Sijamwelewa Lema, anasema anasubiri maazimio ya Kamati Kuu, iwapo hayataeleweka atalazimika kujitetea binafsi

Kwamba maamuzi dhidi yake yakiamuliwa ndani ya vikao halali vya Chama na kwa kufuata Katiba,Kanuni na Taratibu za Kichama..yeye anasehemu nyingine ya kwenda kuyaongelea/kuyasemea!!!!???
 
Chama ukihoji , kesho yake unafukuzwa ..Wajinga tu .
 
Somaaaahioooooooo
 
Sio wa kumuamini sana, hata zamani aliwahi kuuza ubunge alipokuwa TLP. Alipoingia cdm akishindana na Batilda alitaka kuchota hela, kama si watu wa Arusha kumuambia akipokea wanammaliza angeuza tena Jimbo.
Sasa pale CDM nani mnamwamini sasa ?
 
Kwanza jiridhishe tuhuma zimetolewa wapi na nani na kwa utaratibu gani.
Ukianzia hapo nadhani itakuwa rahisi kuyasema haya unayozungumzia hapa.
Hizi tuhuma zimetolewa mtandaoni na Hilda, sijaona pengine tofauti, nakumbuka hata huo uzi upo humu JF.

Hata utaratibu aliotumia nae kutoa tuhuma aliangalia upande mmoja, hakuuliza upande wa pili unasema nini apate maoni yao ili aijue picha kamili.

Kwa hilo nimejiridhisha, Hilda nae hayupo KK ya Chadema, zaidi anaishi kwa kupewa taarifa na wengine, anaweza kupotoshwa pia, sio malaika yule, asiaminiwe 100%
 
Unaweza ku-back-up tuhuma zako na data? Ninachojua ni kuwa maeneo ya uchagani yana upinzani kuliko sehemu nyingi za Tanzania. Toa hesabu ni wachaga wangapi wamewahi kusaliti na wasio wachaga ni wangapi! Unajua Kigoma ni wangapi wamesaliti?
Humu JF mambo mengi siku hizi yanaletwa bila data au ushahidi.
Ukisema uombe walete data , agenda nyingi zitakufa kifo cha mende
 
Hilda newton ni mashine ya kutengeneza na kusambaza taarifa za uongo.
Asipochukuliwa hatua atazidi kuharibu image ya chadema
 
Hatutafanya Maridhiano yoyote bila Medieta (Mpatanishi).
Huu ndo Msimamo wa chama.
Nchi yoyote Duniani haijawahi fanya Maridhiano bila Medieta, Yaani #Msuluhishi au mpatanishi, Eidha kutoka #Sadc, kutoka Umoja wa Africa #African_Union (AU)
🗣️Kama wanania njema, Wakubali kumwachia #Lissu na Wakubali Uchunguzi ufanyike juu ya Mauaji yaliyofanyika Oktober 29, na waliouliowa watu wachukuliwe hatua, walioagiza Mauaji wawajibishwe alafu waruhusu Medieta aje, Tusuruhishe, tutunge Sheria, tutunge KATIBA, tuanze upya.
TUINGIE KWENYE MECHI AMBAYO UWANJA UNALINGANA ALAFU ZIPIGWE DAKIKA 90, WANANCHI WAAMUE.
John Heche See less
 
Uimara wa chadema ni wafuasi wasiokuwa na kadi wasioweza kufikiwa ili kushghulikiwa au kununuliwa. Mbowe amekaa pembeni bado chama kinasonga mbele.
Namna sahii ya kuishughulikia chadema ni kufanyia kazi hoja zao au kuzipinga kwa hoja kinzani zenye tija zaidi. Hata chadema ikifutwa leo hoja zao, itikadi na falsafa vitaendelea kuendesha vuguvugu la siasa [Chadema inaweza kuendelea kuwepo hata bila ofisi au uongozi rasmi].
 
Wapo wengi, mfano Jumanne Abdallah Kikungo.
Lema mmeishi naye kwa benefit of doubt muda mrefu sana lakini kila mara ameendelea kuwa na msimamo wake ule ule hamjamwamini tu.

Kama Lema hakununulika kipindi cha Magufuli alipoweka gerezani muda mrefu sana, ikaja kipindi cha uchaguzi hadi akalazimika kukimbiza familia mnadhani kwa sasa anaweza kubadilishwa na serikali chafu kama hii ?
 
Tatizo la wafuasi wa chadema ni kuamini kila ujinga unaotolewa mitandaoni.
Kuna mtu aliwaita Nyumbu siku hizi huwa namwelewa sana. They are definitely wild beast in human bodies.

Wafuasi wasioweza kuchambua agenda zinazodhoofisha chama chao ni kuzipuuza hawawezi kutengeneza taasisi imara.
IMagine sasa hivi mmeacha agenda ya kuvunjwa kwa katiba na waziri wa mambo ya ndani mnarushiana vijembe wenyewe kwa wenyewe.

Lissu, Lema na Heche wanasafari kubwa sana angalau ya kuwabadilisha hawa watu wenye mtazamo wa nyumbu wawe sungura.
 
Si lazima nimwamwini boss wangu.
 
Wapo wengi, mfano Jumanne Abdallah Kikungo.
Chadema huwa mnakivuruga chama chenu kwa upumbavu wenu wenyewe.
Mmefukuzana sana tangu kipindi cha Walid Kaborou, Zito, Dr Slaa, Covid 19 na wengineo hamjui kuwa wenzenu wanatumia ujinga wenu kuwadhoofisha ?
 
Si lazima nimwamwini boss wangu.
Hatukulazimishi lakini kwa kuishi naye kwa mashaka kwa zaidi ya miaka 20 hamuoni kuwa wenye mashaka naye amshawaprove wrong kwa muda sasa.

Anyaway wakiondoka Lema, sugu na wengineo itawachukua muda gani kutengeneza watu wa aina hiyo au lengo lenu ni kuwa chama cha upinzani milele?
 
Wafuasi wasio na kadi hawawezi kutengeneza chama imara hao ni mashabiki wa muda tu huwa wanabadilika kulingana na wakati tu.

Walid Kaborou aliondoka na wafuasi wake, Zito aliondoka na wafuasi wake, Slaa akaondoka na wafuasi wake, Mbowe kaondoka na wafuasi wake mnategemea wafuasi wataendelea kuamini taasisi yenye mtazamo wa nyegere kwamba kila msimu lazima mmfukuzane.

Hamjifunzi ?
 
Ni hivi, unajifanya uko smart lakini ni mpuuzi fulani. Huku kwenye mitandao sio kwenye vikao vya cdm. Humu watu wanajadili wapendavyo maana sio kikao rasmi cha chama, labda hujui maana ya mitandao ya kijamii. Kama wengine hawajadili hiyo ajenda ya kuvunjwa kwa katiba, ww umeijadili wapi ili tuone ww ni tofauti na hao unaowalaumu?

Kwenye mitandao ya kijamii kunajadiliwa chochote kinachokuja, na kila mmoja kwa uelewa na hisia zake. Ukitaka ajenda fulani tu zijadiliwe, nenda kwenye platform rasmi za kufanya hayo. Lakini huku kwenye mitandao mijadala ni ya chochote ie, umbea, soka, uchawi, uesharati nk.
 
Naona unachanganya kuwa kiongozi na kuaminiwa. Anaweza kuwa kiongozi bila mimi kumuamini, maana hawi kiongozi kwa maamuzi yangu. Mimi binafsi simuamini, kama ww unamuamini hilo ni juu yako. Kwani hicho chama Kiko hao hadi leo kwa sababu ya hao uliowataja tu? Je wakifa achia kuondoka ndio chama nacho kitaifa? Kaondoka Slaa na Zito mbona hicho chama hakijafa?
 
Endapo kamati itasema tuhuma ni za uongo Lema ataendelea kujitetea nini tena.
Lema hakusema kuwa atajitetea ila alisema akilazimika atasema ili kulinda heshima yake. Wahuni wale wa G55 wanamchafua kuwa anataka Heche aondoke. Sasa Heche kaiba nini? Hizo hela za mafuta za tonetone au? Akili zingine banah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…