Wanaume kama ilivyo Kwa wanawake, hatupendi stress za rejareja. Hatupendi makelele ( hapa namaanisha mjifunze kyfikisha malalamuko, mapendekekezo au kukosoa Kwa staha). Mwanaume anaeweza kutulia na mtu yeyote anaempa utulivu, hata kama Hana kingine Cha ziada, ili tu anaonyesha kumheshimu na kumkosoa Kwa staha.
Pia kutuelewa kwamba tunavurugwa na mambo mengi kama ilivyo kwenu pia. Inahitaji kumwelewa mtu wako wakati Gani umwambie jambo Gani akakusikiliza.
Ya mwisho, hauwezi kumchunga binadam. Onyesha kumwamini na yeye ajue unamwamini hata kama unaona viashiria na chembechembe za ugaidi ( kuchepuka). Tulizana ukikusanya ushahudi wako huku ukitumia diplomasia kuigiza uko sawa. Kutufuatilia sana na wasiwasi uliopitiliza hua inafanya mpoteze point kirahisi sana. Kuna wakati jambo halihusiani kabisa na mambo ya mahusiano mtu anataka akufuatilie Kila kitu na kuongea Kwa kujiamini huku akiwa Hana uhakika. Kwa ufupi wanaume hatupendi kelele.
Niwatakie maadhimisho mema Mama zetu, Dada zetu, Binti zetu, malkia wake zetu, na wanawake wote Kwa ujumla.