Siku yangu ya kwanza kuingia ofisi za kubeti kwa bahati mbaya

Siku yangu ya kwanza kuingia ofisi za kubeti kwa bahati mbaya

Tukiangalia issue hiyo Kwa jicho la kiserikali,

Kila siku Kila kijana anabet wastani wa 1000 Kwa siku na inaliwa.

Tufanye assumption,

Vijana milioni 20 wanabet Kila siku,

20,000,0000*1000= Trillion 2. Per day., Kwa mwaka ni pesa ngapi?

Hiyo pesa unaenda nje ya Nchi Kutoka JASHO la Watanzania.

Pesa hiyo ingeingia katika banks zetu na vijana wakakipeshwanbila riba kufanya miradi Yao, Nchi ingekuwa wapi?
Word 📌
 
Pesa ya betting Ili vyo na LAANA,

Ukitetereka kidogo, utavuuza vyote Ili urudi kubeti.

Niliona Kwa macho yangu, mtu aliyejenga nyumba kutokana na pesa ya betting akiiuza Kisha kumaliza pesa zote kwenye kubeti.

Mungu atusaidie.
Hazina laana bali hiyo tafsiri hutokana na kiwewe cha mhusika kinachopelekea kuhisi hicho kiasi cha fedha ni kikubwa sana hivyo anakuwa na matumizi yasiyokuwa na tija. Akishituka amebakiwa na sh 250 kutoka 6M.

Sasa anaanza kusingizia laana.
Mimi nikaa siku 3 hata familia yangu na majirani bila kujua na fedha ziko bank,walipoanza kuniuliza kuhusu safari jibu wakuja kulipata nilipowachukua kwenda kuwa mashahidi kipindi ninanunua maeneo.

Utulivu na umakini ni mhimu.
Mimi ni mvuvi na nimepata fedha kiasi kutokana na kazi hiyo lkn pia na shughuri za uchimbaji madini.
Niamini mimi,hakuna fedha inayopatikana kihalali ikawa na laana labda wewe ndiye uwe na laana.

Zingatia matumizi yasizidi kipato,bet kiafya na siyo kama kazi.
 
Betting ni office sema unaitumiaje tu. Mwezi wa kwanza huu nilikuwa na 10,000 tu nikanunua mazaga ikabaki kama 1,500 nikaingia office (Betting) nikachagua timu 13 kwa jero mkeka wa siku mbili nikausikilizia Jumatatu Sina hata mia halafu Kuna Mjinga alikuwa ananidai kama 35,000 hataki hata kuongea na Mimi. Kwenda kuumlulika zote Kijani 277,000 hii hapa. 😂😂😂
Alafu Leo hii Mtu frm no where anakuja anakataza aisee Mimi hata simuelewi
Wana laana wao halafu wanasingizia fedha.
Siyo kila mtu ana kichwa kidogo km wao.
 
Hazina laana bali hiyo tafsiri hutokana na kiwewe cha mhusika kinachopelekea kuhisi hicho kiasi cha fedha ni kikubwa sana hivyo anakuwa na matumizi yasiyokuwa na tija. Akishituka amebakiwa na sh 250 kutoka 6M.

Sasa anaanza kusingizia laana.
Mimi nikaa siku 3 hata familia yangu na majirani bila kujua na fedha ziko bank,walipoanza kuniuliza kuhusu safari jibu wakuja kulipata nilipowachukua kwenda kuwa mashahidi kipindi ninanunua maeneo.

Utulivu na umakini ni mhimu.
Mimi ni mvuvi na nimepata fedha kiasi kutokana na kazi hiyo lkn pia na shughuri za uchimbaji madini.
Niamini mimi,hakuna fedha inayopatikana kihalali ikawa na laana labda wewe ndiye uwe na laana.

Zingatia matumizi yasizidi kipato,bet kiafya na siyo kama kazi.
Kwamba bet kiafya sio😀

Ni sawa tu na dini Ile inayosema kunywa kidogo ila usilewe!!

Yaani sababu Hasa ya kunywa ni ipi ikiwa unakunywa Ili usilewe?

Dunia ni hadaa, walimwengu shujaa.

Kijana, kaa mbali na betting!!
 
Salaam, Shalom!

Siku moja nilitoka nyumbani kwangu nilipanga kwenda mjini kununua baadhi ya mahitaji muhimu ya vifaa vya umeme,

Niliondoka nyumbani majira ya saa tisa hivi, baada ya nusu saa, nilifika mjini, Sasa Pana duka la vifaa vya umeme kubwa nililokuwa nikitumia kununua mahitaji yangu hapo mjini muda mrefu uliopita, nikiwa natembea nikasema, niende duka lile nikapate mahitaji yangu na kuokoa muda.

Nikapaki gari yangu pembeni kidogo ya sehemu lilipokuwapo duka lile, Nilishuka na kutembea kulikaribia duka lile.

Kilichonishangaza, nikakuta mazingira tofauti kabisa, nje Kuna huduma za chakula watu walionekana wanakula na kunywa Kwa furaha.

Nilikuta duka lile limeongezeka ukubwa na kuongewza urefu, nje alikaa afisa wa ulinzi smart, palifungwa camera za USALAMA, ofisi ilinakshiwa kisasa zaidi. Ndani palikuwa na wazungu kadhaa na wafanyakazi waliovalia mavazi nadhifu.

Nikavutiwa kuingia ndani ya ofisi hiyo kujua nini kinaendelea humo, pia nilitaka kujua muuza electronics alihamia wapi,

Kuingia ndani ya ofisi hiyo, nikakuta watu wenye Rika mbalimbali watanashati, wengi walikuwa vijana na wanawake Wachache,

Mle ndani palikuwa na utulivu wa kutosha, AC Kila Kona, kila mtu alikuwa ameshika kalamu na karatasi na alionekana kumakinika na kusoma kilicho kwenye karatasi,

Nikawaza hiki ni nini watu Hawa wanafanya, niliwaza, yaezakuwa wanafanya labda mtihani hivi, niliwaheshimu sana, nilipoona hali Ile, nami nikalazimika kusogea pembeni alipokuwa askari yule wa USALAMA na kuuliza watu wale wanafanya nini, na ofisi Ile inajishughulisha na nini,

Mlinzi yule alinijibu kuwa pale ni ofisi za BETTING, watu wanachukua mikeka kutabiri timu za mpira wa miguu.

Sura yangu ilifura ghafula, nilitoka haraka ndani ya ofisi Ile nikijilaumu kupoteza muda wangu kuingia ofisi ya ulaghai Kwa nguvukazi yetu ya Taifa inayowateka vijana kuamini kuwa maisha yaezapatikana Kwa Bahati nasibu.

OMBI: Atokee kiongozi mmoja mkorofi aina ya Magu, afute Ujinga huu unaopoteza nguvu KAZI ya Taifa.

Haiwezekani mchina anapokea coin Kwa wanafunzi wa shule za msingi mtaani Ili wabet, Taifa tunalipeleka wapi?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.

Amen.
Huwezi kuukwepa utandawazi
 
Kwamba bet kiafya sio😀

Ni sawa tu na dini Ile inayosema kunywa kidogo ila usilewe!!

Yaani sababu Hasa ya kunywa ni ipi ikiwa unakunywa Ili usilewe?

Dunia ni hadaa, walimwengu shujaa.

Kijana, kaa mbali na betting!!
Sijui umeelewa nini niposema kiafya.
Nimesema kiafya kwa maana kwamba isiwe km dozi,isiwe lazima wala mazoea.
 
Mfano wilaya ya Kilolo nimetembea Idete lipo ,bomang'ombe yapo,, ,lulanzi ,kisinga yapo mengi,, inaumiza sana hadi wabibi na wababu wanacheza
Wale wachina wanatokaga Kilolo na kuja hapa mjini wakiwa na ile Kruger yao wakiwa na 20M kila week.
 
Wale wachina wanatokaga Kilolo na kuja hapa mjini wakiwa na ile Kruger yao wakiwa na 20M kila week.
Halafu Serikali inakwenda kuomba mikopo nje ilhali wachina wanaingia nchini na kufukarisha wananchi kupitia betting Kisha wanarudi kwao matajiri!!
 
Nashukuru huu mwez utaisha vizuri.
Screenshot_2024-03-17-09-39-16-658_com.android.chrome.jpg
 
Uzoefu wangu wa kubeti asee huu mchezo mbaya yan ukiweka 5000 afu posibo winning after tax unaona milion moja basi ww unawaza milion tu ile unasahau oabisa kama umetoa 5000 imeenda.... Unachana kesho unaweka tena...

Siku ukila kama unatunza kumbukumbuku za mikeka uliyochana ukatoa ulizopta na ulizoliwa utakuta inakuja hasara...
 
Pesa ya betting Ili vyo na LAANA,

Ukitetereka kidogo, utavuuza vyote Ili urudi kubeti.

Niliona Kwa macho yangu, mtu aliyejenga nyumba kutokana na pesa ya betting akiiuza Kisha kumaliza pesa zote kwenye kubeti.

Mungu atusaidie.
Acha watu wabet ka wewe hubet. Mbona watu wanapokea mishahara na hakuna jambo la maana wanafanya. We mwenyewe umesema ushaona mtu amejenga kwa pesa ya kubet hii tu inaonyesha huko kuna hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom