chini ya Samia wameenda mbali na kuanza kunyooshea vidole mambo mengine pia ambayo viongozi binafsi ndani ya TEC waliwahi kuyafanya hayakuwa mazuri hapa nchini. Kuamini kwamba baadhi ya maaskofu hawana makosa wamewahi kufanya ni kujilisha upepo na kujidanganya. Kuna mengi tu ya kutisha waliwahi kukosea maaskofu.

==================================================================
Mvutano huu ulipofika ni pabaya kwamba, TEC wameshika Samia pabaya. CCM wameamua kuungana na BAKWATA kuligawanya taifa kwa kuanza kutaja hata mambo mengine ambayo yataligharimu taifa. Ifahamike kwamba usalama wa Tanganyika na hii kanda nzima ya Africa, inategemea ushirikiano baina ya TEC+CCM+BAKWATA. Kwanini wamefika hapa bila kutafuta A Common Ground ???

Samia ataondoka na kiukweli hawezi kushindana na Catholic Church na hata yeye analifahamu vizuri hili. Lakini, nini kitatokea baada ya Samia kuondoka. Unadhani huu mpasuko utapotea tu ndani ya usiku mmoja kisa Raisi amekuwa Tundu Lissu ??? Hebu tusaidiane hapa
​
 
Ndio maana nikasema,

Kupata Tanzania mpya,

Lazima tumpate kiongozi asiyepokea mashinikizo toka bakwata wala Tec.


Tukianzia hapo, tutafanukiwa vyema sana.
 
Mi nasaidia kujibu moja kwa sasa,

Walivyoshtakiwa kwa papa, badala ya kujibu kistaarabu wao wakawatukana wenzao
Huu ulikuwa ni udhaifu
 
Na wameshajaribu sana.

Kugawanyisha TEC, kuua (Kitima) na KUTEKA.

Hivi vikelele ni kuwa WAMEGOTA.

Na hakuna wakati TEC imeungana vilivyo kama sasa.

 
Akiua, KUFIRA, KUTEKA WATU, NEPOTISM ataambiwa.

Kutokuwa na DINI siyo JIBU la MUUA watu, MUTEKA na KUFIRA watu.
Kwani nani kakwambia Tec na Bakwata ndio dini pekee?

Fikiri kwa undani.

Bakwata na Tec + CCM ndio wametufikisha hapa.

Kuanzia up ya ni kuwaondoa wote, tuongee namna Bora ya kujenga nchi yetu bila kutumia hizi taasisi fake copy ya watawala wa kimasonry.
 
US waliweza kuwatia Tec na Bakwata wakafanikiwa.

Nasi twaweza.
 
Kwahiyo makinikia yalikamatwa kwa sheria ipi?

Hata hivyo mbona mpaka leo bado yanasafirishwa?

Unapokuwa na mikataba ya siri ya madini. Sauti zote mbadala ni sahihi mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo.

MAFISADI Sijawatetei na Sijawatetea. Lissu nasimama naye mpaka mwisho kwasababu nilipishana naye hoja kisomi siyo kisiasa. Hili wengi hamtaki kukubali.​
Unapishana naye kwenye hoja zipi?

Mikataba ya madini iko wapi?

Ili sisi Umma tujue kati yako na Lissu ni nani alikuwa mkweli.
Sasa mambo binafsi ya VIONGOZI wa Katoliki yanahusu nini Kanisa Katoliki?

Kama yanavunja sheria na hawachukuliwi hatua, maana yake DOLA ZIMA limekufa, limefeli.


Mambo gani yanatjwa?
Ifahamike kwamba usalama wa Tanganyika na hii kanda nzima ya Africa, inategemea ushirikiano baina ya TEC+CCM+BAKWATA. Kwanini wamefika hapa bila kutafuta A Common Ground ???​
TEC na kila mwenye akili timamu alisema kabla hatujafika hapa.

Watawala walikaza fuvu na mpaka sasa bado wanakaza fuvu.

Kuanza upya haijawahi kuwa ujinga.
Nani amesema Rais awe Tundu Lissu?

Tunataka UTAWALA WA SHERIA, HAKI ZA KIRAIA, HAKI ZA KISIASA, THAMANI YA KURA, HAKI YA UHAI hata kama Rais akiwa WANU na Makamu wake MCHENGERWA.

Kuheshimu TARATIBU TULIZOJIWEKEA WENYEWE kwa HIARI kuna SHIDA gani??
 
Hakuna sehemu nimesema hizo ndio dini pekee.
 
Suluhu ni kumpata Rais asiyekuwa Mkatoliki wala Muislamu.

Na ndipo itazaliwa Tanzania mpya.
Mnaongea mambo kirahisi sana na huwa nawashangaa mno.

Tanganyika ni nchi ambayo katika huu ukanda wetu ina idadi kubwa sana ya Waislamu walioelimika kuliko sehemu nyingine za huu ukanda. Waislamu wa Tanganyika wana sifa kubwa za kipekee: UVUMILIVU WA HALI YA JUU.

Tunapenda kuwabagaza sana Waislamu wa Tanganyika ila ukweli ni kwamba ndugu zetu wana kiwango kikubwa cha Tolerance kuliko hata Zanzibar. Ukienda hata Nigeria huwezi kukuta ushirikiano mkubwa baina ya Wakristo na Waislamu kama ilivyo hapa nchini Tanganyika. Kule Zanzibar Wakristo wanabaguliwa mno na waislamu.
====================================================================

KIUSALAMA, Tanganyika imekuwa ndiyo kinara wa ulinzi ukanda huu kwasababu mitandao mingi ya kigaidi inafamika vizuri na vyombo vya usalama vya Tanzania. Waislamu wa Tanganyika ndiyo wanasadia kupambana na mitandao ya kigaidi kama Al Shabaab, Boko Haram, ISIS, Al Qaeda na Waislamu wenye misimo mikali kama The Muslim Brotherhood.

Miaka ya 2000's wakati ugaidi umeshamiri kwenye ukanda wetu TISS ilisaidia mno kuimarisha usalama kwasababu ilikuwa na taarifa nyeti kuhusu mitandao ya waislamu wenye msimamo mkali kwenye ukanda huu. Watu kama Balozi Adadi Rajabu ambaye ni Muislamu kindakindani ndiyo walikuwa vinara wa kupambana na magaidi. CIA na MI6 mpaka leo hii wanategemea taarifa kutoka TISS kuhusu mitandao ya kigaidi.

Marekani walipoanza kuvutana na Magufuli, aliwaambia TISS waache kuwapa CIA taarifa za kiintelijensia kuhusu makundi ya kigaidi ukanda huu. Huu ni ukweli ambao wengi hamuujui.

CCM iko madarakani mpaka leo hii siyo kwasababu wameshindwa kuitoa, ila kwasababu usalama wa Tanganyika is within the best interest of everyone. Kenya, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Uganda, Zanzibari, Somalia, Ethiopia na Congo zote zinategemea usalama wa Tanganyika. Waislamu wa Tanganyika mbali na madhaifu yao, wana uungwana mkubwa.

Siku hali ya siasa ikiwa mbaya hapa nchini na ukatokea mpasuko baina ya Wakristo na Waislamu, mitandao ya kigaidi itajipenyeza na kuvuruga ukanda wote huu. Marekani na Uingereza wanafahamu fika, ndiyo maana kuna ujinga wa CCM wamekuwa wakiuvumilia. Samia na genge lake wameanza kugawanya nchi na hili lina madhara. Wakristo wengi wameingia mkenge kwenye hii vita (They Took The Bait).

NIKUPE MIFANO HAI: Majasusi wa Tanzania wengi wamekufa sana Sudan, Nigeria na Somalia. Wengi wao ni vijana wa kiislamu waliokulia madrasa. Wamekufa wakilitumikia taifa kuhakikisha mimi na wewe tunaandika ujinga hapa mtandanoni. Siku unadhani mpasuko ukiwa mkubwa naina ya TEC na BAKWATA, hata hizo BARUA ZA KIKUHANI zitaandikwa kweli ????
================================================================
AU nawewe unaamini propaganda kwamba CATHOLIC CHURCH lina intelijensia kali ya kuweza kujipenyeza kwenye mitandao ya kigaidi bila msaada wa waislamu waungwana ???

-Mwisho wa haya yote utakuwa nini ???

-Hakuna njia nyingine za mazungumzo ambazo zinaweza kufanyika kuliko hii ya kutunisha misuli na kuzidi kutugawa ???
​
 
Ndio maana nikasema,

Kupata Tanzania mpya,

Lazima tumpate kiongozi asiyepokea mashinikizo toka bakwata wala Tec.


Tukianzia hapo, tutafanukiwa vyema sana.
Ni mashinikizo gani TEC na BAKWATA wanatoa???
 

Hujajibu maswali niliyouliza. Nimesisitiza kwa context ya Tanzania. Dini zote huko nyuma zimetumika vibaya ukiangalia historia.

Umewashutumu TEC. Baraza la maskofu Tanzania.Tunaongelea wakatoliki wa Tanzania. Jikite kujibu haya maswali

Tafadhari toa jina la hao viongozi Wakatoliki, vituo vyao vya kazi hapa Tanzania na walisema hayo mambo unayowashutumu wapi, lini, wakilenga nini, context ku-support na kuthibitisha madai yako, tuwekee ushahidi wa video au text kwenye madai yako namba hapo chini 1-5.

1.Viongozi wa Katoliki huwa wana udini uliopitiliza.

2. Wanaamini hii nchi ni mali yao.

3. Wanajiona wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU.

4.Ukiwasikiliza huwa hawaelewi kwanini wanatetea mengi wanayotetea.

5.Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…