Siku yako ya kwanza kuendesha gari ilikuwaje?

Utakuwa na shida kwenye psychomotor domain
 
2012...Nilivunja saitimila ya kushoto wakati naitopa parking,mzee aligomba sana si unajua gari za kiinua mgongo...

baada ya week alikuja fundi kuirekebisha hapo nikafundishwa kuendesha rasmi..
Duh watoto wa matajiri mnatia hasara
 
Ukitaka kujua gari uwe nayo karibu, uzoefu ni kila kitu
 
Msaada wa haraka nikitaka ku overtake nafanyaje wazee dah haya maisha magumu washikaj wote wako bise kila nae mtafuta anisaidie najuta kilanga komo
 
Hongera , ila anza kuendesha nje ya High way mdogo mdogo , na kama umewez kuendesha hadi posta tayar upo VZR

Jipe mazeoz nje ya high way mdogo mdogo utaweza , umakin unatakiw zaid kwakuw chombo sio yako.
 
Siku ya kwanza kuingia barabarani pekeyangu, niligonga mataa, baada ya kutoka hapo kwa hofu na kutetemeka mita kama 30 nikagonga bodaboda na abiria, na huyo bodaboda akampamia bodaboda mwingine, aiseee nilisikitika sana ila wote walinisamehe. Nikaizira gari kama siku nne. Baada ya hapo ikawa muda wa kutoka kazini naanza kua na mawazo na kukosa raha, siku nyingine nasahau badala ya kukanyaga break nakanyaga mafuta. Baada ya wiki tatu nikawa nimezoea 🤣 🤣 🤣
 
Sitaki kukumbuka mimi round about zilinichanganya nikaelekea kusiko[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyie ndio mnaomaliza watu wewe hujui kutumia chombo cha moto halafu unakitumia bila kuwa na mazowea ni hatari sana kwako na watumiaji wa bara bara.
Ushauri wangu kajifunze kwanza ukishakua umeshaelewa kutumia chombo cha moto ndio uingie bara barani tena kwa uangalifu sana mpaka utakapo kuwa driver mwenye uzoefu
 
Nilinunua gari kabla sijajua kuendesha. Anko ndio alikuwa dalali akaendesha toka Dar mpaka nilipo Kuelekea home akaniambia anko nisaidie kumalizia safari 🤣🤣🤣
Naikimbuka sana 2013
Ukaendeshaje sasa
 
Nilikuwa najua kipindi iko sikuwai endesha tena
 
Ile gari ya mzee baada ya kuninyima Sana siku Ile akanambia nitafute dereva akanifundishe nikamchukua mshikaji wangu flani wa kitaa ni dereva kwa wakati huo alikuwa ana gari,tukaenda home mzee akajiridhisha akampa gari,tumetoka vizuri home mpaka kiwanja Cha mpira
Mshikaji alinifundisha nikawa nishamulewa idea ya gari kichawi ilikuwepo tatizo kweny kukanyaga moto nilikuwa bado.

Baada muda tukaenda barabar flani hivi jamaa anaendesha huku anaelekeza hapa inabidi ufanye hivi maelekezo njia nzima...

Akaniachia Sasa Mimi na uwoga nikasema sijui Kama sijagonga mtu leo nimeendesha Kuna sehemu ikabidi nigeuze ili turudi nilikotoka nimepiga Rivers fresh ikabidi nikate Kona ili nigeuze gari kwa mbele Kuna fremu za maduka nilikanyaga Moto kwa nguvu aisee breki siioni nishavurugwa gari ilienda spidi ikagonga nguzo moja ya zile fremu......


Naishia hapa kilichoendelea ni Majanga makubwa😣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…