Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Unadhani tatizo ni viongozi? Tatizo kuu ni mashabiki kukosa consistency kwenye hoja zetu kwa timu. Kidogo tu mashabiki wanaridhika wanatoka kwenye hoja ya msingi.
Mara nyingi viongozi wa mpira TZ huficha makosa yao kwa kutimua makocha ili kutuliza mashabiki. Tulipotolewa mapema na Galaxy alifukuzwa Gomes na viongozi wakabaki.
Lakini, mwalimu aliweka orodha ya wachezaji anaowataka ila bila maelezo hawakusajiliwa wote. Kocha aliondoka lakini matokeo yalibaki kuwa vilevile hadi leo.
Unaona kabisa Try Again amefeli kwenye hiyo nafasi yake, ila kwa kuwa kocha kafukuzwa basi mashabiki wameridhika na maisha yanaendelea.
Mimi najua Simba ina mipango mingi lakini karibu yote imeishia mdomoni. Uwanja umekwama. Ofisi za club ilikuwa zihamie katika ofisi kubwa zaidi hadi leo ziko palepale.
Nilikutana nao kabla sijasafiri nao wakasema ofisi zinahamia maeneo ya Victoria kwa kuwa pale kwa sasa ni padogo, ila hakuna kitu, kuna maneno tu.
Documentary ya msimu wa Simba ilikuwa itengenezwa tangu tukiwa na Gomes kwenye benchi la ufundi, ila hadi imekuja kutengenezwa na Yanga, yetu bado.
Aziz Ki, Nzengeli na Yao si ilikuwa wawe wachezaji wetu, waliishia wapi? Adebayor na Manzoki? Mipango iko mdomoni tu, na CEO Kajula ndiyo bingwa wa mipango ya mdomoni.
Wengi hamjui kama Nabi ilikuwa aje Simba ila hadithi ni ileile. Ilikuwa wakati ule ambao Yanga ilichukulia ubingwa Mbeya na Nabi alitengwa katika sherehe za ubingwa.
Tukachelewa hadi akaja kuongeza mwaka mmoja na Yanga, tena alikuja kwa kuchelewa. Mwisho tukasaini na yule kocha aliyedumu nasi kwa miezi mitatu tu akiwa na 'Mlete Mzungu'.
Ova