Hi hoja imekaa vibaya. Uteuzi wa viongozi wa juu unapaswa kufanywa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha mtu sahihi anapatikana katika nafasi hiyo. Ukiona kila kukesha kuna kuteuliwa na kutenguliwa ujue kuna tatizo kubwa, hasa katika uteuzi. Katika hali ilivyo, tunaona mtu anateuliwa, anatenguliwa halafu anateuliwa tena katika nafasi ile ile ! Katika hali hii, huyu mtu atakuwa anapandishwa mshahara leo, kesho kutwa anapunguzwa mshahara halafu anapandishwa tena. Hali kama hii itafanya kazi ya kupata watu makini wa kujaza nafasi hizo kuwa ngumu. Mimi napendekeza yafuatayo:
1. Uteuzi ufanywe kulingana na sifa, uzoefu na vigezo vinavyoendana na nafasi husika. Ikiwa mwalimu wa praimari atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya itakuwa ni kumuonea.
2.Mtu akiteuliwa awe na muda wa matazamio, kama ni uteuzi wake wa kwanza katika nafasi hiyo.
3. Akionekana anafaa basi apandishwe cheo kitaaluma kinachoendana na wadhfa huo. Kama mwalimu anateuliwa kuwa Katibu Mkuu basi apandishwe cheo cha kufikia cheo cha mwisho cha walimu. Kama anateuliwa kuwa Mkurugenzi basi apandishwe cheo kitaaluma kifikie kimshahara wa Mkurugenzi n.k.
4. Mtu akitenguliwa apewe haki ya kukata rufaa katika tume husika. Kama itaonekana kuwa ametenguliwa kwa sababu binafsi tu, apangiwe kazi zitakazoendana na taaluma na uzoefu wake. Kwa vile ataendelea kuwa na cheo alichopewa basi mshahara wake hautaathirika sana.
5. Kama ametenguliwa kwa sababu ya utendaji mbovu, ashushwe cheo, astaafishwe kwa lazima au afukuzwe kazi. Sababu ziwekwe wazi kwa jamii.
Wakati serikali inalalamika kuhusu watu kulipwa mishahara wasiyostahili, ijiangalie na yenyewe jinsi inavyotumia kigezo cha ukaimu kuwatumikisha watu katika nafasi kubwa huku wakiwalipa mshahara wa chini kabisa. Iangalie pia jinsi inavyowatumia vijana kwa kivuli cha kujitolea bila ya kuwaajiri.
Kitu cha msingi ni tusifanye maamuzi ya kuteua watu kutokana na sababu nyepesi nyepesi. Kila wakati tujitahidi kuhakikisha kuwa watu wenye weledi na sifa stahili ndio wanateuliwa kushika nafasi za uongozi serikalini. Aidha, tuhakikishe kuwa watu wanahakikishiwa kuwa watatendewa haki baada ya uteuzi.
Amandla....