Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Zambia hii hii madereva wetu wanavyoibiwa coper na mafuta au zambia ya kwenye mitandao?

Hapo lusaka ni kama boda tuu na hizo pesa wanazobadikisha ata bida zetu karibia zote zipo hivyo labda kipindi cha awanu ya 5 ndio wakalazimisha iwe kubadili pesa ni benki pekee.

Ukitaka kujua udhaifu wa Zambia miliki lorry au tafuta wanaisafirisha mizigo huko.
 
Hujakosea kabisa kuhusu Zambia
Hata askari polisi wao si washenzi kama wa kwetu. Askari ni waadilifu, wanatumia akili.
Hali ya hewa pia ni nzuri. Ni nchi fulani naipenda sana, ukiongeza na Namibia, Seychelles, Botswana na Cape Verde.
Hivi ni hawa hawa askari wa kutoka Nakonde to kasumbalesa ndio mnaowasifia humu?
Nina clip nyigi tu za madereva wetu juu ya manyanyaso wanayoyapata huko zambia.

Kama unapita na basi hayo hauwezi kuyajua wala kuyaona.
 
Sijawahi kufika Chingola, ila Kitwe, Kapilimposhi, Lusaka na Ndola. Chingola kina kipi?
Chingola kumetulia,mji uko kama vimji vya waingereza bado...kamji hkana kokoro
Hata kitwe pia nimepapenda,nmekaa sana nkana East hapo na Riverside
Ukitokea chilalabombwe kama unaelekea chingola kuna sehemu inaitwa musenga ndani kule kuna mashamba ya wazungu na wanafuga pia,nilikaa pia....huko sasa ndy tuliwasanua wazambia biashara ya skrepa miaka hiyo
Vitabiatabia fulani wanavyo,sema kdg wazambia wana ustarabu,ila ni watu wa kuhoji mambo na kuwaburuza wagumu

Ova
 
Kuna siku pale magomeni kanisani palikuwa na foleni. Kuna abiria mwenzetu aliagiza maji kwa wale wanaopitisha madirishani, kabla hajamkabidhi hela daladala likaondoka.

Yule abiria akamwomba dereva apunguze mwendo ili ampe yule muuzaji hela yake, licha ya kuwa dereva alichomoa kwamba pale sio kituo tena, lakini abiria wa karibu waligeuka wote kumwangalia yule ni abiria wa namna gani.
Kufika mapipa akashuka tukaona anarudi (tulihisi anaenda kumpatia hela muuzaji), mle kwenye basi ukawa mjadala kwamba inawezekana yule sio mtanzania maana sisi watz kwa tunavyojuana uaminifu ni sifuri kabisa asilimia kubwa.
 
Kama baliega kule gomz pamoja na kujua tabia zake walikuwa wanamlea tu mpka pale alipouwawa wanajifanya wanalia wana huzuni
 
Hivi ni hawa hawa askari wa kutoka Nakonde to kasumbalesa ndio mnaowasifia humu?
Nina clip nyigi tu za madereva wetu juu ya manyanyaso wanayoyapata huko zambia.

Kama unapita na basi hayo hauwezi kuyajua wala kuyaona.
Kwa upande wa askari ni kweli wanaushz fulani,Rushwa wanayo
Jela zao lockup zenyewe siyooo

Ova
 
Huyo mvuta guta licha ya kula hicho chakula bado anafanya mambo mengine ya Maendeleo vizuri tu kushinda Mwalimu wa Kibongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…