Wewe hapo hupaswi kunena.
2019 nilitengeneza mikeka yangu mi3,mia 5 kila mmoja.
Ilikuwa siku ya ijumaa nikiwa ninatoka kazini na mshahara kibindoni.
Mingine miwili sina kumbukumbu nayo na siku iliyofuata ilichanika,ukabaki m1 wenye match 24 sawa na teams 48.
Jumapili saa 2 usiku nikaona unaendelea vizuri,zimebaki match 6.
Jumatatu yake ilikuwa nikakate ticket nielekee mkoani Tanga.
Sasa nikiwa njiani hiyo Juma 3,nikaona ngoja niangalie mkeka kwanza,kwa haraka nikaona zimeenda vyema games 23,moja sijaiona.
Nikaona isiwe tabu,ngoja nikae chini nijiridhishe.
Ebuana eee,6,464,276/- hii hapa kwa 500.
Hapo kodi ilishakatwa.
Sema mimi nilikuwaga sikai betting station.
Nilikuwa ninatenga km ni 5000/- kwa mwezi basi.
Ikiisha siongezi,sikuwa nikiitegemea kazi ya betting.
Nilinunua viwanja viwili vya kujenga ndani ya manspaa flani,vipo kimoja nilishaanza ujenzi.