Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 20,877
- 43,633
Nimecheka kama mtoto mdogo....pole sana nduguAcha hiyo sasa wiki moja baada ya kutoka veta nikajidai teyari nimeshakuwa dereva kwani nilishapata leseni yangu ya mchongo, bwana nikaitwa kwenye interview moja kulikuwa na gari mpya tupu.
Na hata kwenye hiyo interview tulitestiwa na gari mpya... mimi nimeshazoea migari mibovu ile ya veta ukiendesha jinsi tairi linavyozunguka unalisikilizia kwenye stering mikono.... na clutch pia nimezoea zile ambazo nilazima uilazimishe kuikanyaga utumie kanguvu kidogo....kumbe bwana nilikuwa mshamba kuna clutch nyingine haziitaji nguvu kukanya...yani ukigusisha mguu tu imo...ni kama vile umekanyaga sponch la godoro...kwenye ile interview niliaibika sana...
Nimefika kwenye gari nimekutana na kiyoyozi kikali ambacho sikuwahi kuzania kuwa kwenye gari panaweza kuwa na kiyoyozi kama hicho, ile gari haikuwa na muungurumo hata kidogo, gari ilikuwa imewashwa ila kutokana na kuwa nilikuwa mshamba wa magari nilivyoingia nikafanya kitendo tena cha kuiwasha...doh nikaumbuka mbona tena gari haiwaki...hali ya kuwa gari ipo on...ila haina muungurumo hata kidogo....kijasho kikaanza kunitoka....nikaamua kukanyaga clutch kisha nikaweka gia na 1. baadae nikakanyaga na mafuta. clutch ilikuwa nyepesi kama sponchi kilicho tokea niliondoka kwa mwendo kama wanaoondokaga nao wanaoendesha magari ya mashinda....yule jamaa alie kuwa ananifanyia test akatingisha kichwa...nikajua hapa nimesha boronga....akaniambia simama...hata kwenye break napo hali ikawa ile ile....nilikanyaga break kwa nguvu gari ikaslip...hadi abiria wengine wakajibamiza na interview ikaishia hapo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]gari rahisi sana na kulijua gari si kulikimiza
Mkuu kunyoosha sehemu ya pakingi ndio shida kwahiyo nimetoka natembeaa tu sikoni popoete af nilikuwa na mtu yeye nikamuacha fire ndio alikuwa ananielekezaMmmmh, sasa huu uongo ulitokaje home na gari kama haujui hata ku-pack gari?
Sent using Jamii Forums mobile app
duuh basi we ni mzito,ni kweli gari huwezi lijua kwa siku moja ila wiki inatosha pia uzoefu barabarani ni kitu kingine kinacho weza kukuchukua mwezi mzima[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hata pikipiki watu waliniambia rahisi sana unaweza kununua leo na kuendesha leo ( yaani siku hiyo hiyo ) LAKINI kilichonotokeaa baada ya kununua SINORAY mayai cc 150-6 nilikaa wiki mbili hata mita mbili siwezi kusogeza.
Uneshapata mtu wa kulirudisha nyumbani?Mkuu kunyoosha sehemu ya pakingi ndio shida kwahiyo nimetoka natembeaa tu sikoni popoete af nilikuwa na mtu yeye nikamuacha fire ndio alikuwa ananielekeza
Yah nishafika mda
Hapo njema, nilitaka kukushauri umlipe dereva tax akusaidie.Yah nishafika mda
[emoji23][emoji1787]Enzi hizi za hangaya ungepigwa chuma
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] omba mshikaji alirudishe halafu ukiwa free nenda nalo uwanjani panga mawe ya rivasi kushoto na kulia endelea hapo endesha 360 ,, ili usichoke mkono mmoja ,, zunguka uwanjani haswa mikono itachoka kisha itakuja kuzoea hapo ndo utaanza mbwembwe za mkono mmoja na kishoka ,,Bora ingekuwa mkoani ila Dar ngumu sana na jioni nawaza itakuwaje kila mtu anataka kuwahi
[emoji23][emoji23][emoji23] Dah umenikumbusha nimeacha hivi karibuni ilikua niki rudi reverse lazima nivue viatu mpaka nikawa addicted aisee hasa manualNunua laki utaacha wenge by way Mimi nilinunua gari lakini nikawa sivai viatu ili niweze kubalance nafuta vzr
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Amekuja rafki yangu
Hilo nadhani ni wotee maana ukivaa viatu mwanzoni yani Utagongeshaaa balaaa.Nunua laki utaacha wenge by way Mimi nilinunua gari lakini nikawa sivai viatu ili niweze kubalance nafuta vzr
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app