Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Mleta mada ni miongoni mwa mananga wanaozalishwa jeshini kwa kupiga zile kozi za mtoto wa binamu anafundishwa na mtoto wa nmmjomba. Kuna cheo kinaitwa askari luteni kweli katika jeshi lolote!!, huyu askari luteni bia yake inamwagwa na kuambiwa aende mahabusu baada ya kugoma bunduki anaelekezewa sajenti.
Acha kushabikia typos. Niliandika Sajenti nikaambiwa alikuwa Luteni. Katika kurekebisha ndio imetokea mchanganyiko kidogo
 
Kwanza hamna Silaha inayoitwa SMG
Bali SMG ni .kundi la silaha za aina fln za upigaji.
Yaan SMG uzi gun
SMG Ak47 nk sasa wewe ulikuwa unamaanisha nini ulivyosema SMG? Na mara luten mara sajent. Aliyehariri story yako hajahariri vzr
Hakuna silaha inaitwa SMG? Wewe serule kweli wewe.

Nachojua SMG ni silaha iliyotengenezwa China, inachukua magazini ya risasi 30. Ni silaha iliyoboreshwa kutoka SAR. Wamarekani waliiga wakajidai wao ndio waliitengeneza kwanza

AK 47 ni silaha iliyotengenezwa (ilikuwa designed) na askari wa Kirusi akiwa hospitali anatibiwa. Inachukua magazine ya risasi 40. Tofauti ya SMG na AK47 ni kwamba AK47 kule mbele imetahiriwa (inechongwa) wakati SMG ni ya mviringo. Pia AK47 ni silaha yenye kutumainika sana, haina tazito kupiga risasi hata ukizama nayo majini. Pia AK47 unapopiga risasi haikupindishi, wakati SMG inakuvuta kushoto, hasa ukiweka "burst". Ndio maana hata mtoto mdogo anaweza kukulenga kwa AK47 akakupata lakini sio SMG
 
Mie mwenye ndo nmetahamaki baada ya kusikia hivi na bado watu wanachangia kama vile story ipo sawa
Story ipo sawa na ya kweli. Makosa yalikuwa kusema Sajenti badala ya Luteni. KUna mtu amechangia alikuwapo Mgambo na kuthibitisha tukio.
 
Umeleta story ya kufikirika mara luteni kamwagiwa bia yake hapo hapo sajenti kagoma kunyanyuka kaelekezezewa SMG.ebu acha kutuletea chai mkuu
Mkuu hiii sio chai, ni tukio lilitokea. Ila nilikosea, hakuwa sajenti alikuwa Luteni. Na kuna mtu anakumbuka na kasema alikuwa jamaa Luteni bongebonge hivi Msukuma, na amesema kabisa ilikuwa mwaka wa Operasheni Nidhamu
 
Ila mtoa Mada kwa kupika story sjui umetuona wote mazuzu ujinga mtupu useless story kawadanganye wajukuu zako
Acha kuwa Thomaso. Nakiri kukosea kusema Sajenti badala ya Luteni. Na kuna jamaa amekuja kunikumbusha kwamba jamaa alikuwa Luteni mmoja Msukuma. Sasa kama wewe siku zote ni mbishi wa kuamini hilo ni shauri yako. Sio kila mtu humu JF anapika stori kama wewe. Kama kuna mazuzu basi ni wewe ambae unadhani kila stori ya JF ni ya kupika
 
Luteni na sajenti ni vyeo viwili tofauti, nani mhusika kutaka kuuwawa? All in all, CO hakuwa na sababu ya kuamrisha mauaji. Alitakiwa kuagiza mp commander amchukue aliegoma kutii anti, apelekwe mahabusu kesho yake mahakama ya kijeshi. Ilikuwa uamuzi wa kilevi na ungemgharimu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Luteni ndo cheo gani hicho? We utakua huna tofauti na mtu anayesema nna degree ya Bachelor.

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada ni miongoni mwa mananga wanaozalishwa jeshini kwa kupiga zile kozi za mtoto wa binamu anafundishwa na mtoto wa nmmjomba. Kuna cheo kinaitwa askari luteni kweli katika jeshi lolote!!, huyu askari luteni bia yake inamwagwa na kuambiwa aende mahabusu baada ya kugoma bunduki anaelekezewa sajenti.
kwaiyo unataka kusema jeshini hakuna cheo cha luteni?

askari wa cheo chochote anaweza kumnyooshea bunduki askari wa cheo chochote inategemea hyo amri anapewa na nani mda huo
 
Hii stori nzima imelenga kutolea ufafanuzi dhidi ya alichokifanya Sabaya na utetezi wake aliotoa!! [emoji2377][emoji2377][emoji2377]
 
kwaiyo unataka kusema jeshini hakuna cheo cha luteni?

askari wa cheo chochote anaweza kumnyooshea bunduki askari wa cheo chochote inategemea hyo amri anapewa na nani mda huo
Cheo hicho kipo lakini hakuna "luteni askari" mkuu.
 
Hakuna silaha inaitwa SMG? Wewe serule kweli wewe.

Nachojua SMG ni silaha iliyotengenezwa China, inachukua magazini ya risasi 30. Ni silaha iliyoboreshwa kutoka SAR. Wamarekani waliiga wakajidai wao ndio waliitengeneza kwanza

AK 47 ni silaha iliyotengenezwa na askari wa Kirusi akiwa hispotali anatibiwa. Inachukua magazine ya risasi 40. Tofauti ya SMG na AK47 ni kwamba AK47 kule mbele imetahiriwa (inechongwa) wakati SMG ni ya mviringo. Pia AK47 ni silaha yenye kutumainika sana, haina tazito kupiga risasi hata ukizama nayo majini. Pia AK47 unapopiga risasi haikupindishi, wakati SMG inakuvuta kushoto, hasa ukiweka "burst". Ndio maana hata mtoto mdogo anaweza kukulenga kwa AK47 akakupata lakini sio SMG
Kuna mengi huyajui katika hii fani. Ukweli ndio huo hakuna silaha inaitwa SMG ila hilo ni kundi la silaha lenye sifa fulani fulani, lakini kwakuwa ulikaririshwa ni ngumu kukubadilisha mkuu.
 
kwaiyo unataka kusema jeshini hakuna cheo cha luteni?

askari wa cheo chochote anaweza kumnyooshea bunduki askari wa cheo chochote inategemea hyo amri anapewa na nani mda huo
Cheo cha luteni kipo lakini hakuna cheo cha askari luteni boss.
 
Nimeshindwa kuelewa kosa la sargent kutaka kupigwa risasi wakati luten ndio mwenye kosa.
Na kingine nimeshindwa kuelewa imekuwaje mesi ya ma afisa inakuwa sehemu moja na askari wa vyeo vya chini.
Kingine sijui au sijawahi ona askari akiwa mesi na silaha tangu niko jeshini labda huu ni utaratibu wa kikosi chenu hapo mgambo tanga kwenye shamba la gendaheka lenye kontua 400 kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa kuna mengi hayajui katika hii fani mkuu.
 
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
Kama nia yako ni Kuzungumzia Suala zima la Ole Sabaya na Utetezi wake wa Kutumwa katika Oparesheni za Kikatili na Kiuhalifu na Hayati Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais ( sasa ) Dkt. Mpango na BOT Governor Wala hukuwa na haja ya Kufumba na Kuzunguka sana hivi.
 
Back
Top Bottom