Sijui nilikurupuka au nilikosa mtu wa kuniongoza na sasa sijui nifanyeje?

  • Thread starter Thread starter guest-1788672427
  • Start date Start date
  • Tags Tags
    mtu
Ukipata wasiwasi tena nshutue nikupe 5.5 zako hapo karibu Na zahanati, offer hii natoa siku Tano kuanzia Leo, utakuja inbox utaniachia namba mi ntakutafuta,

Nikurudishie Na Mimi nikajute , Niko serious, ,,Ila vimepimwa!?
Vimepimwa vyote na ramani ya vipimo ninazo na vina bicon zenye namba

Kimoja kipo kanisa la kkkt galagza au wanapaita kwa mchungaji na kingine kipo kule karibu na zahanati ya galagaza karibu na kiwanda cha kuku cha wahindi

Ila kuuza nilihairisha ila ninq maumivu
 
Ahsante dear
Nilinunua kiwanja mwaka 2013/2014 hapo mjini Dar maeneo ya Goba kwa 7M. Hapakuwa na maji wala umeme, hapakuwa na lami njia kuu za Mbezi Beach -Mbezi Luis, Goba -Madale-Tegeta, Goba -Temboni, Goba-Kimara, Goba-Makongo-Mlimani City.
Zingine hapo ndiyo zilikuwa zina anza kujengwa.
Sasa lami njia zote hizo, maji na umeme vipo, vituo vya mafuta hadi napakana navyo.
World bank wanatuwekea barabara za zege hadi magetini kwetu.
Sasa hivi hupati kiwanja hapo hata kwa 40M.
 
Uli target eneo la kimkakati mkuu
Hongera sana
 
Ku Kukurupuka umekurupuka wewe? Mm ndo nimekurupuka kuhonga kiwanja cha familia kwa mdada wa jf kisa tu ana mkia. Kaniahid vitu kibao kaja kuniacha solemba Lamomy
 
Usiuze, utajuta baadaye
 
Kabla yakushika hiyo ela uliyonunulia kiwanja, je uliwahi kufikiria unataka kununua kiwanja wapi? Na je ulitimiza hiyo ndoto ya yakununua huko

Kama hukutimiza hiyo ndoto, hicho ndicho kinachokusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…