"Sijafurahishwa" na ushindi wa Mwabukusi: Kwanini ninasema hivyo...

Magufuli hakuwa na muda wa kuingilia mambo ya TLS ndio maana wakosoaji wake wakubwa Lissu na Fatma Karume uraisi wao ulikuwa kipindi chake.

Hata ilo Sakata la Mwabukusi ni mambo ya siasa za TLS tu, sema mnayakuza sana.
Mwabukusi ni Wakili pekee aliyeenda Mahakamani kupinga Mkataba mbovu wa DP World.

Kwa mtu anayejielewa na timamu kichwani lazima amuunge mkono kwasababu ni uzalendo na kulinda rasilimali zetu dhidi ya kukwapuliwa na waarabu.

Wamasai wanatimuliwa kwenye ardhi yao kwenda zaidi ya kilometa 540 ili kupisha waarabu kuiba rasilimali zetu.

Madini ya kwenye hifadhi zetu yamepewa baraka ya Rais Samia yachimbwe.

Nchi inapigwa Mnada hii ( Ndugai)

TLS inahitaji mtu jasiri na aliyeonesha mfano kutetea wananchi Mahakamani kulinda rasilimali zetu dhidi ya waarabu.
 
Ndio haya ya β€˜expectation gap’, good-luck.

Kama unadhani serikali aina mandate ya kufanya maamuzi ya matumizi ya ardhi.
TLS inawaonesha wananchi serikali imekosea wapi.

Kazi kwenu nyie wananchi kuchukua hatua.

Kwasababu TLS sio muwakilishi wa wananchi, wawakilishi wenu ni Rais na wabunge.
Wakikengeuka nyie ndio mnachukua hatua kuwajibisha kama Kenya.
Msikae huko kwenye sofa mkidhani TLS ataenda kuwajibisha Serikali nyie mkiwa mmerelax.

Hapana, kila mmoja acheze nafasi yake, namna hiyo mambo yataenda vizuri.
 
Hii 'minimal impact' ni ipi? Hawa TLS walishawahi saidia wapi? Msiwarembe sana waambieni ukwel hawana impact yeyote Katika jamiii
TLS imeanza 1954, wewe unaijua TLS ya Lissu & Karume (2017-2018).

Hiyo Katiba yenye haki za Binadamu, Tume ya Uchaguzi & Mfumo wa vyama vingi vya siasa ni matokeo ya Movements za TLS tangu Nyerere.

Hivyo, mchango wa TLS 1954-2024 ni Mkubwa. Kasome historia yake ambayo wanasiasa hawataki muijue ndio utaelewa kwanini hata chaguzi za TLS zinafuatiliwa kuliko vyama vingine vyovyote kitaaluma.
 
Legitimacy ya power zao ndio inataka kila mtu awaimbie pambio za sifa na kuwa chawa wao??
 
Ccm sio wajinga kutumia nguvu kubwa harafu watu wakuamini wewe hata mjinga kabisaa asiejua kitu ataona kuna kitu sio bure haiwezekani Serikali itumie nguvu kubwa vile...
 
Wasiwasi wangu wasije wakampiga risasi tu huyu Mwabukusi kwani wakishindwa kwa hoja wanakimbilia risasi kama walivyo magaidi wote duniani wao violence ndiyo option yao.
 
Uko sawa KABISA.
 
Dah yaani wamamuibua kura nyingi sana Adv. Nkuba. Yaani hili jopo la wahesabu kura na wasimamizi nasikia hela zilitembea balaa
 
Nmekuelewa lakini wao kushindwa haimanishi Boniface atashindwa

Tuone atakachofanya
So far Tanzania is a rotten country with a dead soul
 
Tatizo la Chadema wanafikir kupata uenyekiti wa TLS ndio kuiondoa CCM madarakani hiz taasis za serikali zinaongozwa kwa sheria na miongozo
 
A
A very good analysis. Hata lisu aliwahi kusema mje kwa wingi mpige kura. hata wakiiba itafika mahali kura fake zitakuwa chahce kuliko halali. Mfano mmepenyeza kura 1,000, lakini wapiga kura ni 5,000..............fanya mfanyavyo mkija kuhesabu margin itakuwa kubwa sana kuliko kura fake! mtashinda!
Dah yaani wamamuibua kura nyingi sana Adv. Nkuba. Yaani hili jopo la wahesabu kura na wasimamizi nasikia hela zilitembea balaa
Nani kaibiwa Nkuba au Mwabukusi? unanichanganya
 
TLS ni kongwe kuliko Tanzania, ilianzishwa 1954 by Act of Parliament.

Usifafanishe TLS na vyama uchwara.

Unaonekana una wivu na wasomi wa sheria. Pole, unaweza kurudi shule!
Mimi nimesoma sheria as part time hobby nikiwa kazini na safari za majuu kila mwezi almost kwa kazi yangu ilivyokuwa, nimefuzu kabisa with B+ GPA, sikwenda law school! Sina wivu
 
Tatizo la Chadema wanafikir kupata uenyekiti wa TLS ndio kuiondoa CCM madarakani hiz taasis za serikali zinaongozwa kwa sheria na miongozo
This is your thinking! Wapi mtu wa chadema kasema hivyo?
 
Correct, wananchi wasibweteke wakadhani TLS itawakomboa including Mayor Quimby ambaye anaona TLS haina la maana wakati yeye hatimizi wajibu wake wa kuiambia serikali ukweli/kero
 
A
A very good analysis. Hata lisu aliwahi kusema mje kwa wingi mpige kura. hata wakiiba itafika mahali kura fake zitakuwa chache kuliko halali. Mfano mmepenyeza kura 1,000 fake, lakini wapiga kura ni 5,000. kura za halali za wapinzania.............fanya mfanyavyo mkija kuhesabu margin itakuwa kubwa sana kuliko kura fake! mtashinda!
 
TLS ishakuwa na raisi Tundu Lissu na Fatma Karume kama wakosoaji wakubwa wa serikali.

Sasa huyo Mwabukusi atakuja na lipi jipya. Zaidi ya kujigamba tu kwa nafasi yake

A fuss about nothing

A storm in a tea cup as far as Tanzania politics goes.
Naona unajitekenya Na unacheka mwenyewe
 
Kwani hii TLS kwa kuongozwa na ambao siyo wakosoaji, imefanya jipya lipi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…