Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Uko sahihi Somalia ndio kiboko

Mtu anaenda msikitini kaacha maburungutu ya hela wazi njiani anapobadilishia na haibi mtu

Nchi Haina amani vurugu tupu lakini uaminifu wa pesa uko juu mno kuliko Sisi watanzania tuliojaa amani
Watu wanazungumzia habari za democratic countries wewe unaleta habari za failed states? Hawazungumzii fedha na mali tuu, bali hata usalama wako
 
Aiseeee brother Hivi umekielewa ulichokiandika au umeamua tu kuandika acha hizo bwana.Mambo ya kishamba kabisa umeandika
Jamaa mshamba kinoma, afu anaonekana hajawahi kutoka nje ya kijiji chao.
 
Ni kweli kabsa yan uko sheria zao kali na wanazifatilia sana ndio maana wananchi wao wanatii sheria bila shuruti!! Lakin waho wazambia braza wako na roho mbaya sana kuna visa wanatufanyia sana sisi wapita njia mi nimeishi hapo MPIKA
Visa gani mkuu na vinafanywa na akina nani raia,polisi au jeshi la Zambia
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu,sisi wazee wa road trips ndani ya barabara za Zambia 🇿🇲 unaweka kambi popote na kama unawasiwasi zaidi unalala kwenye check points za police au jeshi!
Yani Zambia ni nchi tamu sana kiusalama na hata kimaisha vilevile. Watu hawapigiki kivile haswa wageni
 
Usalama unaanzia udogoni kwani watoto wanashuhudia wazazi na jamaa wanavyofanya biashara na kuaminiana nao wanakua na kuiga

Sisi ni tofauti kabisa mtoto anakuwa kwa kushuhudia utapeli au nyumbani mtu anagonga kuja kudai utasikia mtoto anaambiwa mwambie baba hayupo

Wizi ni janga la Taifa letu na hakuna wa kumuamini na utakaesema huyu kalia sana Acha nimkope ndio kabisa hiyo imekula kwako

Lingine ni kuwa kuna wengi wanatetea wizi yaani mfanyakazi au kiongozi serikalini au sekta binafsi anaiba na akibainika utasikia- Safi sana wacha waibe hata mimi nisingeacha

Hapo tegemea hakuna mwenye unafuu na wizi hautaisha hata serikalini


Hili la kuweka hela za kubadilisha hadharani zipo sehemu kadhaa hata kuna mji Somaliland panaitwa Hargeisa ipo kwenye YouTube
Yaani kina mama wanauza Dhahabu hadharani huku vijana wakibadilisha hela zikiwa juu ya meza kibao na hakuna wa kuiba
Tena anaenda kusali anafunika na shuka [emoji3064]
Utashangaa ya Zambia ila kuna wengine waaminifu pia
Kweli ndugu yang usalama na uaminifu huanzia kwenye ngazi ya familia, jamii na baadae nchi. Ikiwa familia haziaminiani, jamii haiaminiani na viongozi wa nchi hawaaminiani, basi tegemea kutengeneza taifa lenye wizi na unadhilifu mkubwa wa pesa.
 
Nimekumbuka kitu kutokana na mchango huu!!

Ndugu zetu Waislam asilimia kubwa hujitahidi kuyaishi wanayofundishwa tofauti ki % na upande mwingine.(naomba nisishambuliwe ni mtazamo wangu)
Wasomali wana weakness nyingi tu kama waislamu

Mfano Tanzania ni nchi isiyo na dini kabisa lakini mirungi ni haramu iko kwenye kundi la madawa ya kulevya ukikamatwa unalo

Somalia ni nchi ya kiislamu asilimia mia moja mirungi kwao sio haramu hutafuna kabla kuingia msikitini na wakitaka msikitini

Binafsi nawasifia tu eneo la uaminifu kwenye pesa huko kwingine Hawako vizuri
 
Ni kweli kabsa yan uko sheria zao kali na wanazifatilia sana ndio maana wananchi wao wanatii sheria bila shuruti!! Lakin waho wazambia braza wako na roho mbaya sana kuna visa wanatufanyia sana sisi wapita njia mi nimeishi hapo MPIKA
Inategemea mkuu. Kila jamii au nchi huwa haikosi watu wa roho mbaya na wa roho nzuri. Laiti kama wangekuwa na roho mbaya kwa namna unayofikiria, basi nchi ile isingekuwa na wageni wengi kama waliona sasa. Zambia kuna kila aina ya wageni kama vile watanzania, wanigeria, wazimbabwe, warundi, wakongo, wanyarwanda, wa south, wanamibia, wamalawi nk. Ila wote wanaishi kwa amani, wanafanya biashara zao na kazi zao bila mtu yeyote kuwagusa.
 
Back
Top Bottom