Siku hizi hatutongozi tena wanawake… tunawapa tu “idea” tu!

Siku hizi hatutongozi tena wanawake… tunawapa tu “idea” tu!

Kuna jambo nimekuwa nikiliangalia sana kwenye mahusiano ya siku hizi. Dunia imebadilika, na hata namna ya kuanzisha mahusiano imebadilika.

Zamani kulikuwa na kitu kinaitwa kutongoza. Mwanaume alikuwa anakaa chini, anatafuta maneno mazuri, anahangaika kweli kweli mpaka mwanamke aelewe kuwa anavutiwa naye. Ilikuwa ni mchakato kabisa.

Lakini siku hizi ukweli ni kwamba watu wengi hawatongozi tena, wanachofanya ni kutoa idea tu.

Yaani unaweka mazingira au unapendekeza kitu, halafu kama mtu yupo interested ataelewa tu.

Mfano mdogo:

Badala ya kusema:
“Naomba uwe girlfriend wangu”

Siku hizi mtu anasema tu:
“Unaonaje weekend hii uje home tupike kitu pamoja tucheki movie?”

Hapo hakuna mahali kasema anakutongoza, lakini idea tayari ipo mezani.

Mfano mwingine:
Badala ya kusema:
“Nakupenda sana, nataka tuwe wote”

Mtu atasema tu:
“Leo nilikuwa napita sehemu fulani nikakumbuka ungekuwa hapa tungekula kitu pamoja.”

Idea tayari imetolewa.

Mfano mwingine wa kawaida sana siku hizi:

“Unaonaje tukutane coffee kesho jioni tuongee kidogo?”

Au
“Weekend hii nina plan ya kuangalia movie mpya, ungependa kujoin?”

Hapo mtu hatongozi moja kwa moja, anatoa tu opportunity. Kama mtu ana interest ataingia kwenye hiyo idea.

Hata kwenye chatting hali ni hiyo hiyo.

Zamani ilikuwa:

“Naomba namba yako, nakupenda.”

Siku hizi ni rahisi sana:
“Tuendelee na hii story WhatsApp itakuwa rahisi.”

Ukikubali kutoa namba, story inaendelea yenyewe.

Mfano mwingine:
Badala ya kusema wazi “nataka tuwe karibu”, mtu anasema:

“Unaonaje siku moja nije nikutembelee hapo kwako?”

Au

“Unaonaje siku moja nikupikie?”

Au

“Unaonaje tukasafiri hata day trip tu tukapumzike?”

Hizi zote ni ideas.

Ukweli ni kwamba hii style imekuwa common sana kwa sababu watu wengi siku hizi hawataki kukataliwa moja kwa moja. Kwa hiyo wanaweka idea mezani.

Kama mtu ana interest ataishika.

Kama hana interest, ataiacha tu ipite kimya kimya bila drama.

Na mara nyingi mwanamke akipenda hiyo idea, hata yeye anaweza kuendeleza conversation kama vile:

“Weekend hii naweza nikaja, lakini nitakuja mchana.”

Au
“Hiyo movie tunaweza kuiangalia wapi?”

Hapo tayari mchezo umeanza.

Kwa kifupi:

Siku hizi mahusiano mengi yanaanza kwa ideas, sio kwa kutongoza rasmi kama zamani.

Mtu anaweka tu mazingira, halafu chemistry ikikubali mambo yanajiendeleza yenyewe.

Swali la kujiuliza ni hili:
Hii style mpya ya kutoa idea badala ya kutongoza moja kwa moja ni bora zaidi, au imeondoa ile ladha ya mahusiano ya zamani?

Me siku hizi natengeneza idea , demu akiipenda basi mchezo unakua umeisha hivyo
Duh! Acha Akitoka mama achukue Nchi Abdul....bado muda wa ukombozi haujafika.
 
Je, inawezekana kuwa wanaume wamekua madomo zege na hawajui tena kutongoza au ndiyo ukisasa?
Kizamani ndiyo ilikua poa, unatumiwa mpaka barua za kuimbishwa kwa maneno matamu!
Tumeamua ku-adopt new effective method, yaani nguvu kidogo matokeo makubwa.

Tumeachana na mambo ya msuli tembo matokeo sisimizi.

Hata wao wameikubali, ukiwa mchana mistari wanakuona wakuja tu 😊
 
Sasa mshangazi ushapitia pirika nyingi mpk midudu imechana kipochi manyoya unaanza kumtongoza “Ooh nakupenda nataka nikuoe.” Huoni kama unajichoresha unataka kumdanganya?? 😹😹😹

Wewe nenda direct kwenye point ya msingi upewe mzigo. Kama hujaeleweka basi jaribu kwingine..!!
Watu tuko nje ya muda sasa hivi 😹😹
Hahaha so wote bna wamechanwa kipochi manyoya....
Ndo maana nawapendaga coz wanakuwaga waelewa kwenye yake mambo yetu
 
Zamani ndio ilikua nzuri, mtu anakufukuzia muda mrefu na yupo serious sio hawa wa sasa akiomba namba ukiringa kidogo tu ndio imeisha hiyo.
Huyu ni mimi mtupu mtu anakuoa namba vizuri unampa utaratibu anaringa ringa unasema okay nikikausha nakuja kuambiwa mimi tena ndio naringa na hapo ndio inakuwa imeishaa hiyo.

Wanawake bilion 3 duniani kwanini uteseke.
 
Katika kitu huwa najilaumu mpk kesho.... nimewah muandikia mtoto wa mtu barua mbili, majibu kimya🥺
Nikaenda dukani kwao kujua tunafanyaje kuhusu hisia zangu,,, zile barua zikachanwa mbele yangu halafu nikarushiwa😂😂

Kama movie ya kihindi, ila zamani hapana kwakweli🏃
Uweeh ilikuwa raha!! Ukimuadmire mtu unamuandika kwenye diary inabaki siri yako mpaka unamaliza shule, sikuhizi dem likimtaka mtu mpaka linampata within a few days 😆

Kumchania mtu barua kuna raha yakee😌 hapo mpaka kamati yake ije ikubembelezee ndio ukubali sasa na kuliwa sio leo🤗
 
Nadhani sababu kubwa wanawake wa sasa wengi ni warahisi hivyo mwanaume anaona ya nini kujitesa ukiringa wewe leo kesho atapata mtu mwingine, na pia wanaume wengi wametanguliza tamaa mbele wenye kumaanisha na upendo wa kweli ni wachache ndio sababu hawaoni maana yoyote kumbembeleza mtu ikiwa lengo ni kupita tu, mwenye nia ya dhati atavuta vuta muda.
Uko sahihi kabisa, ni mwendo wa kuviaziana sikuhizi kila mtu anamuona mwenzake tapeli hakuna cha kuaminiana wala nini😆
 
Wa kuclear mzigo bandarini kwa zama hizi...mmmh! Watu wanaitaka waichape wakupe ya kuogea na kufulia hiyo bikini 👙😅😅
Wapo inategemea na circle yako bana..!!

Bora kiliwe na nyenyere sigawi kipapa changu otherwise nipende mwenyewe na ni kitu ambacho nadra kutokea..!! 😹😹
 
Noma sana...
Now npo mabush huku napambana na kilimo sasa juzi nimeenda sheri na trekta nikaweke dizeli,after kuweka yule muhudumu akawa ananidai 400,nikampa hela kubwa akasema hana chenchi...nikamwambia nikuingizie kwenye simu akakubali ila akadai kama ni kumrushia sharti iwe 10000...
Nikampa hyo 10k cash halafu nkamwambia ntakupigia badae uje tunywe wine....sikumpigia na sina wazo la kupiga kwakua nipo swaumu ila kila akienda dogo anamwambia kaka ako mbona hapigi simu
 
Noma sana...
Now npo mabush huku napambana na kilimo sasa juzi nimeenda sheri na trekta nikaweke dizeli,after kuweka yule muhudumu akawa ananidai 400,nikampa hela kubwa akasema hana chenchi...nikamwambia nikuingizie kwenye simu akakubali ila akadai kama ni kumrushia sharti iwe 10000...
Nikampa hyo 10k cash halafu nkamwambia ntakupigia badae uje tunywe wine....sikumpigia na sina wazo la kupiga kwakua nipo swaumu ila kila akienda dogo anamwambia kaka ako mbona hapigi simu
Mtoto anasubir hiyo idea ya kunywa wine, hapo mcheki tarehe 19 usiku ,then sikukuu ya eid unakamilisha mchongo
 
Zamani ndio ilikua nzuri, mtu anakufukuzia muda mrefu na yupo serious sio hawa wa sasa akiomba namba ukiringa kidogo tu ndio imeisha hiyo.

Mambo yamerahisishwa sana kupitia utandawazi. Siku hizi hata domo zege anakupa idea, ukijaa tu kwenye mfumo...imoooo
 
Back
Top Bottom