Ndugu MPWIMBE, hakuna haja ya kufanya mjadala kwa ghandabu.
Hakuna MJADALA TIMAMU uliojengwa kwenye UONGO, ILLUSIONS na STORI ZA KUFIKIRIKA.
Unataka mjadala TIMAMU jenga hoja kwenye USHAHIDI.
Tunajenga nchi moja na wala hakuna anayefurahia unyanyasaji ambao watanganyika na wazanzibari wamefanyiwa. Pengine nadhani tunapishana padogo sana, hebu jaribu kunielewa tena katika hili.
Hufurahii unyanyasaji, ila wanaopinga unyanyasaji WANAKUKERA.
Kasimulie wajinga hizi stori.
Mosi, TEC wamekuwa wakikemea maovu na kuonesha misimamo yao ya kisiasa tangu awamu ya kwanza. Hili ni muhimu kulifahamu kama msingi wa mjadala wetu.
Binafsi, sijawahi kuona TAMKO la TEC la Kisiasa, kama lipo liweke hapa.
Matamko ya TEC ni ya KIBINADAMU, KIUTU na KIJAMII kama UHAI, HAKI ZA KIRAIA na KIBINADAMU.
Sijaona TAMKO la TEC la kusema WANANCHI WACHAGUE MTU FULANI. Kama lipo liweke.
MAUAJI, WIZI, UPORAJI, RUSHWA, DHULMA siyo SIASA.
Pili, TEC wamekuwa wakivutana hadi na viongozi wa kikristo akiwemo Mzee Nyerere na Mzee Mkapa. Minong'oni inasema Mzee Mkapa alishawahi kwenda kupiga magoti kwa Kadinali kuomba msamaha (Hii ni minong'ono tu haina ushahidi). Swali, je kweli Samia anapingwa na TEC kisa uislamu wake au kuna jingine ???
Kupiga magoti kwa KADINALI kama Nani??
ALikuwa kiongozi wake wa Kiroho au kama nani??
Maana Kadinali siyo kiongozi wa Maaskofu Katoliki kama ambavyo vibuyu wa CCM wanaamini.
Tatu, TEC kama taasisi inayoongozwa na watu ni FALLIBLE. Kuna makosa mengi ya kihistoria ambayo mbali na mauaji haya ya kukosolewa, jambo ambalo naunga mkono asilimia 100000%, kanisa liliwahi kukosea kwa kuleta udini hasa kwenye suala zima la utoaji elimu.
Udini upi?
Hebu share hapa huo udini ulioletwa na TEC kwenye elimu.
Hili ni kosa ambalo wengi hatupendi kulisema. Kitendo cha kutaka wasomi wawe Wakristo tu limelichafua kanisa mpaka leo hii.
Hii mada yako, naona NI MATAPISHI YA PROPAGANDA in and OUT.
Umekula KITIMOTO iliyochacha???
Yalikuwa ni makosa na Mzee Nyerere alirekebisha kwa kujenga umoja wa kitaifa. Swali langu hapa ni hili: Je, ni sahihi kutumia haya makosa ya kihistoria kujaribu kuifunga mdomo TEC pale inapokosoa serikali ??? (Nikatoa mfano wa Prof Richard Wolff vs Prof Jordan Peterson)
Hii ilikuwa mwaka gani??
Hoja yako ni nini?
Tuko page ya 4?
Naona kila ukiandika ni KINYESI tupu.
Nne, nimetoa mfano wa kimuktadha wa UFILIPINO nikitegemea kwamba wengi baada ya kusoma wangeenda kufanya utafiti zaidi na kufahamu nini kimemkuta bwana Rodrigo Duterte ambaye aliua maelfu ya watu na kanisa lilipomkosoa kupitia BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) la Ufilipo alianzisha vita dhidi ya kanisa kwa kusema hawatakiwi kumkosoa kwasababu hawana MORAL AUTHORITY kutokana na makosa ya kihistoria na makosa binafsi. Leo hii Duterte ameiingiza familia yake kwenye mgogoro mkubwa na yuko ICC, lakini CBCP ambayo maaskofu wake waliuwawa na kutekwa bado ipo inaendelea. Nilitegemea kwamba wengi mngekuwa mshang'amua maana huu ni mfano hai.
Sisi kama umma tuna HOJA ZETU.
Wanachozungumza TEC ni SAUTI yetu.
Maana sisi tukisema MNATUMUDU, Ndio maana kina MDUDE, DEO SAKA, KIPANYA hawapo.
TEC wanasema kwa niaba yetu. Hizo stori zao za nyuma sisi hazituhusu.
Tano, kwasasabu huu ni mjadala endelevu nilitegemea kwamba tungezungumza kwamba huu mgogoro ambao upo kwasasa na una lengo la kuligawa taifa, ulianza lini ??? Kama kawaida wengi tunaangalia dalili bila kuchimba kiini cha tatizo (We look at the symptoms not disease). Viongozi wa kidini kuanza kutekeswa na kushambuliwa ilianza kipindi cha awamu ya nne. Tuliona mapadri wakishambuliwa kwa risasi kule Zanzibar, huku mwingine akiuwawa.
Wenye akili timamu wana dili na SOURCE.
Hapa unachojaribu kufanya ni kutupia LAWAMA wasiohusika na kutaka ku-NORMALISE UJUHA na MAUAJI.
Kipindi cha JPM ambaye ni Mkatoliki mambo yalikuwa mabaya kupita kiasi kwasababu Mapadri wengi walikimbiziwa uhamishoni kwasababu alikuwa anawawinda. Kilichoshangaza zaidi ni kwamba Maaskofu walisaidia sana kumuweka madarakani bwana JPM na alikuwa ni kijana wao wa seminari.
Walisaidiaje?
Mapadre gani walikimbilia uhamishoni??
Unatapika sana UJUHA kwenye hii mada.
Magufuli aliwekwa na Mkapa kama kijana wa Mkapa, na ushahidi uko humu, tangu mwaka 2014.
Kwamba TEC walimweka, kwahiyo TEC ni NEC ya CCM, na Halmashauri kuu ya CCM.
Kama TEC walimweka MAGUFULI, kwahiyo Samia kawekwa na BAKWATA???
Haya yote ambayo anafanya leo hii Samia kushambulia mapadri yana mlolongo mrefu (The did not just exist in a vacuum, it's a long-coordinated government policy).
Kwahiyo kama yana mlolongo mrefu ndio yanatakiwa kuendelea???
Sita, mambo haya mwisho wake ni hasa utakuwa nini hasa linapokuja suala la usalama wa nchi. Tanzania hakuna UKABILA ila kuna UDINI sana. Kweli imeshindikana kwa CCM+BAKWATA+TEC kuyamaliza haya mambo nyuma ya pazia kweli ??? Ni ukweli usiopingika kwamba CCM+BAKWATA+TEC ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwa usalama wa nchi na ukanda huu. Kuna taarifa nyeti huwa hazitakiwi kufika hadharani kwasababu huwa zinaleta hisia kali baina ya wafuasi.
Wayamalize vipi?
TEC walishatoa USHAURI hata kabla ya uchaguzi na baada ya mauaji wakatoa ROAD MAP.
Hawajaua mtu na hawana hatia.
Wenye hatia wawajibike. Jambo rahisi tu.
Alichokifanya Samia siku ile kilikuwa Unprecedented, lakini hata yeye ni zao la tatizo. Tatizo kubwa limejificha kwa chini ambapo hata akiondoka litaendelea kuwepo endapo hatutakubali kukaa chini na kujisahihisha.
Ukae chini nani na nani?
Hata haya mauaji wengi tuliyazungumzia humu tokea mwaka 2015 mpaka kufika sasa kwasababu tuliona mazingira mabaya. Hivyo hata Samia akiandoka nchi haiwezi kuwa na utulivu. JPM aliondoka na mambo yakawa mabaya mara mbili, unadhani Samia akiondoka ndiyo tatizo litatulia ???
Samia kachaguliwa na nani?
Kaua watu ili amtawale nani??
=================================================================
TANZANIA ilifanya makosa mengi sana miaka zaidi ya 30 iliyopita na mnachokiona sasa ni matokeo tu. Ukiamini kwamba Samia ndiyo tatizo pekee utakuwa unajidanganya na nimeona niwaambie ukweli wote leo bila kuuma maneno. Huko ndani hali ni mbaya na hakuna maelewano na watu wanataka kugawana mbao.
Wenye matatizo zaidi ni waliozika. NGUO.
Matatizo ya MUUAJI, MFIRAJI na MTEKAJI hayawezi kunihusu.
WIZI, UPORAJI, MAUAJI, UTEKAJI ni matendo ya hiari ya KUJITAKIA.
HAKI LAZIMA IPATIKANE, lakini TRANSITIONAL JUSTICE inahitajika hapa. Twende kwenye kiini cha tatizo siyo dalili hizi. Haya muaji ya 2025 ni madogo ukilinganisha na mauaji mengine yatakayotokea siku za mbeleni. Rwanda kabla ya Genocide ya 1994 kulikuwa na muaji mengine makubwa mno, lakini watu kwakupenda kupuuza wakaona siyo ishu. Yalipotokea mwaka 1994 hakuna aliyeamini na kila mtu akawa muhanga.
============================================================
NATAMBUA HIZI MADA huwa zinaleta sana hisia kali, lakini wewe kama msomi hutakiwi kupelekwa kama WIMBI LA MAJI. Lazima ukubali kufanya mijadala inayouma ili uweze kufahamu upande mwingine unawaza nini. Mbali na kutumika kwa karata za Udini, kuna baadhi ya madai ya Waislamu yamekuwepo hapa Tanzania kwa miaka mingi bila kuzungumzwa kwa uwazi. Samia alipowahadaa waislamu kwamba atawasaidia madai yao wengi wamemuunga mkono kwenye huu ufedhuli wake. UKISHINDWA KULIFAHAMU HILI BASI TENAAAAA.
MJADALA TIMAMU unajengwa kwenye UKWELI na USHAHIDI.
Siyo PROPAGANDA MAVI unazojaribu kutapika hapa ndani.