Ndo kitu nilichoshauri jana kwenye haya haya magroup. Imeshatokea wapo wawili. Kwa namna moja au nyingine hawana budi kusameheana. Mke mdogo angemtafuta mkubwa wakae sasa Mzee ameshakwenda, tunamhifadhi wapi? Na tunafanyeje kuhusu shughuli yote hii? Ni yetu sote. Kama Mke mkubwa ana hekima angekaa na kuongea na wangetoka nje wakiwa wamoja. Ukaaji, uvaaji ulionesha hakuna huo utengamano. Tuombe tusiyaone ya mahakama maana mule aibu zote huwa zinaibuliwa. Unaachwa uchi wa mnyama kabisa.Mke Mdogo wa Ndugai , ndo anayetambulika na Serikali Ila kihualisia na mke mkubwa anafahamika na Serikali nikimaanisha wanamjua na anajulikana na viongozi wa Serikali.
Ilibidi wakae nae , waomboleze nae msiba na sio kumtenga.
Ubinadamu ,utu ni muhimu kuzidi Mali , pesa na umaarufu.
Ikiwa huyu mke mkubwa ametengwa katika Msiba je katika Mali itakuaje ?.
Hayo mafao na benefits nyingine anabidi na Huyo mke mkubwa kupata.
Hizi sheria lazima zizingatie utu na ubidamu .