Siku niliyomuona Nyerere live nilisikitika sana

Aiseee...
Hapana alikuwa mzalendo wa kweli. Kwa msafara na kwa matendo.
Ukiwa hujaiba cha watu hofu ya kuuliwa inapungua.
Ukiwa mtumishi wa kweli wa Mungu huwezi kuwa na mabidigadi lukuki.
 
Kwahiyo hukumwona uliona gari tu na watu wakipepea mikono Sasa unasemaje siku uliyomwona live??? Sisi tuliokula nae meza Moja na kushinda nyumbani kwake au kucheza nae BAO tusemeje??
 
Hiki kichwa kina madini sana na visa mikasa mbalimbali
Tatizo wengine hatuna kipaji cha kuandika tungeandika watu mnge burudika na kuelimika [emoji1]

Ova
Ahh sasa hivyo ndio tunahitaji mkuu na vitabu vya bongo kama bongo hakuna vya kuhifadhi matukio ya zamani, wati wote wanafariki na madini yao

Na kuna jamaa kashajitolea hapo kukuandikia, fanya jambo 😁😁😁,
 
Mkuu Kalamu nimeamua kuandika mada hii, baada ya kuona siku hizi kuna vijana wengi mtaani na serikalini wanajiita wazalendo wa nchi hii. Lakini ukiangalia style ya maisha yao ni tofauti na uzalendo wao. Wengi wanaishi maisha ya anasa kimya kimya, kujitukuza kiaina, kujilimbikizia mali nk. Sasa naiona tofauti kubwa kati ya hawa wanaojiita wazalendo wa leo na ule muonekano wa maisha aliyokuwa anaishi baba wa taifa. Yani siku ile kwa kweli nilishangaa sana kumuona baba wa taifa akiwa katika mazingira ya msafara wa kawaida tu, kitu ambacho wengine wanaojiita wazalendo hawakiwezi.
 
Hiyo picha kamili iko wapi??
Picha kamili namaanisha nikatumia kumbu kumbu ya kichwa changu kuvuta taaswira ya sura na muonekano wa Nyerere ili kujiridhisha. Sio kwamb ni picha ya kupiga.
 
Umenifanya nitokwe machozi. Sasa hivi wanajengeana majumba, utadhani watazikwa nayo badala ya kuisaidia masikini.

Huko mitaani wanyonge wanahangaishwa, Tena utakuta na ka mwenyekit kakipewa rushwa
 
Mkuu kalamu angewataja hao wazalendo wengine. Labda mama SSH.
 
Ndivyo msafara wa Nyerere ulivyokuwa hata akiwa madarakani. Hakuwa na msafara mkubwa barabarani naona alijiamini mashushu aliowasambaza nchi nzima wanafanya kazi nzuri.

Tiss ya wakati huo walikuwa wanavaa kila mtu alivyoamka..
Mwingine shati la kitenge, Mwingine Batik ....i

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mwalimu Nyerere alikuwa anajiamini nini mpaka ulinzi wake ukawa wa kawaiiiiida
 
Ahh sasa hivyo ndio tunahitaji mkuu na vitabu vya bongo kama bongo hakuna vya kuhifadhi matukio ya zamani, wati wote wanafariki na madini yao

Na kuna jamaa kashajitolea hapo kukuandikia, fanya jambo [emoji16][emoji16][emoji16],
Yah ni kweli kwa tanzania tunashindwa ku document
Mambo,waandishi wetu wako
To low kwa sasa kwenye kuandika
Mambo ya kihistoria ili vizaz,watoto wanaokuwa wajue sahv watoto wanawajua tu wakina mondi harmonise singeli udaku basi

Mfano tu,pale dodoma,mlowa nlikuwa najuana sana na mzee mmoja anaitwa mathayo myombo,jamaa 1983 alikutana na mugabe pale mlowa kwenye ufunguzi wa chama cha ushirika,yeye alimpokea pale mugabe alilala pale mlowa
Picha zake Alikuwa nazo na kuna baadhi alinipa madini sana picha hizo
Rais mwinyi naye alitimba hapo akanpokea tena kuna picha mwinyi anatimba na gari suzuki samurai
Escort pajeros 1988 hyo
Sasa ukiangalia historia ya mzee myombo,yeye alikuwaga mwizi tu wa mifugo asili yake kutoka bahi ila alikuwa na karma ya hali juu sayansi ya kilimo,wakati rais marekani Jimmy Carter jamaa aliendaga marekani uke mchakato wa kusupply mahindi ya njano kutoka marekani mzee Ali play part kubwa sana kwenye kuyagawa huko kwa watu
Badaye mzee hyo alipelekwa Hungary, Poland kuongeza maujuzi
Mimi nlipokuwa naye kwenye kilaji tulikuwa ananiambia mambo mengi
Sema huyu mzee alikuja kufariki
Na alizikwa dodoma mlowa

Ova
 
Siajabu kwa Marais wastaafu kuwa na gari mbili kwenye msafara
Ata JK msafara wake ni pikipiki Moja na v8 mbili. Tena kunasiku kijiweni tukawaa tunaambiana yani jk kutoka kusindikizwa na magari hamsini hadi magari 2 tu iastaajabisha

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Na amefariki akiwa hajulikani daahhh

Yaani waandishi wa bongo wapo busy na udaku Tu, unaweza kushangaa kila mtu yupo busy na mahusiano ya wasanii kuliko hustles na struggles zao

Huko kwingine kwenye Tv zilizopo serious, utaona wanasiasa daily wakati kuna watu wengi Tu wana stories nzuri..

Kuna kipindi nilikuwa nafanya issue ya kutafuta data na stories za watu wa chini kiasi.. Nilikutana na stories hadi unajiuliza, huyu si alitakiwa kupata tuzo ya malkia wa nguvu ila ndio hivyo, hawaonekani na hawapewi platform kuliko wauza nguo sinza za mastar

Fanya kitu mkuu, hata ulichosimuliwa chote tunaweza kuokota okota na sisi kwenye kitabu chako😁😁
 
Hahaha ngj tuone

Ova
 
Sisi tulishamwona akiwa anapalizi mahindi Butiama, ungekuwepo nadhani ungezimia.
 
Kusimamisha watumiaji wa Barbara wengine wote kumpisha ,protocol tayali ilizingatiwa.

Baada yake, wapo waliyo nyanganywa ulinzi lakini maisha yaliendelea.
 
Umenifanya nitokwe machozi. Sasa hivi wanajengeana majumba, utadhani watazikwa nayo badala ya kuisaidia masikini.

Huko mitaani wanyonge wanahangaishwa, Tena utakuta na ka mwenyekit kakipewa rushwa
Kwa sasa wazalendo hamna nchi hii, kila mtu anapigania tumbo lake na familia yake.
 
Mkuu kalamu angewataja hao wazalendo wengine. Labda mama SSH.
Mama SSM namkubali sana. Ila tungesubiri amalize muda wake, ndo tutoe hukumu kama ni miongoni mwa wazalendo au hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…