Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Sadly taifa letu liliondokana na hizo ideology siku tulipomfikisha Butiama baba wa taifa.
 
Huyu kijana angeishia kulewa na kuchukua malaya pale Element isingekuwa issue kwa baba yake Simbachawene.

Tatizo linaanzia pale anapotumia mamlaka ya baba yake kuvunja sheria na kuonea wengine, leo yuko exposed, Je pale ambapo hayuko exposed inakuaje, Yeye na baba yake lazima wawe responsible kwa hili iwe wengine wajifunze. TUWE WAKALI KIDOGO KUILINDA KUISHAPE JAMII.
 
Sadly taifa letu liliondokana na hizo ideology siku tulipomfikisha Butiama baba wa taifa.

sisi wananchi ndio wakuzirudisha kuishape jamii, hakuna anayeweza kuzirejeshi zaidi ya sisi raia kuwa wakali ili tuheshimiane.
 
Watoto wa wakubwa hawafi kwenye ajali maana wanatumia magari ya uhakika.
Unategemea ile passo ingeathiri gari ya mtoto wa mteule mlamba asali?
Tunamsubiri mahakamani asipooneka tunajua Kuna mkono wa mlamba asali.
 

Kwani enzi za Nyerere hakukuwa na vigogo? Vigogo wapo nchi hii tangu ipate uhuru. Hakuna usawa wa aina yoyote ulioletwa na Ujamaa. Angalia watoto wa vigogo wanavyorithi madaraka ndiyo utajua hakuna usawa. Labda useme vigogo wa siku hizi wamezidi ufisadi na tamaa nitakubali.

Tanzania ingekuwa nchi ya kibepari ingekuwa na matajiri wengi sana kwenye sekta binafsi. Ungeona makampuni, biashara na viwanda vingi sana kwenye sekta binafsi. Nchi ya watu milioni 60 halafu mabilionea wachache huwezi kusema ni nchi ya kibepari. Na umaskini uliopo nao ni matunda ya sera za Ujamaa zilizoharibu uchumi.
 
Mzazi wangu mmoja ni mwalimu na alikuwa anawafundisha sana tuition hawa "watoto wa wakubwa"; kiufupi hakuna watoto wapumbavu na wasio na adabu kama hawa.... katika 10 ni nadra kukuta 1 mwenye discipline, wengine ni majinga makubwa. Huyu hata mbele ya kamera kashindwa kuficha ujinga wake.
 

Ufisadi na ubepari ni tofauti. Hao wanaotajirika kwenye siasa siyo mabepari. Ubepari ni sekta binafsi. Halafu Ujamaa hauwezi kuleta self reliance kwa sababu Ujamaa unaongeza umaskini. Maskini daima atakuwa omba omba.
 
Self reliance ni kile wanachokifanya urusi, una materials unauza nje unaendeleza nchi. Mengine unachakata bidhaa unauza ndani na kwa majirani.
Huko ndiko kujitegemea.

Serikali inakuwa center of the stage ku control na ku regulate uchumi. Private sector inakuwepo ila inadhibitiwa isifanye mambo ya hovyo kama wafanyayo mitandao ya simu.
Ufisadi na ubepari ni tofauti. Hao wanaotajirika kwenye siasa siyo mabepari. Ubepari ni sekta binafsi. Halafu Ujamaa hauwezi kuleta self reliance kwa sababu Ujamaa unaongeza umaskini. Maskini daima atakuwa omba omba.
 
Kwahio bongo sio bepari ila watu ndio wanaishi kibepari?
 
Yeah, namkumbuka sana RSO mzee mayala alivyojitahidi kuwasave wale jamaa, kipindi hicho mimi nilikua DSO wa sengerema
 
Mh. Simbachawene alipaswa afanye kujiridhisha na upande wa askari. Kutoa ruhusa kumshughulikia kijana wanaweza kimdhulu dogo wafiche ushahidi
 
Hapana, asingesema polisi wangemnyanyasa huyo kijana kama wanavyotunyanyasa sisi kajamba nani, kasema kumaanisha kwamba huyo kijana hajitapi bure, kweli ni kijana wake na atakae mgusa ajiangalie!
Safi kwa kujitambua kuwa wewe ni kajamba nani
 
sikubaliani na ww hata kidogo..kwan huyu aliefanya kosa ni under 18? awajibike kivyake kwa sheria za nchi
 
Umri wangu hauna umuhimu kwenye mada. Nilikuwa Advance akiwa O level. Mpira tulienda wote kutazama na alifanya mambo ya kawaida kabisa ya wanafunzi wengine.
Can you imagine first time nimefika dorm namtazama hivi namuona Simbachawene huyu hapa.
Nimeelewa.! Ila unaonekana ulikuwa mwoga sana kwa huyo dogo, ukizingatia kuwa wewe ni mtoto wa mlala hoi kama ulivyojipambanua.
 
Ni malezi tu wala si kingine. Labda hujawahi kukutana na watoto, ndugu au wake wa viongozi wa CCM. Wengi wana fikra kama za huyu kijana kwamba hawagusiki na ukiwagusa umekwisha. Wahanga wakubwa wa tabia zao ni Polisi na Madaktari.
Kiukweli dogo kamuaibisha dingi wake
 
Ni ngumu mno nakuhakikishia. Yaani mtoto wa bosi hahahah. Yaani hapo Mama mtu akisema tu sitaki mwanangu ateseke hao polisi watakoma. Unakumbuka yule traffic wa Mke wa Dkt Mahiga, unajua kilichomtokea??? Alijuta!
Ni kipi hicho? Dk Mahiga huyu marehemu au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…