Hakika tamasha limependeza saana.Doa pekee ni pale mdosi (MO ambaye ndiye Muwekezaji mkuu wa Club ya Simba) kama kawaida yao (wadosi) na heshima ya unafiki na uwoga alipotaka kuleta siasa wakati akimtambulisha mgeni rasmi Mh. Zungu (aliyekuwa Mbunge wa Ilala CCM) kwa kumfanyia kampeni na kama haitoshi akaendelea kwa kumfanyia pia kampeni Rais Magufuli. Lakini kwa kuwa washabiki wengi wa Simba ni watu makini na wasioendekeza upuuzi wa ugabochori wakampa za uso kwa kumchunia pale aliposema Magufuri oyeeee. Kama ana akili atakuwa amenyooka kwani inaoneka baada ya kupigwa "spana" katika hizi siku mbili zilizopita kuhusu wapi zilipo 20bil alizotakiwa kulipa kabla kuinunua Simba na sio baada ya kuanza kunufaika na Simba inaonekana amekuwa akitafuta kila aina ya "Platform" ya kumuunga mkono hasa mamlaka za juu kwa kujipendekeza ili kuweka mambo yake sawa