Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Sikubaliani na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali

Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.

Serikali ya Samia Suluhu ninakubaliana kwa 100% na pendekezo la Waziri wa Fedha kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa arudishwe kwenye mshahara wake wa awali​

Mkuu Koryo2, kwanza msome huyu

Mkuu Johnny Sack , kumbe hili wewe ndio umelijua jana!, karibu angalia tarehe ya bandiko hili uone watu tulisema nini na lini
Nilisema

P.
Kuna wakati una hoja nzuri sana, tatizo ukada unakuharibia
 
Yani mfano kama mtu alikuwa mwalimu akateuliwa kuwa DED anakuwa anakula M 3 na malupulupu kibaoooo.Sasa ikatokea paaap akatenguliwa basi anarudi kwenye laki 7 badala ya M 3
Ukisikia mtu kafa kwa msongo wa mawazo ndio hapa sasa,mtoto yupo Feza form two Mara paaap umetenguliwa unarudi kwenye mshahara wa TGS D[emoji3]
 
Ni sawa kabisa ili kupunguza matumizi ya serikali
 
Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.
Mkuu hakika sijaona ubaya wowote wa pendekezo hilo, tena limelenga kuhakikisha kila mmoja analipwa mshahara kulingana na jasho lake, Mpaka sasa kuna watu wengi wanalipwa mshahara wa kazi wasiypifanya, Mfano wakurugenzi wote waliotumbuliwa hata kama awali walikuwa walimu eti waendelee kulipwa mshahara wa mkurugenzi ilihali hawafanyi kazi za wakurugenzi!
Hivi sasa kwenye mikoa na mikoa na halmashauri zote nchini serikali imefuta idara na vitengo kadhaa mfano kitengo cha uchaguzi, hata hivyo wakuu wa hizo idara na vitengo mpaka sasa wanaendelea kuvuta mshahara wa mkuu wa idara ilihali hawafanyi kazi za cheo hiko.
Kwaiyo serikali itakuwa imefanya jambo la maana iwapo itarekebisha kasoro hii. Wengi walikua wakimsifia Hayati Magufuli kwa tumbuatumbua za kila wakati lakini hawakujua kuwa hakuna kipindi ambacho serikali ililipa watu wengi mishahara wasiyostahili kama kipindi hicho cha JPM, Hata utumbuaji wenyewe unakosa maana kama unaemtumbua anaendele kula mshahara kama kawa! Sanasana ilikuwa ni mzigo tu kwa serikali!
 
Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.
Kipimo cha kiwango cha mshahara ama ujira wa mfanyakazi hitegemea aina majukumu ambayo mtu hukasimiwa katika nafasi ya ajira aliyopewa katika muda husika. Ni sahihi mtu akalipwa kutokana na kile alichopangiwa kukifanya katika nafasi na muda husika.

Kama hamisho la mfanyakazi ni "vertical movement" yaani "promotion, demotion or temporary career" basi hupaswa kuongezewa ama kupunguziwa kiwango cha malipo ya mshahara na marupurupu yake. Kwa aina hii ya uhamisho kama huu waziri alikuwa sahihi kabisa kuja na pendekezo kama hili.

Aidha kama hamisho ni "horizontal movement" yaani mtu licha ya kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini bado anabakia na majukumu yanayolingana na nafasi aliyokuwepo, basi hapo malipo yake hupaswa kubakia yaleyale. Hapa pendekezo la waziri haligusi hamisho la namna hii.
 
Ni sahihi kabisaaa

Tena kipindi cha JPM, unachagua kijana miaka 40, unampa mshahara mkubwa, unamtengua, anarudi ofisi yake ya zamani anamzidi boss wake mshahara

Heshima itatoka wapi?
Issue sio heshima,issue ni Tax Payer money ambayo watu wanahaha kuilipa,lakini haitengenezi tija yeyote ile
 
Nimefuatilia hotuba ya Bajeti ya mwaka 2022/2023 na kwenye kipengele kinachosema kuwa kama mtumishi wadhifa wake umetenguliwa basi arudi kupokea ule mshahara aliokuwa anapokea kabla ya uteuzi. Hili ni pendekezo.

Binafsi sikubaliani kabisa na pendekezo hili. Mhe. Waziri usije ukaleta vurugu hapa nchini. Nchi hii tunapendana. Utakuta wengi wanaotumbuliwa ni uonevu.

Wabunge hili ni pendekezo mkatae kwa asilimia mia moja.
Mi naungana na wewe.

Maisha ya watu yatakuwa ya ajabu sana nchi hii.
 
Ok ok sasahivi ukipewa cheo butua kabisa likitokea baya uwe ushajipanga
 
Kwa nini mtumishi wa atenguliwe? Kama amekwenda kinyume na kanuni na taratibu za kazi yake, zipo sheria na kanuni za utumishi. Alalamikiwe, ashtakiwe na akipatikana na hatia aadhibiwe kulingana na sheria. Kama hana hatia arudishwe mahali alipokuwa.
Tatizo mnawafukuza watu kwa mihemuko ya kisiasa na kutaka sifa.
Unapata umbea kuwa mkurugenzi ni Chadema au Chauma,unamuundia visa vya kijinga ili umtumbue.
Wapo hata maheadmasters wameteswa kisa vyama.
Tukitenda haki kwa kuheshimu sheria za utumishi hatutakuwa na shida hizo. Aliyekosea,atashtakiwa kulingana na sheria na siyo kujitamkia kwenye mikutano iliyokusanya watu wenye wivu na roho mbaya. Halafu unawauliza wao,nitumbue, nisitumbue, na yanaitikia,Tumbuaaa!!
 
Hi hoja imekaa vibaya. Uteuzi wa viongozi wa juu unapaswa kufanywa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha mtu sahihi anapatikana katika nafasi hiyo. Ukiona kila kukesha kuna kuteuliwa na kutenguliwa ujue kuna tatizo kubwa, hasa katika uteuzi. Katika hali ilivyo, tunaona mtu anateuliwa, anatenguliwa halafu anateuliwa tena katika nafasi ile ile ! Katika hali hii, huyu mtu atakuwa anapandishwa mshahara leo, kesho kutwa anapunguzwa mshahara halafu anapandishwa tena. Hali kama hii itafanya kazi ya kupata watu makini wa kujaza nafasi hizo kuwa ngumu. Mimi napendekeza yafuatayo:
1. Uteuzi ufanywe kulingana na sifa, uzoefu na vigezo vinavyoendana na nafasi husika. Ikiwa mwalimu wa praimari atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya itakuwa ni kumuonea.
2.Mtu akiteuliwa awe na muda wa matazamio, kama ni uteuzi wake wa kwanza katika nafasi hiyo.
3. Akionekana anafaa basi apandishwe cheo kitaaluma kinachoendana na wadhfa huo. Kama mwalimu anateuliwa kuwa Katibu Mkuu basi apandishwe cheo cha kufikia cheo cha mwisho cha walimu. Kama anateuliwa kuwa Mkurugenzi basi apandishwe cheo kitaaluma kifikie kimshahara wa Mkurugenzi n.k.
4. Mtu akitenguliwa apewe haki ya kukata rufaa katika tume husika. Kama itaonekana kuwa ametenguliwa kwa sababu binafsi tu, apangiwe kazi zitakazoendana na taaluma na uzoefu wake. Kwa vile ataendelea kuwa na cheo alichopewa basi mshahara wake hautaathirika sana.
5. Kama ametenguliwa kwa sababu ya utendaji mbovu, ashushwe cheo, astaafishwe kwa lazima au afukuzwe kazi. Sababu ziwekwe wazi kwa jamii.

Wakati serikali inalalamika kuhusu watu kulipwa mishahara wasiyostahili, ijiangalie na yenyewe jinsi inavyotumia kigezo cha ukaimu kuwatumikisha watu katika nafasi kubwa huku wakiwalipa mshahara wa chini kabisa. Iangalie pia jinsi inavyowatumia vijana kwa kivuli cha kujitolea bila ya kuwaajiri.

Kitu cha msingi ni tusifanye maamuzi ya kuteua watu kutokana na sababu nyepesi nyepesi. Kila wakati tujitahidi kuhakikisha kuwa watu wenye weledi na sifa stahili ndio wanateuliwa kushika nafasi za uongozi serikalini. Aidha, tuhakikishe kuwa watu wanahakikishiwa kuwa watatendewa haki baada ya uteuzi.

Amandla....
 
Yani mfano kama mtu alikuwa mwalimu akateuliwa kuwa DED anakuwa anakula M 3 na malupulupu kibaoooo.Sasa ikatokea paaap akatenguliwa basi anarudi kwenye laki 7 badala ya M 3

Sasa aendelee kulipwa M 3 kwa misingi ipi wakati hicho cheo kilichokua kinamfanya alipwe hiyo M 3 hana tena?
 
Unajua haya yote yamesababishwa na Serikali kwa teuzi zisizozingatia vigezo vya Utumishi wa Umma.Kabla Magufuli hajafanya aliyoyafanya ilikuwa kuna succession plan nzuri vyeo vya uteuzi vikizingatia mambo mengi ikiwemo ujuzi,uzoefu na waledi-wengi ambao walikuwa wanapata ni ambao tayari mishahara yao inakaribiana kabisa na nafasi atakayo pewa,hivyo ongezeko la mshahara lilikuwa ni dogo sana.
Sasa alipokuja Magufuli MTU anachukuliwa akiwa na mashahara wa 700K anakwenda hadi mshahara wa 4M mwisho wa siku akitenguliwa anabaki na mshahara wa 4M.Wakati kipindi cha nyuma anatafutwa MTU ambaye tayari mshahara wake ni 3M na zaidi ili aisongeze wage bill.
By the way wameyakoroga wenyewe wayanywe.
 
Kitila Mkumbo alipoteuliwa katibu mkuu wizara ya maji alikuwa amefikia level ya principal officer?
Kitila Mkumbo alikuwa Professor na Mshaharabwa Professor ni kuanzia 4M,na huku ule wa Katibu Mkuu nao unacheza kwenye 5M so ongezeko linakuwa sio kubwa.
 
Mamlaka ya uteuzi iliyokuteua ikishasema hufai basi inatosha we pisha kiti.

Ulipoteuliwa ukapata salary mpya kwa sababu ya cheo kipya, unapotenguliwa ni sahihi urudi salary yako hakuna cha kuonewa mara kusingiziwa mbona kuteuliwa kwa upendeleo na mishemishe huzungumzii?
Layman speaking sheria inasema atabaki na mshahara wake
 
Back
Top Bottom