Siku hizi hatutongozi tena wanawake… tunawapa tu “idea” tu!

Duh! Acha Akitoka mama achukue Nchi Abdul....bado muda wa ukombozi haujafika.
 
Je, inawezekana kuwa wanaume wamekua madomo zege na hawajui tena kutongoza au ndiyo ukisasa?
Kizamani ndiyo ilikua poa, unatumiwa mpaka barua za kuimbishwa kwa maneno matamu!
Tumeamua ku-adopt new effective method, yaani nguvu kidogo matokeo makubwa.

Tumeachana na mambo ya msuli tembo matokeo sisimizi.

Hata wao wameikubali, ukiwa mchana mistari wanakuona wakuja tu 😊
 
Hahaha so wote bna wamechanwa kipochi manyoya....
Ndo maana nawapendaga coz wanakuwaga waelewa kwenye yake mambo yetu
 
Zamani ndio ilikua nzuri, mtu anakufukuzia muda mrefu na yupo serious sio hawa wa sasa akiomba namba ukiringa kidogo tu ndio imeisha hiyo.
Huyu ni mimi mtupu mtu anakuoa namba vizuri unampa utaratibu anaringa ringa unasema okay nikikausha nakuja kuambiwa mimi tena ndio naringa na hapo ndio inakuwa imeishaa hiyo.

Wanawake bilion 3 duniani kwanini uteseke.
 
Uweeh ilikuwa raha!! Ukimuadmire mtu unamuandika kwenye diary inabaki siri yako mpaka unamaliza shule, sikuhizi dem likimtaka mtu mpaka linampata within a few days 😆

Kumchania mtu barua kuna raha yakee😌 hapo mpaka kamati yake ije ikubembelezee ndio ukubali sasa na kuliwa sio leo🤗
 
Uko sahihi kabisa, ni mwendo wa kuviaziana sikuhizi kila mtu anamuona mwenzake tapeli hakuna cha kuaminiana wala nini😆
 
Wa kuclear mzigo bandarini kwa zama hizi...mmmh! Watu wanaitaka waichape wakupe ya kuogea na kufulia hiyo bikini 👙😅😅
Wapo inategemea na circle yako bana..!!

Bora kiliwe na nyenyere sigawi kipapa changu otherwise nipende mwenyewe na ni kitu ambacho nadra kutokea..!! 😹😹
 
Noma sana...
Now npo mabush huku napambana na kilimo sasa juzi nimeenda sheri na trekta nikaweke dizeli,after kuweka yule muhudumu akawa ananidai 400,nikampa hela kubwa akasema hana chenchi...nikamwambia nikuingizie kwenye simu akakubali ila akadai kama ni kumrushia sharti iwe 10000...
Nikampa hyo 10k cash halafu nkamwambia ntakupigia badae uje tunywe wine....sikumpigia na sina wazo la kupiga kwakua nipo swaumu ila kila akienda dogo anamwambia kaka ako mbona hapigi simu
 
Mtoto anasubir hiyo idea ya kunywa wine, hapo mcheki tarehe 19 usiku ,then sikukuu ya eid unakamilisha mchongo
 
Zamani ndio ilikua nzuri, mtu anakufukuzia muda mrefu na yupo serious sio hawa wa sasa akiomba namba ukiringa kidogo tu ndio imeisha hiyo.

Mambo yamerahisishwa sana kupitia utandawazi. Siku hizi hata domo zege anakupa idea, ukijaa tu kwenye mfumo...imoooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…