Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Pole kwa Simba kuchapwa,pole pia kwa Man u kuchapwa na Barcelona,nadhani leo hautolala na inavyoonyesha wewe ni mwenyeji wa mkoa wa Mwanza ambao pia leo wamelikosa kombe la Taifa kwa kuchapwa na Mbeya.Pole sana najua leo umelia sana kama kawaida yako.

mbeya ndio kwetu, but match za jana zimesababisha simu zangu ziishiwe charge ghafla
 
simba ushuzi...manchester uharo.
mbaaaav Simba sasa waje kulipa deni ls chapati wanalo daiwa na yule bimkubwa.
 
Haya ndiyo yalimo ndani. Msomali kaiuza timu yetu

Kwa wenye uwezo mdogo wa kufikiria atasema mechi imeuzwa, ila Haikuwa Haki yenu(Simba) Ile nafasi ilikuwa ya TP Mazembe timu yenye sifa zifuatazo:
Mpira Mzuri,
Hawana Majungu kama Simba,
Waliwafunga simba Kihalali ila simba wakaenda CUF kuwawekea MadoA
wanamipango na soka Lao kitu ambacho Simba Hawana!, wao full porojo na roho mbaya

HAIKUWA NAFASI YA SIMBA ILA SIMBA WALIFANYA DHULMA NA NDO MAANA IMEWATOKEA PUANI!

Timu nzima ya simba they are full of Wolokoso!
 
Uchawi wao auruki bahari ndugu hili ndilo tatizo lao
 
Kama mlikuwa hamjui, Friends of Somba wako KIBIASHARA ZAIDI! Chunguza Mnjombaa Utagundua!!
 
Simba nao bwana tatu!
Kheri niwe mshabiki wa Barca kuna ahueni waweza kufa na BP
 
Tumezoea visingizio, kumbuka mpira unachezwa uwanjani na sio mezani.
 
Mmeanza unafiki wenu.....Kumbukeni mpira ni dakika 90 na kanuni zifutwe..TP mazembe walitufunga lakini kanuni hazi kufatwa...kama mnataka soka ichezwe bila sheria/Kanuni pelekeni mapendekezo FIFA
 
Kwa hiyo mlitaka TP Mazembe wachezeshe mamluki halafu sisi tuwachekee kisa mabingwa watetezi au kwa sababu tunawaogopa waarabu?

Kubalini tu Tp walichemka hata kama simba isingeshinda rufaa basi tungejua katika soka letu kumbe hakuna kanuni zipo tu ila hazifuatwi.

Mnaotubeza eti hatuwezi kushinda nje ya Tanzania si bora hata sie angalau tunashinda kwa rufaa na hiyo ni kudhihirisha kuwa tuna viongozi wenye ufahamu.

Kuna timu zingine za Tanzania usajili wao ni mamilioni lakini kwenye mechi za makitaifa ni round ya kwanza tu chali wanarudi kucheza kiduku Tanzania.
 
usiende mbali kote huko, cha msingi hapa ni kuwa Mheshimiwa sana mbunge wa (hivi ni Tabora au sehemu za DSM!?) Rage alijua fika kuwa TP Mazembe wana uwezo na simba wasingeweza kufika popote. Badala ya kuwa patriotic na kuiacha timu ya ukanda wetu ikasonga mbele akakubali kutumiwa na 'Northerners", cha ajabu anajiita mzalendo lakini huu ni muendelezo wa kilichotufikisha hapa, we have a long way to go!
 
Back
Top Bottom