Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Wematafuta wa kumtoa kafara!viongozi ndo wazembe
 
255654363295_status_68e155f8b01844e887b3b319e57577b1.jpg
 
Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Ametolewa kwa sababu zingine, sio kufungwa.
Kwanza bora atokeee, huenda phiri atakua na wakati mzuri uwanjani.

Bado kipenzi chake Ntibanzokizaa naye atafurushwa.
 
Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Kocha hajiamini tofauti na makocha wa timu nyingine kubwa ambao wanawapa nafasi na wachezaji wengine ambao hawakudhaniwa lakini wanakuwa tegemeo la timu.Huyu alikuwa anapanga kikosi kile kile ambacho hata Julio ukimpa kazi atapanga hivyo hivyo mbaya zaidi hakina maajabu zaidi ya kuunga unga.
 
Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
No yule kocha hajui kujilinda Simba hata wakishinda lazima goli la lilambwe!,Kila mechi lazima watiwe kitu kambani iwe na timu yoyote hata timu ndogondogo huoni kuwa ni tatizo hilo..??
Mi naona Tena wamemvumilia sana tu ilikuwa wanasubiri alama kubwa kama hii ya juzi ndo wampe go ahead.. Sasa mara hii ndo watajua shida kocha au sajili zao!.

Yanga ipo on fire now...
 
Yanga sio vzuri kumsababishia mwenzenu akose kula
 
Hebu huko nawee mbilikimoo, mfyuuuuh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acha mitusi bure msiambiwe ukweli...🤣 Kimeliwa kimeliwa tu ..😂
 
Uongozi wa Simba waache Uhuni, inakuwaje wanauza mechi alafu lawama atupiwe kocha? Bado kocha alikuwa anatufaa huyu hakuwa na ubaya wowote
 
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba Yanga yamfukuzisha Kocha Objective na kusababisha kocha Kishingo au Profesa Nabi kurudi Tanzania
 
Back
Top Bottom