Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Wakati mwingine sheria za kijeshi zinahitaji reforms.....nchi nyingine kama ujerumani askari anahaki ya kutotii amri ya kamanda wake kama amejiridhisha kuwa amri hiyo ikitekelezwa itakiuka haki za kibinaadamu..
Kuna kipengele Cha kutii AMRI HALALI ndo hicho unakisema

Maana amri isiyo halali mwisho lazima italeta shida tu either kwa raia au hata mtu yule ambae sheria inatekekezwa kwake

Kwahiyo bado mulemule tu Kama hao ujerumani


Ukitekeleza amri ISIYO HALALI utawajika wewe mtekekezaji maana utetezi wa kwamba nilipewa amri hawezi kukutoa kwenye hatia
 
Wakati mwingine sheria za kijeshi zinahitaji reforms.....nchi nyingine kama ujerumani askari anahaki ya kutotii amri ya kamanda wake kama amejiridhisha kuwa amri hiyo ikitekelezwa itakiuka haki za kibinaadamu..
Hawataki yajirudie ya World War Two na Final Solution, kama hii sheria ingekuwepo before, holocaust isingetokea
 
Sio kila kitu kinakuwa juu ya Sabaya. Na kama uko interested na Sabaya nilishajieleza kwa muungwana mmoja hapo juu. Jitahidi kusoma.

Unajua Mkuu, tukiwa jeshini, tulikuwa tukiambiwa askari anapaswa kutii amri wakati wote, ili mradi iwe wazi ni amri halali.

Kwa hiyo Sabaya alijua wazi alikuwa anapewa amri isiyo halali, hivyo hakupaswa kutii. Lakini hata hivyo, inawezekana kabisa amri halali ya Magufuli ilikuwa ni Sabaya kwenda kuwakamata wale watu. Lakini unadhani aliambiwa utakapoenda kuwakamata uwapige na kuwaumiza? Hata hivyo bado kuna maswali kama, kwa nini Magufuli akamtumia Sabaya na sio vyombo halali vya usalama kama TISS na Polisi? Ni wazi basi Magufuli na Sabaya walijua wazi walikuwa wanafanya uhalifu.

Sasa Sabaya akijua alikuwa anatekeleza amri ya kihalifu, utetezi wake haupaswi kuwa alitumwa, kwa sababu anajua hupaswi kutii amri isiyo halali. Ukiwa mhasibu huwezi kujitetea niliiba fedha za kampuni kwa kuwa meneja wangu aliniambia niibe. Utetezezi wa Sabaya unapaswa kujikita kwamba alifanya vile kwa kuwa kwa alivyomjua Magufuli, asingetekeleza maisha yake yangekuwa hatarini.

Na labda Sabaya awe na ushahidi kwamba fulani aliamriwa kutekeleza jambo la kihalifu na Magufuli na alipokataa aliuwawa katika mazingira tatanishi. Na pia anaweza kuweka ushahidi ambao unamwonyesh kuwa Magufuli alikuwa anaua watu waliompinga. Hapo ndipo anaweza kujiokoa na hii kesi.
 
Luteni ndo cheo gani hicho? We utakua huna tofauti na mtu anayesema nna degree ya Bachelor.

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
Tanzania kuna watu wajinga lakini hamjui kama ni wajinga, kwa hiyo mnaishia kuwa wabishi na kuongea ujinga.

Sasa wewe unanikandia mimi eti Luteni ndio cheo gani, na unanipa mfano wa mtu kusema degree ya bachelor, sasa huo si wendawazimu? Acha kuropoka pale unapokuwa mjinga wa jambo, unajiabisha mbele za watu. Mie nimepitia jeshini ndio maana nikaweka hii thread. Wewe umewahi kwenda hata jeshi la mgambo? Watu kama wewe ndio mlimuudhi Mwakyembe akaishia kusema wewe darasa la saba unabishana na mimi wa digrii nne!

Kwa taarifa yako basi, kukusaidia kuondoa ujinga wako, Tanzania Luteni (Lieutenant) ni cheo jeshini cha mtu mwenye nyota mbili.

Na neno Luiteni linakuja kutumika tena kwa kanali, ambapo kuna Luteni Kanali kabla hujawa Kanali kamili.. Na pia kuna Luteni Generali kabla hujawa Generali kamili

Iko hivi;

Kuruta
Private
Koplo
Sajenti
Sameja
Sekandi Luteni
Luteni
Kepteni
Meja
Luteni Kanali
Kanali
Brigedia
Meja jenerali
Luteni jenerali
Jenerali
 
We jamaa huna akili na huko jeshini sijui ulienda kufanya nini? hivi mtu anaweza kukuuliza mwanao anasoma la ngapi ukamwambia yuko "form" ilihali kuna form one mpk six.
Sa huo mfano ndo sawa na ujinga wako.
Jeshini kuna
2nd lieutenant
1st lieutenant
Lieutenant colonel
Lieutenant general.
Sa we unaposema lieutenant unamaanisha cheo gani kati ya hivyo?
Afu unajiona mwanajeshi wakati hujui hata ranks.


Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Hivi akili yako ina nini?

Nimekuambia Lieutenant jeshini ni cheo cha nyota mbili, lakinini pia neno lieutenant linatumika kama prefix kwa kanali na jenerali.

Umewahi kuona mtu amevaa cheo chenye alama ya nyota mbili na ngao? Unamwitaje?

Na mtu mwenye nyota mbili, unamwitaje?

Usijifanye kujua wakati hujui
 
Naomba elimu kidogo tofauti ya KURUTA na PRIVATE

Tafadhali
 
We unachokiongea hukijui mtu mwenye nyota mbili ni first lieutenant na sio lieutenant kama unavyosema

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Naomba elimu kidogo tofauti ya KURUTA na PRIVATE

Tafadhali
Unapoingia jeshini bado una maji magotini hujui hata kupiga mguu upande, wewe ni kuruta. Kwa JKT hupewi hata kombati, unavaa bukta na vesti.

Unapokuwa umamaliza mafunzo yote ya msingi ya jeshi lakini wewe ni askari bila cheo chochote, wewe ni private. Ukiona polisi au mwanajeshi hana kitu chochote begani, huyo ni private
 
We unachokiongea hukijui mtu mwenye nyota mbili ni first lieutenant na sio lieutenant kama unavyosema

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
Ahaa, kwa hiyo Lieutentant sio cheo kwa kuwa kuna first na second?

Sasa huo sio utaratibu wa JWTZ. Sisi nyota mbili tunaita Luteni, kama unatuletea mambo ya USA nenda USA kaongelee puani tuondolee shombo za kina Trump hapa.
 
Ahaa, kwa hiyo Lieutentant sio cheo kwa kuwa kuna first na second?

Sasa huo sio utaratibu wa JWTZ. Sisi nyota mbili tunaita Luteni, kama unatuletea mambo ya USA nenda USA kaongelee puani tuondolee shombo za kina Trump hapa.
We jamaa ni mbishi we unaongelea kimazoea au ki uhalisia?


Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Anhaaa hapo sasa nimeeelewa
 
Nimekusoma in reference to Naneya aka Tisaya aka Panki one at Kisongo over!

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ya kwako imeandikwa na mmarekani, sisi tunaita luteni usu, sio luteni wa pili na wa kwanza
We uache ubishi we sema tu kwamba kimazoea luteni wa kwanza mnamuita "luteni" bas tutakuelewa ila ki rasmi anaitwa luteni wa kwanza na kiukweli jeshini hakuna cheo kinachoitwa luteni bila kufuatiwa na neno lingine.

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…