Siku niliyojua mama yangu anaumwa UKIMWI mwaka 2005

Siku niliyojua mama yangu anaumwa UKIMWI mwaka 2005

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
978
Reaction score
2,313
Ilikuwa kipindi Ferouz ndio ametoa wimbo wake wa starehe, mama alikuwa anaumwa ila nyumbani tulikuwa tunaambiwa anaumwa TB. Sasa siku jioni tumekaa mi nikaimba kipande cha wimbo wa Ferouz " starehe mnazipenda ila mwisho wake ni mbaya, wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya...."

Kwa kweli sikuwa nafahamu lolote ukizingatia nilikuwa mdogo, kumbe usiku tulipoenda kulala, mama akamuita bibi akamuuliza, "kwani huyu Haszu ni mdogo sana hajui mimi naumwa nini?" Asubuhi mapema sana bibi akaniambia nimsindikize shamba, tukaenda kufika akanijuza uhalisia.

Nililia, sema ndo hivyo haikuwa na jinsi. Kwa wale wakongwe wanafahamu miaka hiyo hali ilikuwa ni hatari sana.

My she rest in eternal peace.
 
Hatari sana hilo, lakini pia kila kwenye maneno 20 tunayoyaongea basi mawili yapo yanayomgusa jirani yako.
Pole sana ndugu.
 
Pole sana. Huu ugonjwa miaka ya nyuma uliua sana kama covid ilivyoua kipindi cha kwanza.
 
Siku hizi hakuna tena ukimwi! Watu wanakunywa dawa, na huwezi hata kuwadhania kama wanaugua huo ugonjwa.
 
Ina huzunisha sana.

Ila sio wote wanaopata Ukimwi, kwasababu ya sex ( ngono zembe ) au malaya. Tusihukumu waathirika, tuwapende tuwajari tuwatie moyo. Ingawa sasa hivi hofu ya ukimwi haipo watu wanatiana kama mbwa
"Watu wanatiana kama mbwa"[emoji848]
 
Back
Top Bottom