Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #21
Duh mkuu kumbe na ww umekula chumvi kiasi chake.Nlikuwa formone kibasila
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh mkuu kumbe na ww umekula chumvi kiasi chake.Nlikuwa formone kibasila
Ndivyo msafara wa Nyerere ulivyokuwa hata akiwa madarakani. Hakuwa na msafara mkubwa barabarani naona alijiamini mashushu aliowasambaza nchi nzima wanafanya kazi nzuri.
Hahahaha.. mkuu unamaanisha fimbo yake ilikuwa na mataa mawili, yani kijani na nyekundu? Afu hivi ile fimbo yake iliendaga wapi au alizikwa nayo?Hakuamini walinzi aliamini fimbo yake ilikuwa inampa warning ishara fulani ikiwa kijani nenda kiwa nyekundu usiendee .
Sio kuzaliwa. Alikua amesha jitambua vizuri kabisaWewe ulimwona Nyerere gani wakati uliliona gari lake?
Halafu 1995 ulikuwa umeshazaliwa tayari? Duh!
Ile fimbo pamoja na baadhi ya vitu vyake muhimu vipo makumbusho Butiama. Ukipata nafasi fanya ukatalii Butiama utaviona.Hahahaha.. mkuu unamaanisha fimbo yake ilikuwa na mataa mawili, yani kijani na nyekundu? Afu hivi ile fimbo yake iliendaga wapi au alizikwa nayo?
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze katika mada husika.
Nakumbuka siku 1 mimi na mjomba wangu tulikuwa tunatoka feri kula samaki, tukijielekeza mnazi mmoja kupanda basi turudi nyumbani. Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 1995, kabla ya uchaguzi mkuu.
Basi bwana wakati tunatoka feri kufika maeneo ya post mpya, tukaona magari yamesimama foleni kuashiria kuwa kuna kiongozi mkuu anatarajia kupita muda huo. Kwa vile kulikuwa na watu wengi wakishangaa shangaa ili waone ni kiongozi gani atakaepita, ikabidi na sisi tujiunge na ule msururu wa watu kuangalia kinachojiri. Wengi walihisi ni raisi Mwinyi alikuwa anatoka ikulu kuelekea sehemu tusioijua.
Lahaula, ghafla tukaona pikipiki moja zile zinazotumika kushindikiza viongozi ikichomoza, huku ikiwa imeambatana na benzi moja ambalo lilionekana ni la kawaida sana, kwani raia wengi tu walikuwa wanamiliki mabenzi tena ya maana kuliko lile, na nyuma ya benzi kulikuwa na land rover inayofanana muundo na hiyo picha niliyoambatanisha na uzi wangu hapo chini (watu wakawa wanapepea mikono) kuashiria kufurahishwa na yule aliekuwa anapita.
Sasa baada ya ule msafara wa pikipiki, benzi na land rover kupita, ndiyo magari mengine yakaruhusiwa yaendelee na shughuli zao. Ikabidi mimi nikamuuliza mjomba wangu, vipi mbona magari yanaruhusiwa na wakati kiongozi mwenyewe hajapita, mjomba akaniangalia kisha akaniuliza, kwanini wewe haukuuona ule msafara wa piki piki na magari mawili yakifuatana, nikamwambia niliona, akanijibu sasa ule msafara si ndo ulikuwa na kiongozi mwenyewe, nikamuuliza huyo kiongozi mwenyewe sasa alikuwa nani?
Mjomba akacheka kidogo kisha akanambia kwani wewe haumjui baba wa taifa mwl Nyerere, nikasema namjua vizuri sura yake kupitia tv, magazeti na vitabu mbali mbali, kisha mjomba akasema basi ndio yeye yule aliepita akiwa ndani ya benzi, alikaa siti ya nyuma, amevaa suti ya kijivu na juu alikuwa na kofia ya balaghashia. Dah kwa kweli alivyonambia vile sikuamini macho yangu. Nikamuuliza tena mjomba unauhakika kuwa yule ni baba wa taifa kweli, akasema bila shaka ni yeye kijana, kwani ulitegemea kumuona Nyerere bonge ya mtu au? Nikamwambia hapana simaanishi hivyo, ila kwa heshima aliyonayo katika nchi yetu, sikutarajia kumuona akiwa na msafara wa kichovu namna ile.
Mjomba akasema Nyerere ni mzalendo wa kweli, ndio maana maisha yake yote amekuwa akiishi ya kizalendo. Pia akanambia kwamba nchi yetu toka uhuru ilikuwa na wazalendo watatu tu, ila kati yao wawili washafariki amebaki yeye Nyerere. Nikamuuliza unasema toka uhuru nchi yetu ilikuwa na wazalendo watatu tu na Nyerere akiwa mmoja wapo, sasa hao wengine ni kina nani mbona mimi au sisi hatuwajui. Mjomba akasema wazalendo waliokuwa na Nyerere na sasa wametangulia mbele ya haki ni aliekuwa raisi wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi marehemu mzee Abeid Amani Karume, na mwingine ni aliekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Hapo nikawa nimeelewa, basi tukafika mnazi mmoja tukakuta watu wamejazana karibu na stand wakiangalia mchezo wa karata tatu, na sisi tena maongezi yakahama na kujikuta tumeingia katika maongezi mengine nje na yale na Nyerere. Ila ki ukweli siku ile nilisikitika sana kumuona baba wa taifa kubwa kama Tanzania anazunguka mjini na msafara wa gari mbili tu na piki piki moja. Huyu ndio baba wa Taifa na mzalendo wa kweli kabisa toka moyoni hayati Julius Kambarage Nyerere. Kama kuna mungine ashawahi kukutana mwamba huyu katika mazingira ya kawaida kama yale niliyomuona nayo mimi, aje atusimulie kidogo ili tujifunze uzalendo wa kweli kupitia kwake.
Asanteni sana.
View attachment 2297012View attachment 2297041
Mhenga kabisa mimiDuh mkuu kumbe na ww umekula chumvi kiasi chake.
Alipofariki tu ilizima nahaikufanya kazi tenaHahahaha.. mkuu unamaanisha fimbo yake ilikuwa na mataa mawili, yani kijani na nyekundu? Afu hivi ile fimbo yake iliendaga wapi au alizikwa nayo?
Imehifadhiwa kwenye jumba la makumbusho Butiama.Hahahaha.. mkuu unamaanisha fimbo yake ilikuwa na mataa mawili, yani kijani na nyekundu? Afu hivi ile fimbo yake iliendaga wapi au alizikwa nayo?
Ok mkuu, panapo majaaliwa siku 1 nitaenda kufanya utalii wa ndani katika kaburi la mzee wetu.Ile fimbo pamoja na baadhi ya vitu vyake muhimu vipo makumbusho Butiama. Ukipata nafasi fanya ukatalii Butiama utaviona.
Ikiwa njano ajiandae kuondoka 😀😀😀Hakuamini walinzi aliamini fimbo yake ilikuwa inampa warning ishara fulani ikiwa kijani nenda kiwa nyekundu usiendee .
Fimbo alikuwa nazo nyingi tofautitofautiIle fimbo pamoja na baadhi ya vitu vyake muhimu vipo makumbusho Butiama. Ukipata nafasi fanya ukatalii Butiama utaviona.
Tuwe wazalendo na viongozi wapunguze ukubwa wa misafara yao.Hadthi hii inatufundisha nini?
Duh kweli ile fimbo ilikuwa ya miujiza. Nasikia aliendaga kuzingua Kigoma wazee wa kazi wakamsahawisha fimbo yake makusudi, basi ile yupo ndan ya ndege akakumbuka kuwa kasahau fimbo Kigoma, alipotaka kurudi wakati wa mawasiliano wazee wakamwambia watampelekea fimbo yake Dar. Nyerere akacheka akiamini hakuna mtu anaeweza kuibeba ile fimbo isipokuwa yeye mwenyew, ila wazee wakasisitiza kuwa atatumiwa tu fimbo yake asiwe na hofu. Basi ile Nyerere anafika kwake ikulu ya Dar kuingia ndani anaikuta juu ya meza. Alitaka kutoka nduki sema walinzi wakamwambia mzee usikimbie acha sisi tutawasiliana na wale wazee kwa hatua zaidi. Baadae wazee wakamtoa uoga mambo yakawa shwari.Alipofariki tu ilizima nahaikufanya kazi tena