Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sudan kaskazini naona ni mara 100, achilia mbali kuiba huku hata mtu akusaidie kitu na umuachie tip ya dola 500 hapokei anakushukuru tu unaendelea na mambo yako
Ya mkuu Nigeria ni nchi ya kwanza yenye idadi kubwa ya watu, na asilimia kubwa ya raia wake hawana kazi. Kwahiyo ili mtu uweze kuishi na kujikimu kimaisha ni lazima ujiongeze kwa njia mbali mbali kama vile rushwa, utapeli, ufisadi nk.
 
Sudan kaskazini naona ni mara 100, achilia mbali kuiba huku hata mtu akusaidie kitu na umuachie tip ya dola 500 hapokei anakushukuru tu unaendelea na mambo yako
Kumbe Sudan nayo ni miongoni mwa nchi zenye raia waaminifu sana mkuu!!
 
Wazambia nadhani ni utamaduni wao... Hata habari kubagain kushushushiwa bei wakati wa manunuzi hawanaga sana.
Ni watu wa tofauti ukilinganishaa na sisi wabongo kilife
 
Mkuu Isanga family mbona hoja yako nimeshaijibu kitambo kwenye post namb #287. ikichek utaiona.
 
Wazambia nadhani ni utamaduni wao... Hata habari kubagain kushushushiwa bei wakati wa manunuzi hawanaga sana.
Ni watu wa tofauti ukilinganishaa na sisi wabongo kilife
Ya ni kweli mkuu, jamaa wako smart sana aisee.
 
So ni majambazi ya Tanzania ila yanajificha zambia...!! Aisee tz noma sanaa
Ya hao wako wengi. Tatizo mwana hakufafanua kama hao majambazi walikamatiwa Zambia au Tanzania. Ni ngumu kwa mimi kuamini tu moja kwa moja kama polisi wa Tanzania waliingia Zambia kuwakamata hao wahalifu. Ni kwa vile jamaa alisikia tu kwenye news akajua kuwa hao wahuni walifuatwa wakakamatwa na polisi wetu. Ila kwangu mimi naona hao wahalifu walikamatwa na polisi wa Zambia kwa kushirikiana na mamlaka ya Tanzania, kisha wakakabidhiwa kwa polisi wa Tanzania pale mpakani Tunduma. Polisi wa Tanzania nao wakafanya yao kama kawaid yao.
 
Duh ndo maana Kagame alifyata kwa Kikwete. Maana anaifahamu Tanzania vizuri zaidi ya watanzania wenyew wanaoshinda kweny vijiwe vya kahawa. Jeshi la Tanzania halijawahi kushindwa ktk oparation yoyote tangu kuumbwa kwa dunia hii.
 
Duh ndo maana Kagame alifyata kwa Kikwete. Maana anaifahamu Tanzania vizuri zaidi ya watanzania wenyew wanaoshinda kweny vijiwe vya kahawa. Jeshi la Tanzania halijawahi kushindwa ktk oparation yoyote tangu kuumbwa kwa dunia hii.
Jeshi letu halijawahi kushindwa katika oparation yoyote ya moja kwa moja.

Ni umahiri, umakini, ujuzi, uzoefu na jitihada za jeshi letu ndio zilizoweza kuleta ukombozi katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Kaburu, Comoro na kwengineko. So Kagame asingeweza kuthubutu kutuletea unyonge kama ule anaouleta kwa Congo na wakati mtoto wetu mwenyew hayati Ngulunziza wa Burundi alimshindwa.
 
Hata Tunduma pale Mkuu kwenye ishu ya kubadili fedha palikuwa na usalama wa kutosha mtu yupo na mamilioni kwenye kifungashio na hakuna mporaji ila ni miaka minne tangu nitoke pale sjui kwa ss hali ikoje
 
Hata Tunduma pale Mkuu kwenye ishu ya kubadili fedha palikuwa na usalama wa kutosha mtu yupo na mamilioni kwenye kifungashio na hakuna mporaji ila ni miaka minne tangu nitoke pale sjui kwa ss hali ikoje
Tatizo la Tunduma usalama upo katika maeneo yale ya kubadilishia hela tu, kwa sababu maeneo hayo yamezingirwa na askari polisi wengi pamoja na askari wa uhamiaji. Ila utapomaliza kubadili hela zako na kutembea mwendo wa dakika 10 tu kutoka eneo la mpakani, lazima ushikishwe adabu na vibaka uchwara.
 
Miaka ya nyuma watu wametekwa sana kwa njia hiyo yaani anapanda bus la Lusaka huku kabadili lundo la hela kaweka kwrnye begi Wezi walikua wanaongea na wana usalama wasio waaminifu upande wa mpika huko bus linasimamishwa unaambiwa wewe ushuke na begi lako una tatizo la Passport wale polisi na wale wahuni walikuja kukamatwa siku moja dereva wa bus alipogoma kushusha begi la abiria wakashushie kituo cha polisi au begi libaki waende na mtu wao maana palikua na dola za kutosha baadae walipostukiwa wengine wakakimbia ila walikuja kuksmatwa na kuishia jela na hizo mambo ndio ukawa mwisho wake...harafu ramani ilikua inasomwa uhamiaji wao wanamlazimisha msafiri aonyeshe hela ya safari wengine wanaonyesha nyingi ili agongewe kumbe unaingia kwenye mtego wa kuibiwa...
 
Duh kumbe miaka ya nyuma ilikuwa balaa, ila askari uhamiaji wengi wanatamaa. Nafikiri huwa wanakamilisha ule msemo wa kila mtu ale kwenye kazi yake, na wanakula kweli πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wale walifuta 000 zile ile hela haina thamani hata kuizidi Tsh ila kuelewa hapo kwa watu wengine mtakesha...
Mzee naelewa na najua maana ya 1 Kilometre is equal to 1000 metres Mzee. Kuna mtu aliyekimbia 1 km then akamcheka aliyekimbia 1000 metres akidai amekimbia umbali mfupi.
 
Naamini ipo siku ntatembelea nchi zetu jirani hizi aisee.

Ni majirani zetu ila daah tupo tofauti saana.

Mfan kipindi cha nyuma kidg mji wa tunduma ulikua unasifika kwa wizi, udokozi, ujambazi, magendo na uhalifu mwingine lakini cha ajabu ndo hapo karibu na hiyo Zambia isiyo na hizo sifa. Na wakazi wa hapo wengi shughuli zao hufanyia hiyo nchi jirani!!.

Ama kweli jasiri haachi asili, pamoja na kukaa na uaridi bado hatujanukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…