Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Simbachawene: Kijana wangu Mshugulikieni hadi awe na adabu kwa mujibu wa Sheria

Nipo upande wa mtoto wa waziri... usitake kujua kwanini
 
A

Ajiuzulu Kwa lipi? Mbna tunakuwa wepesi kuhukumu. Mtoto na ego yake baba ajiuzulu??

Simbachawene ni waziri na mtoto wa Simbachawene ametumia jina la baba yake kuzuia serikali kufanya kazi yake pamoja na kunyanyasa watu.

Mtoto angekutwa mtaani anavuta bangi, mlevi, nk tusingemwambia Simbachawene ajiuzuru, issue ni kutumia jina la baba ambaye ni Waziri kufanya uhalifu na kuhatarisha maisha ya watu.

Simbachawene kujiuzuri ni kuonyesha uwajibikaji wake na kugushwa na tukio la mtoto wake kutumia jina lake kufanya uhalifu.
 
kutochukulia kwetu mambo serious na kuleta mzahamzaha ndio matokeo ya kuwa na shida kila mahala.

Siku tukies serious kama jamii na kuacha mzahamzaha ndio siku hii nchi itanyoka na kupata maendeleo.
 
Ila Mshana buana eti clip imetrend kuliko watani wajadi kweliiiiii???...mlete mdhungu ndo trending wabongo tunamambo yetu aisee
 
Tatizo la huyo mtoto wa Waziri Simbachawene ni kugonga na kukimbia, ingekuwa kagonga na kusimama, hapo tatizo lingekuwa dogo, inaonekana ana malezi mabovu sana huyo kijana.
 
Nimeiona clip inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii , nakiri kuwa huyo ni kijana wangu ambae ni mtu mzima anajitegemea na anafamilia yake….

Nimemwagiza Mkuu kituo kwa sababu amekosa adabu kwa jeshi la polisi na ametenda kosa la usalama barabarani ASHUGHULIKIWE BILA HURUMA KWA MUJIBU WA SHERIA … Binafsi naomba RADHI SANA kwa walioathirika na mkasa huo lkn pia kwa jeshi la polisi na Watanzania wote.

POLENI KWA USUMBUFU WOWOTE MLIOUPATA

George B. Simbachawene (mb).
View attachment 2329436
Ninajambo gumu sana naliona litakuja kuleta madhara makubwa ambayo itapelekea kuikosa Tanzania kabisa lakini naokopa kulitaja
 
Hili ni tukio la kawaida. Limekuzwa kwa sababu ni mtoto wa waziri...
Magari yanabutuana kila cku Dar na watu wanakula kona.
Mwenyewe kafanya kosa alafu kabla hajaulizwa anatoa utambulisho yeye mtoto wa waziri simba....kwangu mm hili nikosa kubwa inaonesha nijinsi gani anapokuwa nahuyo wazir hawapeani mipaka kuwa waziri nimali yauma kupitia kosa hili ilikuleta umoja kuondoa zana hiyo kwa watoto waviongozi wengine kwa wananchi nashauri mh waziri kwakujuwa nafasi hiyo ni yaumma nasio yafamilia yake ajipime au atafakari na achukue hatua bado nasubiri busara zake waziri
 
Behind the door wenzake walimshughulikia. Unajua iko hivi, kila mtu anataka kujipendekeza, huyo mtoto wa Simbachawene kitakachoenda kutokea ni afisa mmoja tu tena anaweza kuwa IGP akaamrisha dogo aachwe na akampigia waziri tunaomba utusamehe na hapo hao traffic kibarua kipo hatarini. Yaani hao polisi hawakutumia hekima. Ni muhimu walipaswa baada ya kujua wawasiliane hata na baba yake kwa sababu ni waziri then kimya kimya wanamaliza zali. Hiyo ya mapicha video, wamuulize mwenzao kilichomtokea.
Ukweli Traffic wamekosa busara, kimakusudi wanamdhalilisha waziri

1. Just baada ya kujua ni mtoto wa bosi wao wangemsweka ndani, kumwepusha na macho ya umma wasingeruhusu mabishano yeyote then kimya kimya wamfikishie ujumbe baba yake .....naamini Simbachawene angewatengenezea magari na kuwapa fidia waathirika na hii issue isingekuwa public, that is how you should shield your Boss.
 
Usitetee basi kama haujaona clip za kutukuna za huyo mtoto, narudia tena waziri kuomba msamaha sio kwamba kusema anawatahadharisha bali aibu aliyoipata si nzuri kwake.
Hajatetea ila ni ukweli kuwa baada ya waziri kukiri na kuomba radhi Kwa upande mwingine hyo ni very serious warning Kwa wale askari.na asikudanganye mtu dam nzito kuliko maji mkuu.
 
Ila wakati mwingine polisi wanamaudhi sana, usipotumia busara na HEKIMA unaweza kujikuta kwenye matatizo mazito bila sababu.

Kuna siku nimesimamishwa Posta, nikaambiwa barabara gari haziendi huo upande nnaopita, nikamuuliza kibao au maelekezo Yako wapi? Kama mtu ni mgeni atajuaje? Akaanza hiyo inajulikana, nikamuomba msamaha kwamba kazi yake ni kunielekeza na hapo ameshanifundisha, akakomaa kuendelea kunipigia makelele. Nikamwambia Sasa sheria inasemaje? Akasema twende kituoni, nikamuuliza, utaratibu ukoje, tunaacha gari hapa mnanichukua, au mnapanda kwenye gari yangu? Dah! Hilo likawa kosa, wakaita defender , ilupofika wakanigeuzia kibao nimewadharau nimekwambia wachafu, hawawezi kupanda kwenye gari yangu.

Kwa vile haikua mbali na kituo Cha traffic pale central na nilikua na mtoto, nikawaambia ntatembea Hadi kituoni.

Kufika pale boss wao anawauliza shida Nini, wakanipa maelezo ya uongo Tena kwamba nimewafanyia fujo. Nikatoa maelezo yangu na kuwaambia kama nalipa pesa wanipe risit mchana huo nasafiri sitaki mambo ya kufuata risiti kesho. Uzuri sikupanic Wala kuwarusha maneno yoyote yaliyo nje ya kosa langu licha ya kunichokoza niingie kwenye huo mtego.

Hawa jamaa wanakera sana. Lakini hapohapo Kuna wachache wanajielewa sana.
 
Baba yake angeagiza kuwa Anyongwe kabisa ningemuona wa maana, ila kwa Kuagiza kuwa ashughulikiwe naona nae Akili zake pia zinatakiwa Kushughulikiwa vile vile kwani hazijamkaa sawa.
Anyongwe Kwa kosa gani mkuu mbona kama umevurugwa
 
Back
Top Bottom