SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

Hiyo ya polisi nina uhakika polisi ndo wenye makosa. Wote wapumzike kwa amani, na majeruhi speedy recovery.
 
Reactions: Lax
Inasikitisha sana.
 
Reactions: Lax
Mfano kwenye hiyo ajali polisi walipokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari lipi?
Sikuwepo mkuu,siwezi kujua. Ila huwa tunawaona madereva wanavyopokea rushwa tena kuna wakati wanalazimisha, wanaona ni haki yao,usipotoa unaandikiwa faini na huna pa kushtaki.
Na kuhusu weledi,kitendo cha magari mabovu kuwepo barabarani ni uthibitisho hao maaskari hawatimizi wajibu wake,ingekuwa maaskari wanatimiza wajibu wao magari mabovu yasingekuwepo barabarani. Hapo bado hatujaja kwenye pikipiki, watu hawavai helmet na polisi wanatazama tu..
 
Watawala wa Tanzania ni watawala wenye majigambo hewa. Ukiwasikia wanavyojisifia, tumefanya hiki na kile, kama hujawahi kutoka nje ya Tanzania, unaweza kufikiria, labda tunaongoza kwa ubora wa kila kitu wakati kila kitu ni hovyo!

Hizi ajali zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na ubaya wa barabara. Barabara ni finyu, zimejaa mashimo na matuta ya ajabu kabisa ya kuharibu magari!

Nenda tu hata kwenye nchi ambazo hazina utajiri mkubwa sana kama Chile, ukaone jinsi barabara zao zilivyo bora na pana. Barabara za mjini kabisa, mpaka zina lanes 10, yaani upande huu lanes 5, na upande wa pili lanes 5. Flyovers, unaweza kupita juu kwa juu bila ya kushuka chini, umbali kama wa kutoka Dar Posta mpaka Kibaha. Bado wana barabara za chini ya ardhi, wana treni za chini ya ardhi. Kaangalie mji kama Santiago ulivyopangwa, hakuna hata sehemu moja utakayokosa parking au kusimama kwa sababu ya msongamano wa magari. Wao, kadiri gorofa linavyopanda juu, ndivyo ardhi tupu inayolizunguka jengo inavyozidi kuwa kubwa. Siyo huu upuuzi wa Tanzania! Halafu eti unaambiwa kuna wasomi wa mipango miji! Miji ambayo hata aliyeishia darasa 7 mwenye akili timamu hawezi kupanga hovyo kiasi hiki.

Hata ukienda baadhi ya nchi za Afrika, kama Botswana au Mali, tena zenye pato la jumla dogo kuliko la Tanzania, miji na barabara zao zimepangwa vizuri, kiasi ukilinganisha na hali ya Tanzania, unaona kabisa TZ ni takataka. Matatizo mengi ya Tanzania hayasababishwi na umaskini wa pesa bali yanasababishwa na umaskini wa akili na dhamira, hasa kwa viongozi wake.
 
Hivi hizi ajali ni mpaka nchi zingine ni hivi 😢

nini kitafanyaika sasa? serikali wakitaka kujaribu kuzipuguza kwa kuwabana madereva kwamba warudi shuleni wanagoma na watanzagiza wanawasapoti maderava against askari br. wengine wakishikwa wanakataa wanaanza kuwashambilia askari kwa mangumi kwamba wao ni "madaktari bingwa" na hawapswi kuguswa na "form 4 failure" i.e police.

ni ngumu sana, dereva wa basi wa tanzagita analalamika kwamba akitoka dar-kgm leseni yake itakuwa imeshajaa points hivyo ni lazima serikali wawarudishie points zao na anatetewa na watanzagiza mpaka siku unaenda zako likizo na familia yako unaendesha kwa kufwata sheria basi au lori inaovertake na kukandamiza na kuua familia nzima halafu tunarudi hapa kuuliza maswali magumu tena ...
 
Wapumzike kwa amani raia waliofariki
Hao polisi waliokufa walale pabaya kulingana na matendo yao ya hovyo
 
Wkati Serikali inatengeneza kanununi kuwabana madereva waligoma na mkawashangilia na kuwapongeza mkiwaunga mkono kukataa kubanwa, haya sasa hata mwezi bado wameshaanza kuuwa abiria
 
Hiyo serikali ingekuwa kweli ina nia ya kupunguza ajali ingejenga kwanza barabara za kueleweka sio huu uozo tunaouita barabara.
Halafu ibadili kikosi cha polisi wa usalama barabarani sio hawa wala rushwa tulionao sasahivi. Hapo ndo tutasema serikali ina nia ya kupunguza ajali. Yaani barabara zimejaa mashimo halafu unasema unapunguza ajali??.
 
Dah! Watu 28 ni familia 28 ziko kwenye majonzi ya kupoteza ndugu zao, Mungu tusaidie
 
Mara wanalalamika polisi wengi barabarani
Wakiachwa tena wanalalamikiwa askari kuwa hawawasimamii yaani.
Madereva hawawezi kujisimamia hata siku moja, wana ujinga mwingi sana barabarani..!!

Basi tu ni vile mambo siku hizi yameparangana kila kitu kinaendeshwa kisiasa na mihemko…!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…