Siku niliyomuona Nyerere live nilisikitika sana

Uzalendo wa nyooko.

Ni vile huyo aliishi zama za ujima ambapo wahuni wengi hawakuwa wamejanjaruka kupata technolojia nzuri ya kupambana na serikali.

Leo hii jidai mzalendo, anza kuwapambania masikini kwa kuzuia rushwa, kuzuia madawa ya kulevya, kuzuia na kupambana na ushoga, kuzuia uhalifu&ujambazi, kuzuia uwizi wa resources za nchi, then chukua escort ya kitoto mtaani uzulule kama hawajakutungua within the minutes,(referred tukio la japan).

Mnautafsiri uzalendo kwa sababu za kitoto sana,yaan mnataka kiongozi wa nchi aishi maishi ya chini na kimasikini kama ninyi ili mujuwe kweli anawapenda? WaTz kweli upumbavu hauishi, elimu mliyoletewa iwakomboe kutoka kwa ujinga imekuwa kazi bure?

Kiongoz yeyote ambaye ni mkuu wa nchi ni lazima aishi maisha mazuri bila kusahau ulinzi mkubwa utakao muepusha na ubaya wa wahuni, mkuu wa nchi si sawa na balozi wa nyumba 10 kwamba apendwe na kila mtu, huyo huwa na maadui wengi sana, ni vile watu ambao hamjabahatika kuujua uongozi ama kuugusa utajiri ni ngumu kuelewa hili jambo.

We are not the same, acha kila mtu aishi kulingana na level yake, kamwe tusiforce kufanana.

Na huu ndio ukweli mchungu
Aiseee...
Hapana alikuwa mzalendo wa kweli. Kwa msafara na kwa matendo.
Ukiwa hujaiba cha watu hofu ya kuuliwa inapungua.
Ukiwa mtumishi wa kweli wa Mungu huwezi kuwa na mabidigadi lukuki.
 
Kwahiyo hukumwona uliona gari tu na watu wakipepea mikono Sasa unasemaje siku uliyomwona live??? Sisi tuliokula nae meza Moja na kushinda nyumbani kwake au kucheza nae BAO tusemeje??
 
Hiki kichwa kina madini sana na visa mikasa mbalimbali
Tatizo wengine hatuna kipaji cha kuandika tungeandika watu mnge burudika na kuelimika [emoji1]

Ova
Ahh sasa hivyo ndio tunahitaji mkuu na vitabu vya bongo kama bongo hakuna vya kuhifadhi matukio ya zamani, wati wote wanafariki na madini yao

Na kuna jamaa kashajitolea hapo kukuandikia, fanya jambo 😁😁😁,
 
Yapo mengi tu mkuu.

Lakini nikuulize swali. Hii mada imeanza anzaje hadi ikaingia kichwani mwako?

Swala la uzalendo na kuwapenda na kuwatakia mema waTanzania na nchi yao, hakika Mwalimu Nyerere ni mfano usiokuwa na mashaka juu yake.
Wapo waTanzania wengi, zaidi ya hao uliowataja hapo ambao ni/walikuwa wazalendo wa nchi hii.

Kwa bahati mbaya sana hatuna utaratibu wa utambuzi wa watu hawa na kuwapa heshima stahiki. Ninaelewa kulikuwepo na tuzo mbalimbali zilizowahi kutolewa kwa watu wenye sifa za kulitumikia taifa na kuonyesha uzalendo wao. Sielewi utaratibu huo ulikomea wapi, maana siku hizi hakuna anayejikujishughulisha na jambo hili.
Mkuu Kalamu nimeamua kuandika mada hii, baada ya kuona siku hizi kuna vijana wengi mtaani na serikalini wanajiita wazalendo wa nchi hii. Lakini ukiangalia style ya maisha yao ni tofauti na uzalendo wao. Wengi wanaishi maisha ya anasa kimya kimya, kujitukuza kiaina, kujilimbikizia mali nk. Sasa naiona tofauti kubwa kati ya hawa wanaojiita wazalendo wa leo na ule muonekano wa maisha aliyokuwa anaishi baba wa taifa. Yani siku ile kwa kweli nilishangaa sana kumuona baba wa taifa akiwa katika mazingira ya msafara wa kawaida tu, kitu ambacho wengine wanaojiita wazalendo hawakiwezi.
 
Hiyo picha kamili iko wapi??
Picha kamili namaanisha nikatumia kumbu kumbu ya kichwa changu kuvuta taaswira ya sura na muonekano wa Nyerere ili kujiridhisha. Sio kwamb ni picha ya kupiga.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze katika mada husika.
Nakumbuka siku 1 mimi na mjomba wangu tulikuwa tunatoka feri kula samaki, tukijielekeza mnazi mmoja kupanda basi turudi nyumbani. Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 1995, kabla ya uchaguzi mkuu.

Basi bwana wakati tunatoka feri kufika maeneo ya post mpya, tukaona magari yamesimama foleni kuashiria kuwa kuna kiongozi mkuu anatarajia kupita muda huo. Kwa vile kulikuwa na watu wengi wakishangaa shangaa ili waone ni kiongozi gani atakaepita, ikabidi na sisi tujiunge na ule msururu wa watu kuangalia kinachojiri. Wengi walihisi ni raisi Mwinyi alikuwa anatoka ikulu kuelekea sehemu tusioijua.

Lahaula, ghafla tukaona pikipiki moja zile zinazotumika kushindikiza viongozi ikichomoza, huku ikiwa imeambatana na benzi moja ambalo lilionekana ni la kawaida sana, kwani raia wengi tu walikuwa wanamiliki mabenzi tena ya maana kuliko lile, na nyuma ya benzi kulikuwa na land rover inayofanana muundo na hiyo picha niliyoambatanisha na uzi wangu hapo chini (watu wakawa wanapepea mikono) kuashiria kufurahishwa na yule aliekuwa anapita.

Sasa baada ya ule msafara wa pikipiki, benzi na land rover kupita, ndiyo magari mengine yakaruhusiwa yaendelee na shughuli zao. Ikabidi mimi nikamuuliza mjomba wangu, vipi mbona magari yanaruhusiwa na wakati kiongozi mwenyewe hajapita, mjomba akaniangalia kisha akaniuliza, kwanini wewe haukuuona ule msafara wa piki piki na magari mawili yakifuatana, nikamwambia niliona, akanijibu sasa ule msafara si ndo ulikuwa na kiongozi mwenyewe, nikamuuliza huyo kiongozi mwenyewe sasa alikuwa nani?

Mjomba akacheka kidogo kisha akanambia kwani wewe haumjui baba wa taifa mwl Nyerere, nikasema namjua vizuri sura yake kupitia tv, magazeti na vitabu mbali mbali, kisha mjomba akasema basi ndio yeye yule aliepita akiwa ndani ya benzi, alikaa siti ya nyuma, amevaa suti ya kijivu na juu alikuwa na kofia ya balaghashia. Dah kwa kweli alivyonambia vile sikuamini macho yangu. Nikamuuliza tena mjomba unauhakika kuwa yule ni baba wa taifa kweli, akasema bila shaka ni yeye kijana, kwani ulitegemea kumuona Nyerere bonge ya mtu au? Nikamwambia hapana simaanishi hivyo, ila kwa heshima aliyonayo katika nchi yetu, sikutarajia kumuona akiwa na msafara wa kichovu namna ile.

Mjomba akasema Nyerere ni mzalendo wa kweli, ndio maana maisha yake yote amekuwa akiishi ya kizalendo. Pia akanambia kwamba nchi yetu toka uhuru ilikuwa na wazalendo watatu tu, ila kati yao wawili washafariki amebaki yeye Nyerere. Nikamuuliza unasema toka uhuru nchi yetu ilikuwa na wazalendo watatu tu na Nyerere akiwa mmoja wapo, sasa hao wengine ni kina nani mbona mimi au sisi hatuwajui. Mjomba akasema wazalendo waliokuwa na Nyerere na sasa wametangulia mbele ya haki ni aliekuwa raisi wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi marehemu mzee Abeid Amani Karume, na mwingine ni aliekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Hapo nikawa nimeelewa, basi tukafika mnazi mmoja tukakuta watu wamejazana karibu na stand wakiangalia mchezo wa karata tatu, na sisi tena maongezi yakahama na kujikuta tumeingia katika maongezi mengine nje na yale na Nyerere. Ila ki ukweli siku ile nilisikitika sana kumuona baba wa taifa kubwa kama Tanzania anazunguka mjini na msafara wa gari mbili tu na piki piki moja. Huyu ndio baba wa Taifa na mzalendo wa kweli kabisa toka moyoni hayati Julius Kambarage Nyerere. Kama kuna mungine ashawahi kukutana mwamba huyu katika mazingira ya kawaida kama yale niliyomuona nayo mimi, aje atusimulie kidogo ili tujifunze uzalendo wa kweli kupitia kwake.

Asanteni sana.

View attachment 2297012View attachment 2297041
Umenifanya nitokwe machozi. Sasa hivi wanajengeana majumba, utadhani watazikwa nayo badala ya kuisaidia masikini.

Huko mitaani wanyonge wanahangaishwa, Tena utakuta na ka mwenyekit kakipewa rushwa
 
Mkuu Kalamu nimeamua kuandika mada hii, baada ya kuona siku hizi kuna vijana wengi mtaani na serikalini wanajiita wazalendo wa nchi hii. Lakini ukiangalia style ya maisha yao ni tofauti na uzalendo wao. Wengi wanaishi maisha ya anasa kimya kimya, kujitukuza kiaina, kujilimbikizia mali nk. Sasa naiona tofauti kubwa kati ya hawa wanaojiita wazalendo wa leo na ule muonekano wa maisha aliyokuwa anaishi baba wa taifa. Yani siku ile kwa kweli nilishangaa sana kumuona baba wa taifa akiwa katika mazingira ya msafara wa kawaida tu, kitu ambacho wengine wanaojiita wazalendo hawakiwezi.
Mkuu kalamu angewataja hao wazalendo wengine. Labda mama SSH.
 
Ndivyo msafara wa Nyerere ulivyokuwa hata akiwa madarakani. Hakuwa na msafara mkubwa barabarani naona alijiamini mashushu aliowasambaza nchi nzima wanafanya kazi nzuri.

Tiss ya wakati huo walikuwa wanavaa kila mtu alivyoamka..
Mwingine shati la kitenge, Mwingine Batik ....i

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ahh sasa hivyo ndio tunahitaji mkuu na vitabu vya bongo kama bongo hakuna vya kuhifadhi matukio ya zamani, wati wote wanafariki na madini yao

Na kuna jamaa kashajitolea hapo kukuandikia, fanya jambo [emoji16][emoji16][emoji16],
Yah ni kweli kwa tanzania tunashindwa ku document
Mambo,waandishi wetu wako
To low kwa sasa kwenye kuandika
Mambo ya kihistoria ili vizaz,watoto wanaokuwa wajue sahv watoto wanawajua tu wakina mondi harmonise singeli udaku basi

Mfano tu,pale dodoma,mlowa nlikuwa najuana sana na mzee mmoja anaitwa mathayo myombo,jamaa 1983 alikutana na mugabe pale mlowa kwenye ufunguzi wa chama cha ushirika,yeye alimpokea pale mugabe alilala pale mlowa
Picha zake Alikuwa nazo na kuna baadhi alinipa madini sana picha hizo
Rais mwinyi naye alitimba hapo akanpokea tena kuna picha mwinyi anatimba na gari suzuki samurai
Escort pajeros 1988 hyo
Sasa ukiangalia historia ya mzee myombo,yeye alikuwaga mwizi tu wa mifugo asili yake kutoka bahi ila alikuwa na karma ya hali juu sayansi ya kilimo,wakati rais marekani Jimmy Carter jamaa aliendaga marekani uke mchakato wa kusupply mahindi ya njano kutoka marekani mzee Ali play part kubwa sana kwenye kuyagawa huko kwa watu
Badaye mzee hyo alipelekwa Hungary, Poland kuongeza maujuzi
Mimi nlipokuwa naye kwenye kilaji tulikuwa ananiambia mambo mengi
Sema huyu mzee alikuja kufariki
Na alizikwa dodoma mlowa

Ova
 
Siajabu kwa Marais wastaafu kuwa na gari mbili kwenye msafara
Ata JK msafara wake ni pikipiki Moja na v8 mbili. Tena kunasiku kijiweni tukawaa tunaambiana yani jk kutoka kusindikizwa na magari hamsini hadi magari 2 tu iastaajabisha

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Yah ni kweli kwa tanzania tunashindwa ku document
Mambo,waandishi wetu wako
To low kwa sasa kwenye kuandika
Mambo ya kihistoria ili vizaz,watoto wanaokuwa wajue sahv watoto wanawajua tu wakina mondi harmonise singeli udaku basi

Mfano tu,pale dodoma,mlowa nlikuwa najuana sana na mzee mmoja anaitwa mathayo myombo,jamaa 1983 alikutana na mugabe pale mlowa kwenye ufunguzi wa chama cha ushirika,yeye alimpokea pale mugabe alilala pale mlowa
Picha zake Alikuwa nazo na kuna baadhi alinipa madini sana picha hizo
Rais mwinyi naye alitimba hapo akanpokea tena kuna picha mwinyi anatimba na gari suzuki samurai
Escort pajeros 1988 hyo
Sasa ukiangalia historia ya mzee myombo,yeye alikuwaga mwizi tu wa mifugo asili yake kutoka bahi ila alikuwa na karma ya hali juu sayansi ya kilimo,wakati rais marekani Jimmy Carter jamaa aliendaga marekani uke mchakato wa kusupply mahindi ya njano kutoka marekani mzee Ali play part kubwa sana kwenye kuyagawa huko kwa watu
Badaye mzee hyo alipelekwa Hungary, Poland kuongeza maujuzi
Mimi nlipokuwa naye kwenye kilaji tulikuwa ananiambia mambo mengi
Sema huyu mzee alikuja kufariki
Na alizikwa dodoma mlowa

Ova
Na amefariki akiwa hajulikani daahhh

Yaani waandishi wa bongo wapo busy na udaku Tu, unaweza kushangaa kila mtu yupo busy na mahusiano ya wasanii kuliko hustles na struggles zao

Huko kwingine kwenye Tv zilizopo serious, utaona wanasiasa daily wakati kuna watu wengi Tu wana stories nzuri..

Kuna kipindi nilikuwa nafanya issue ya kutafuta data na stories za watu wa chini kiasi.. Nilikutana na stories hadi unajiuliza, huyu si alitakiwa kupata tuzo ya malkia wa nguvu ila ndio hivyo, hawaonekani na hawapewi platform kuliko wauza nguo sinza za mastar

Fanya kitu mkuu, hata ulichosimuliwa chote tunaweza kuokota okota na sisi kwenye kitabu chako😁😁
 
Na amefariki akiwa hajulikani daahhh

Yaani waandishi wa bongo wapo busy na udaku Tu, unaweza kushangaa kila mtu yupo busy na mahusiano ya wasanii kuliko hustles na struggles zao

Huko kwingine kwenye Tv zilizopo serious, utaona wanasiasa daily wakati kuna watu wengi Tu wana stories nzuri..

Kuna kipindi nilikuwa nafanya issue ya kutafuta data na stories za watu wa chini kiasi.. Nilikutana na stories hadi unajiuliza, huyu si alitakiwa kupata tuzo ya malkia wa nguvu ila ndio hivyo, hawaonekani na hawapewi platform kuliko wauza nguo sinza za mastar

Fanya kitu mkuu, hata ulichosimuliwa chote tunaweza kuokota okota na sisi kwenye kitabu chako[emoji16][emoji16]
Hahaha ngj tuone

Ova
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze katika mada husika.
Nakumbuka siku 1 mimi na mjomba wangu tulikuwa tunatoka feri kula samaki, tukijielekeza mnazi mmoja kupanda basi turudi nyumbani. Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 1995, kabla ya uchaguzi mkuu.

Basi bwana wakati tunatoka feri kufika maeneo ya post mpya, tukaona magari yamesimama foleni kuashiria kuwa kuna kiongozi mkuu anatarajia kupita muda huo. Kwa vile kulikuwa na watu wengi wakishangaa shangaa ili waone ni kiongozi gani atakaepita, ikabidi na sisi tujiunge na ule msururu wa watu kuangalia kinachojiri. Wengi walihisi ni raisi Mwinyi alikuwa anatoka ikulu kuelekea sehemu tusioijua.

Lahaula, ghafla tukaona pikipiki moja zile zinazotumika kushindikiza viongozi ikichomoza, huku ikiwa imeambatana na benzi moja ambalo lilionekana ni la kawaida sana, kwani raia wengi tu walikuwa wanamiliki mabenzi tena ya maana kuliko lile, na nyuma ya benzi kulikuwa na land rover inayofanana muundo na hiyo picha niliyoambatanisha na uzi wangu hapo chini (watu wakawa wanapepea mikono) kuashiria kufurahishwa na yule aliekuwa anapita.

Sasa baada ya ule msafara wa pikipiki, benzi na land rover kupita, ndiyo magari mengine yakaruhusiwa yaendelee na shughuli zao. Ikabidi mimi nikamuuliza mjomba wangu, vipi mbona magari yanaruhusiwa na wakati kiongozi mwenyewe hajapita, mjomba akaniangalia kisha akaniuliza, kwanini wewe haukuuona ule msafara wa piki piki na magari mawili yakifuatana, nikamwambia niliona, akanijibu sasa ule msafara si ndo ulikuwa na kiongozi mwenyewe, nikamuuliza huyo kiongozi mwenyewe sasa alikuwa nani?

Mjomba akacheka kidogo kisha akanambia kwani wewe haumjui baba wa taifa mwl Nyerere, nikasema namjua vizuri sura yake kupitia tv, magazeti na vitabu mbali mbali, kisha mjomba akasema basi ndio yeye yule aliepita akiwa ndani ya benzi, alikaa siti ya nyuma, amevaa suti ya kijivu na juu alikuwa na kofia ya balaghashia. Dah kwa kweli alivyonambia vile sikuamini macho yangu. Nikamuuliza tena mjomba unauhakika kuwa yule ni baba wa taifa kweli, akasema bila shaka ni yeye kijana, kwani ulitegemea kumuona Nyerere bonge ya mtu au? Nikamwambia hapana simaanishi hivyo, ila kwa heshima aliyonayo katika nchi yetu, sikutarajia kumuona akiwa na msafara wa kichovu namna ile.

Mjomba akasema Nyerere ni mzalendo wa kweli, ndio maana maisha yake yote amekuwa akiishi ya kizalendo. Pia akanambia kwamba nchi yetu toka uhuru ilikuwa na wazalendo watatu tu, ila kati yao wawili washafariki amebaki yeye Nyerere. Nikamuuliza unasema toka uhuru nchi yetu ilikuwa na wazalendo watatu tu na Nyerere akiwa mmoja wapo, sasa hao wengine ni kina nani mbona mimi au sisi hatuwajui. Mjomba akasema wazalendo waliokuwa na Nyerere na sasa wametangulia mbele ya haki ni aliekuwa raisi wa kwanza wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi marehemu mzee Abeid Amani Karume, na mwingine ni aliekuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Hapo nikawa nimeelewa, basi tukafika mnazi mmoja tukakuta watu wamejazana karibu na stand wakiangalia mchezo wa karata tatu, na sisi tena maongezi yakahama na kujikuta tumeingia katika maongezi mengine nje na yale na Nyerere. Ila ki ukweli siku ile nilisikitika sana kumuona baba wa taifa kubwa kama Tanzania anazunguka mjini na msafara wa gari mbili tu na piki piki moja. Huyu ndio baba wa Taifa na mzalendo wa kweli kabisa toka moyoni hayati Julius Kambarage Nyerere. Kama kuna mungine ashawahi kukutana mwamba huyu katika mazingira ya kawaida kama yale niliyomuona nayo mimi, aje atusimulie kidogo ili tujifunze uzalendo wa kweli kupitia kwake.

Asanteni sana.

View attachment 2297012View attachment 2297041
Sisi tulishamwona akiwa anapalizi mahindi Butiama, ungekuwepo nadhani ungezimia.
 
Kusimamisha watumiaji wa Barbara wengine wote kumpisha ,protocol tayali ilizingatiwa.

Baada yake, wapo waliyo nyanganywa ulinzi lakini maisha yaliendelea.
 
Umenifanya nitokwe machozi. Sasa hivi wanajengeana majumba, utadhani watazikwa nayo badala ya kuisaidia masikini.

Huko mitaani wanyonge wanahangaishwa, Tena utakuta na ka mwenyekit kakipewa rushwa
Kwa sasa wazalendo hamna nchi hii, kila mtu anapigania tumbo lake na familia yake.
 
Mkuu kalamu angewataja hao wazalendo wengine. Labda mama SSH.
Mama SSM namkubali sana. Ila tungesubiri amalize muda wake, ndo tutoe hukumu kama ni miongoni mwa wazalendo au hapana.
 
Back
Top Bottom