Sikubaliani na watu wanaoamini Fid Q ni genius

Wanaoafiki FID Q ni genius wako sahihi kwa upande wao lakini kwa upande wangu sioni u-genius wake kwa sababu fid q amezezidiwa vitu vingi na ma MC/rapper wengine

Labda tungeJiuliza maswali kablya ya kuanza kumuita GENIOUS

1.Kwani Fid Q ndio rapa/MC mkali Kuliko wote hapa TZ?

Kama jibu ndio

2.Kwa uandishi gani anaomzidi rapa/MC "ONE THE INCREDIBLE" ??

Wasalam!
 
"mnakosea kupick Mc wa kumfananisha na Ngosha". kwa namna hyo hamtang'amua huo "Ugenius".
 
Weeeeeeee fid q ni mkali wao
 
Kwa mfano huo do amekosea? Nenda kijijini watu hawachemshi maji ya kunywa wanakunywa na hawapati shida yoyote kajaribu ww uone matokeo yake.
 
Kweli kabisa.
 
Genius amejibu swali asilolielewa badala ya kuwa muwazi.
 
As The Man Thinketh.....yuko sahihi Fid Q jinsi alivyojibu swali la Niki wa pili. Mtoa mada usitumie taaluma usiyoijua kama point kuu katika kutoa udhaifu kwa kutaka kutetea mada yako. Ijue psychology kwanza n then phylosophy halafu angalia tungo za Fid Q utagundua uwezo alokuwa nao.
 
Yawezekana wanaosema Fid Q sio Genius katika uandishi wakawa na hoja ya msingi au haters tu!.

Kwanini Fid Q anaonekana ni Genius au kwanini sisi wengine tunamuona kuwa jamaa katika uandishi huko juu sana? Ngoja niweke sababu...

1- Mstari mmoja wa Fid Q unaweza kukupa maana zaidi ya 1. tofauti na MC's wengi wa Bongo.

2- Fid Q amejipambanua kuwa msanii anayewakilisha uandishi wenye mafumbo ambayo kama utakaachini kuyatafakari basi lazima ujifunze jambo.

3- Kuna watu wanasema Fid Q sio kitu kwakuwa tu wanaufahamu mdogo wa mambo mbalimbali. Ili kumuelewa Fid Q lazima uwe mfuatiliaji wa mambo mengi sana. Mfano: Hakuna ambaye hakosi labda Zizi kwa DnD, Yangu Self-esteem haitoki kama ripoti za TMZ. (Hapa kama hujui vitu lazima utoke kapa na lazima umponde Fid).

Kama mnasema si Genius labda mnamlinganisha na nani? Kwasababu kiuandishi jamaa hana mtu wa kumlinganisha nae.
 
Wimbo Ambao FidQ Alirap Fresh Na Akaeleweka Ni "Usinikubali Haraka" Aliyomshirikisha Matonya. Nyimbo Nyingine Zote Jamaa Anaimba Kama Ana Kigugumizi Maneno Hayatamkiki Na Kueleweka Ingawa Huwa Anaimba Falsafa Nyingi Alizomeza Kutoka Vitabuni
 
Wimbo Ambao FidQ Alirap Fresh Na Akaeleweka Ni "Usinikubali Haraka" Aliyomshirikisha Matonya. Nyimbo Nyingine Zote Jamaa Anaimba Kama Ana Kigugumizi Maneno Hayatamkiki Na Kueleweka Ingawa Huwa Anaimba Falsafa Nyingi Alizomeza Kutoka Vitabuni
Si bora ungesema katika nyimbo za Fid Q hiyo ndiyo nyimbo unayipenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…