Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Japokua mm ni yanga lialia...ila nimesikitishwa sana na uamzi huo(kumfukuza robatinho),sijaona sababu yamaana iliyowafanya wamtimue unless nikama mbuzi wakafara tu au wanatafuta pakudondoshea jumba bovu...hata kama yanga nibora kwasasa ,ila haimaanishi kua simba nimbovu kupindukia tatizo mpira wabongo ..kuna ligi mbili
1.ligi ya simba na yanga(watani)
2.ligi kuu.
.....ukishinda ligi kuu ukafungwa ligi ya simba na yanga unaonekana haufai kumbe unakua umeuingia mfumo tu wa mpinzani...simba kacheza navilabu vikubwa kama ahly,wydadi na kafanya vizuri tu kitakwimu nawalisifiwa...kawafikisha MAKUNDI CCF,bado kafungwa mechi moja tu namtani kati ya saba.....namengineyobmengi mazuri ya robatinho..ngoja aje kocha mwingine mpigike hadi maji muite mma..
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

ye mwenyewe alijua hilo,ndio maana aliwapongeza Yanga kwa mpira mzuri.
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Ufanyike uchunguzi huenda mahasimu waliwapa tip makocha
 
Niwakati pia wakufanya usafi na kwa wachezaji pia kwani ni jipu linalotusumbua..
Simba tuache usajiri wa mazoea sisi ndio..

Tumeifanya ligi ya bongo ijulikanike kwa 80% sasa tunapoelekea wenzetu upande wa pili wanaanza kwenda mbele halafu sisi ndo.
Tunarudi nyuma baada ya kwenda mbele zaidi.

Katika miaka michache nyuma tulianza vizuri
Lakini kasi imepungua yote inasababishwa na usajiri wa mafungu mafungu oneni upande wa pili wanavo sajiri wana muda mchache tu lakini shirikisho wameionja nusu fainali sisi tunaishia palepale ndani ya timu tuna wachezaji wazee na ni walewale miaka nenda rudi..

Nawahakikishia kama dirisha dogo tutafanya uzembe tena basi tusahau kuhusu ubingwa wowote tunahitaji kuudhihirisha umma kwa vitendo kuwa simba ni timu iliyo leta chachu na kulitambulisha soka la Tz huko duniani.
 
Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Wamesahau kocha huyo huyo ndiye waliyetoka kumshangilia kwa kuchuana vikali na giant wa Africa, bingwa wa Africa ( Al Ahly) na kutoshana nguvu.
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

dah,
Hatimae simbwa wamefikia uamuzi wa hovyo uliotarajiwa na wengi 🐒
 
Ametolewa kwa sababu zingine, sio kufungwa.
Kwanza bora atokeee, huenda phiri atakua na wakati mzuri uwanjani.

Bado kipenzi chake Ntibanzokizaa naye atafurushwa.

Kwa pira lile bora tu alipofukuzwa,ishu siyo kupigwa na mtani bali pira la hovyo sana lilikuwa linachezwa.
Yaani simba wa kupaki basi kila mechi?
Simba inakosa clean sheet kweli?

Thank you Robertinho, see you next time.
Kama sio mpira wa Tinho wa kujilinda kila mechi mngeoga mvua ya magoli kama juzi kwa kikosi chenu kile.
Ngoja tuwaone.
 
Back
Top Bottom