haszu
JF-Expert Member
- Oct 10, 2017
- 978
- 2,313
Ilikuwa kipindi Ferouz ndio ametoa wimbo wake wa starehe, mama alikuwa anaumwa ila nyumbani tulikuwa tunaambiwa anaumwa TB. Sasa siku jioni tumekaa mi nikaimba kipande cha wimbo wa Ferouz " starehe mnazipenda ila mwisho wake ni mbaya, wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya...."
Kwa kweli sikuwa nafahamu lolote ukizingatia nilikuwa mdogo, kumbe usiku tulipoenda kulala, mama akamuita bibi akamuuliza, "kwani huyu Haszu ni mdogo sana hajui mimi naumwa nini?" Asubuhi mapema sana bibi akaniambia nimsindikize shamba, tukaenda kufika akanijuza uhalisia.
Nililia, sema ndo hivyo haikuwa na jinsi. Kwa wale wakongwe wanafahamu miaka hiyo hali ilikuwa ni hatari sana.
My she rest in eternal peace.