Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Mimi nimeishia hapo kwa mjomba Mbagala kibonde maji.

Tuweke mzani sawa, umetembea nchi ngapi kaka kiasi useme zambia ndio nchi yenye amani na usalama zaidi? (uliyoandika humo nimesadiki ila ningependa kujua nchi ulizotembelea ila niweze kufanya tathmini)
 
Nimekumbuka kitu kutokana na mchango huu!!

Ndugu zetu Waislam asilimia kubwa hujitahidi kuyaishi wanayofundishwa tofauti ki % na upande mwingine.(naomba nisishambuliwe ni mtazamo wangu)

Japo mi mkristo ila unachosema nu kweli

Jamii za kiislamu zina ustaarabu sana kwenye biashara na mambo ya wizi wizi sio mkubwa kuliko jamii za kikristo.

Huo ni ukweli kabisa
 
Ni kweli kabsa yan uko sheria zao kali na wanazifatilia sana ndio maana wananchi wao wanatii sheria bila shuruti!! Lakin waho wazambia braza wako na roho mbaya sana kuna visa wanatufanyia sana sisi wapita njia mi nimeishi hapo MPIKA
N hata sasa Kuna mgogoro Kati ya Tz vs Zambia khs Namna Zambia wanavyowa-treat waTz wanaondesha malorry.Bungeni Waziri akisema wanaangalia Namna ya kuweza kuikwepa Zambia wkt wa kupeleka mizigo Congo.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Katika zunguka zunguka yangu yote katika nchi mbali mbali nikianza na nyumbani Tanzania....
Kwa nnachoamini kila nchi ina kitu chakr ambacho imebalikiwa, wao yawezekan wamebarikiwa ilo lakin in other hand yawezekan huo ushuhuda wako hauna uhakika 100% kwasababu hujaweka wazi ni kwa muda gani umekaa uko kwajil ya utafiti huo na malengo ya utafiti wako yalikuwa ni yapi na je majibu uliyoyapata tunaweza kuyathibitisha vipi katika muktadha wa tafiti. Lakin kwa Tanzania niseme tu wazi hali ya usalama imeimarika sana kwa siku za hivi karibuni matukio kam uliyoyatolea mfano hapo kariakoo kuna baadhi ya maeneo matukio hayo hayapo kabisa.

Kwaiyo huwezi kutumia eneo mmoja kujustify kwamba Tanzania hakuna usalama ndugu yangu. Labda ungesema hali ya usalama nchini bado inakumbwa na changamoto ivyo mamlaka ziongeze nguvu ili kuhakikisha usalama unakuwepo kwa 100%.
 
Kingine kinacho fanya waheshimu hela ya mtu ni hofu ya kulogwa. Kama ujuavyo Zambia ni road kuu ya kupitisha mizigo na biashara kwenda KONGO.
Huko nyuma wakongo wengi walikuwa wanatapeliwa sana pesa na mizigo yao wakaamua kutoa fundisho kwa kuloga.
 
Na Kubadili fedha za kigeni enzi hizo mambo ya bureau Ni mizinguo tumebadilisha Sana kwa wasomali,Huku uaminifu ukiwa ni 100%

Tatizo la uswahili ni imani potovu kama ushirikina
Yaani wakiona mtu kaendelea watasema tapeli au kaenda kwa mganga ila hata siku moja huwezi kumsikia mswahili anasema kuwa jamaa kafika hapo kwa uaminifu wake

Bado tuna safari ndefu sana
 
Ugumu wa maisha na kutokuweko mzunguko wa fedha kwa wote ndicho hufanya kuweko na ongezeko la uharifu! Kama kila mtu añapata riziki zake hayuko wakusumbukia cha mwingine.Selikali za nchi zingine zimeweka mazingira rafiki ya sio binya mzunguko wa fedha kwa wananchi wa nvhi husika.
 
Kwa haraka haraka kuwa pale siku 5 niligundua hivi:, chakula anachukula mvuta Guta wa Zambia mwalimu wa Tanzania hawezi kukila mfulilizo kwa wiki nzima unless akubaliane kusave laki ama elfu 80 kwa mwezi.
2) wanawake wa Zambia uwatenganishi na vazi la kanga/kitenge.
Wanapenda sana kujifunga kanga na vitenge no matter kavaaje utamkuta kajifunga kitenge/kanga.
 
Tatizo la uswahili ni imani potovu kama ushirikina
Yaani wakiona mtu kaendelea watasema tapeli au kaenda kwa mganga ila hata siku moja huwezi kumsikia mswahili anasema kuwa jamaa kafika hapo kwa uaminifu wake

Bado tuna safari ndefu sana
Tukiambiwa uaminifu Ni mtaji hua tunaona Kama Ni story tu.Tunaamini hauwezi kutoboa kwny Maisha bila kuiba/kudhulumu.
 
Bongo majizi wengi
 
Tukiambiwa uaminifu Ni mtaji hua tunaona Kama Ni story tu.Tunaamini hauwezi kutoboa kwny Maisha bila kuiba/kudhulumu.

Hilo wengi hawalijui kwa sababu ya kukua kwenye mazingira magumu ya dhulma na uongo

Ukiwa muongo lazima utakuwa tapeli tu huwa vinaendana sana

Ila ukiwa muaminifu utaendelea haraka kwani utapata madili hata kama sio moja ya biashara zako

Unauza duka mtu anakuletea Dili la kumuuzia kiwanja kisa uaminifu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…