Kuna siku pale magomeni kanisani palikuwa na foleni. Kuna abiria mwenzetu aliagiza maji kwa wale wanaopitisha madirishani, kabla hajamkabidhi hela daladala likaondoka.
Yule abiria akamwomba dereva apunguze mwendo ili ampe yule muuzaji hela yake, licha ya kuwa dereva alichomoa kwamba pale sio kituo tena, lakini abiria wa karibu waligeuka wote kumwangalia yule ni abiria wa namna gani.
Kufika mapipa akashuka tukaona anarudi (tulihisi anaenda kumpatia hela muuzaji), mle kwenye basi ukawa mjadala kwamba inawezekana yule sio mtanzania maana sisi watz kwa tunavyojuana uaminifu ni sifuri kabisa asilimia kubwa.