Sijawahi kuona nchini yenye amani na usalama kama Zambia

Hiyo Nchi ina watu wachache sana kulinganisha na ukubwa wa Nchi yao na uwezo wa serikali yao kuwahudumia ni mkubwa so lazima wawe na kaunafuu la maisha kiasi fulani..

Shule zao za msingi ,walimu Wanamiliki magari kitambo sana wakati huku kwetu wameanza kujikongoja miaka hii ya Leo..

Zambia watu mil.16 ,Tzn mol.60
 
Nimeshatembea nchi zaidi ya 5, ila kati ya hizo nchi nimeona Zambia ndio nchi yenye amani na usalama zaidi kwa sababu
1) Zambia ndio nchi pekee ukiingia town iwe sokoni, kwenye mall au stand ya mabasi utakutana na watu wanaochenji pesa tena wengi wao ni wageni kutona Nigeria, Congo nk. Wachenji hela hawa utawakuta wamekaa mstari mfano wa wauza samaki pale feri. Kila mtu utakuta kaweka maburungutu ya usd (yani dola za kimarekani) mia mia, hamsini hamsini na ishirini ishiri.
Kifupi kwa hesabu ya haraka haraka kila meza moja au mfuko wa mchenji hela mmoja huwa haukosi dola elfu 3, elfu 5 na kuendelea. Sasa fikiria kama ukipiga vamizi la meza 10 utaondoka na dola elf ngapi? Na ukizichenj kwa hela ya Tanzania utapata bei gani. Pia watu wanauza vitu vyao nje nje tena vya thamani kubwa, ila hakuna anaelalamika kuvamiwa wala kuibiwa. Zambia nimeshakaa takriban miezi 3 na pia huwa napita nikirudi Tanzania kutokea South. So nina uhakika na ninachokisema.
Nafikiri umesoma na michango ya watu wengine humu na kushuhudia mwenyew jinsi watu waliofanikiwa kupita, au kuishi nchi ile wanavyokubaliana na kile nilichoandika.
 
Mkuu soma post namb #144 utapata majibu yako. Watanzania hatuwafikii hata robo ya uaminifu na usalama hawa jamaa. Labda tatizo lao, au ulemavu wao mkubwa ni pombe tu. Hawa jamaa wanakunywa pombe zaidi ya nchi zote zilizounda umoja wa nchi za East Africa.
 
Kingine kinacho fanya waheshimu hela ya mtu ni hofu ya kulogwa. Kama ujuavyo Zambia ni road kuu ya kupitisha mizigo na biashara kwenda KONGO.
Huko nyuma wakongo wengi walikuwa wanatapeliwa sana pesa na mizigo yao wakaamua kutoa fundisho kwa kuloga.
😂😂🤣🤣🤣
 
Watu mil 16 nchi nzima?
Kulikuwa na ulazima kutolea mfano walimu😂
 
Ya ulichosema kina ukweli mkubwa. Kingine hawa jamaa wanapiga sana mkojo wa mjusi, yani katika nchi zinazoongoza kwa ulevi barani Afrika Zambia haikosi kwenye tatu bora.
 
Dah ndugu unayoongea yana ukweli mtupu. Bila uaminifu lazima maisha yaje yakupige chenga, maana hata ukibahatika kupata matumizi yako yatakuwa ya hovyo hovyo kama akili yako. Ila ukiwa mwaminifu basi na maisha yatakuwa mazuri kwa kuridhika na kile kidogo au kikubwa unachokipata.
 
Hujakosea kabisa kuhusu Zambia
Hata askari polisi wao si washenzi kama wa kwetu. Askari ni waadilifu, wanatumia akili.
Hali ya hewa pia ni nzuri. Ni nchi fulani naipenda sana, ukiongeza na Namibia, Seychelles, Botswana na Cape Verde.
Ya hizo nchi ulizozitaja pia usalama ni mzuri ukilinganisha na nchi zetu za East Africa zilizojaa vibaka.
 
Mkuu mi nafikiri uaminifu wao hausianiani na idadi ya watu wala swala la kuhudumiwa na serikali. Kama ingekuwa kuhudumiwa na serikali ndio mwarobaini wa uaminifu basi Kaburu ingeongoza kwa hilo, maana wao wanapewa huduma za bure, lkn swala la uaminifu kwao ni zero.
 
Inamaana huko hakuna wezi kabisa au Sheria zao ni Kali kwanini kuwe na utulivu hivo na ikiwa watu ni wengi pia?
Wezi wanaweza kuwa wapo, lkn ni wachache mno ukilinganisha na wale ambao sio wezi. Yani ni kama
a) wezi 5%.
b) wasiokuwa wezi 95%.
Nafikiria na sheria zao zimechangia pia kuleta uaminifu ndan ya nchi hizi.
 
Sijaweka idadi ya watu kwamba ndio kigezo cha uaminifu bali kuonyesha kwamba wako wachache hivyo serikali ina nafasi kubwa ya kuwahudumia ikilinganishwa ndio matajiri wa kopa Dunia nzima hapo sijataja mali zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…