Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

IMG_1104.jpg
 
Naomba iwe kweli, kocha simpendi kabisaaa.
Na dirisha dogo, Ntibanzokiza afurushwee.
Tulipowaambia papatupapatu sio nzuri mkaitetea haya sasa chupi la aibu kichwani limewaganda mnahangaika kulivua...😂
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.
Huu utaratibu wa kuajiri na kufukuza makocha kila mwaka hauwezi kamwe kutengeneza utulivu ndani ya timu. Simba mnatakiwa kubadilika. Wapeni makocha wenu muda wa kutengeneza kikosi cha timu.

Tatizo kwenye timu yenu lipo kwa wachezaji wenu. Wengi wana umri mkubwa (wazee), na hawapati muda mwingi wa kupumzika kutokana na kucheza mechi nyingi ndani ya msimu wa Ligi.
 
Back
Top Bottom